SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

14 Tweets 48 reads Mar 25, 2023
UZOEFU WANGU KATIKA BIASHARA YA KILIMO CHA MPUNGA
Najua watu wengi sana wakisikia KILIMO wananyong'onyea, ht hamu ya kujifunza inapotea kbs, lkn nikuhakikishie hupaswi kuIgnore huu uzi.
Nitatoa mrejesho wng binafsi wa miaka minne ktk kilimo cha mpunga mkoani Morogoro.
Thread
Ktk kipindi siwezi kukisahau maishani mwangu ni May 2016, nilikua ni finalist UDSM lkn nililima hekari 43 za mpunga kijiji cha Mngeta, wilaya ya Kilombero
Niligharamika 20M, shamba lilienda vzr mno, mpunga ulifunga, mvua zilikubali, cha kushangaza nikavuna gunia 11 tu. Nilichoka
-Nilikua natoa wapi hela zote hizo wkt bado ni mdogo (Uzi wa siku nyingine)
-Niliwezaje kumanage biashara wkt ni mwanafunzi (Uzi wa siku nyingine)
Loss ya mpunga ilikua ni 1 ya hasara nyingi nilizopata 2016, ikiwemo kutapeliwa broilers 6300 weny thaman ya 34M (uzi wa siku nyngn
Baada ya hayo matukio ya 2016 nilikua broke vby mno. Huu mwaka nilijifunza vitu vingi sana, elimu niliyoipata nikaona hata elimu ya darasani haina content, nikaDrop out wiki 3 kabla ya UE ya mwisho
The next year 2017 sikufanya sana kilimo, lkn I was still in touch.
Uzi sasa ndo unaanza
Sept 2017 nikafika Morogoro kijiji ki1 kinaitwa Kisaki. Km kawa, penye miti mingi hakuna wajenzi. Mashamba yapo makubwa, mto usiokauka upo, climate iko safi, lkn hkn wakulima
Nikalobby serikali ya kijiji nikapatiwa pori la heka 60. Baadae nikaongezewa 20
Nikaleta wataalam wa kilimo kutoka JKUAT, wakanishauri kibiashara nitumie SARO 5 TDX306. Msimu wa 2018 nikalima hekari 35, nikavuna gunia 457, nilikuja kuuza mwezi wa 11 mwishoni gunia 1 TZS 95,000
Nikapata morale baada ya yale matokeo. Msimu uliofata mwaka jana nikalima heka 90
Msimu wa mwaka huu tuliomaliza kuvuna juzi nililima heka 170, naweza kusema ni msimu wng bora zaidi na ndo umenisukuma niandike huu uzi; nadhani elimu hii ilibidi iwe compulsory mashuleni/vyuoni
Ukiwa resilient, focused na una taarifa sahihi, kuna pesa nyingu sn zimelala shamban
HATUA MUHIMU NA GHARAMA KWA ACRE 1. Nitakupa specific costs ninazoingia mimi binafsi
1. Kukodi Shamba - 0.00 (shamba langu)
2. Kulima - 32,000 (Trekta langu)
3. Kupiga harrow - 25,000 (Trekta langu)
4. Mbegu - 25,000
5. Kuandaa kitalu na kung'olea - 40,000
6. Kupanda - 90,000
7. Palizi - 30,000
8. Mbolea - 90,000
9. Ndege/Ulinzi - 10,000
10. Kuvuna - 40,000
11. Kusomba - 20,000
12. Kuchambua - 40,000
13. Miscellaneous - 50,000
Jumla: 492,000
Baada ya mavuno kuna gharama za usafirishaji, kununua magunia na kuhifadhi endapo hutouza shambani
MAPATO:
Kwa mbegu ninayoitumia msimu wa mwaka jana nimevuna kwa heka 'on average' gunia 16, msimu huu nimevuna gunia 17
Kuna wanaovuna hadi gunia 23, na kuna wanaovuna hadi gunia 13
i) Ukiuza shambani mwaka huu bei ni 50K. Kwa heka ningepata 850K, faida 368K
ii) Ukihifadhi na kuuza kuanzia late Nov - April bei hua inafika hadi 105K. Kwa heka inaweza kuwa 1,785,000, faida ni 1.3M
Msimu huu umekua wa neema sana, mavuno yamekubali so scarcity ya mpunga/mchele inawesa kuwa chini, so the price. Nategemea iwe 90K kwa gunia at peak
CHANGAMOTO
1. Kilimo chochote ni 'arbitrage' kwa lugha nyepesi tuseme kamari. Mvua isiponyesha unaliwa kichwa, mvua zikizidi unaliwa kichwa, mvua baada ya mavuno unaliwa kichwa
2. Nguvu kazi. Fanya ufanyavyo ila hawa jamaa lazima wakutese tu
3. Usimamizi. (Uzi wa siku nyingin
4. Nguruwe pori. Tunapambana nao wote, so ulinzi wa shamba lazima uwe makini
5. Price fluctuations. Bei ya mazao haitulii, inaweza kukunyanyasa ama kukunyanyua. Mwaka ambao sikulima 2017 watu waliuza gunia 80,000 shambani
6. Changamoto zingine ni za mtu binafsi. Zinazozuilika
Nisingependa uzi uwe mrefu uanze kuwa kero.
Tufanye hii PART 1. Thrn tuwe na;
PART 2 -Mbinu za kumaximize faida na kumanage calculated risks & losses
PART 3 -Masoko ya uhakika ya Mpunga kuepuka kula hasara
Tutaendelea kujifunza kdg kdg
Tuna jambo letu shambani, mpk kieleweke

Loading suggestions...