REGINALD ABRAHAM MENGI
Jina Mengi si geni masikioni mwa Watanzania, awe anaishi au kijijini au mjini. Mzee Mengi alikuwa mtu wa watu, tajiri aliyetoa kiasi ya mali zake kuwapa faraja wasiokuwa nacho. Mungu si Athumani ndo waweza kusema, kwani mnamo tarehe 2/5/2019

Taifa la Tanzania lilipokea habari za mshtuko juu ya kifo cha tajiri huyu toka Kanda ya Kaskazini. Mwili wake ulipumzishwa kijijini kwake Machame, huku msiba wake ukiacha simanzi na vilio kwa jamii nzima.
Baada ya taratibu za mazishi kama ilivyokuwa kawaida, kiliiitishwa kikao cha familia (yaani familia ya Marehemu Mengi) kujadili mustakabari wa kesho yao bila Mengi. Familia na watu wa karibu walipatwa na mshtuko wa pili, walipokutana na kile kilichoitwa Wosia
aliouandika marehemu Mengi, hawakushangaa kwa sababu ni ajabu Mengi kuacha wosia, hawakushangaa kwamba ni ajabu wosia ule kusomwa kwenye kikao cha familia, kilicho washangaza ni kile kilichokuwa kimeandikwa ndani ya ule wosia.
Turudi Nyuma kidogo, Mzee Mengi alifunga ndoa na mke wake wa kwanza Mercy Anna Mengi mwaka 27/11/1971 na Mungu aliwabariki watoto watatu ambao ni Regina, Rodney na Abdiel ambaye baadaye waliachana kwa kupeana talaka. Mama alifariki 31/10/ 2018 Nchini Afrika Kusini akiwa kwenye
matibabu akiwa na miaka 70.
Baada ya kuwa ameachana na mkewe wa kwanza mzee Mengi alianza mahusiano na mrembo Jacquiline Ntuyabalirwe kuanzia mwaka 2011 na walifunga ndoa ya Serikali Halmashauri ya Manispaa Kinondoni mwaka 2015 na baadaye kufanya harusi Nchini Mauritius.

Katika maisha yao ya ndoa walibahatika kupata watoto wawili mapacha, ambao walizaliwa kabla Jack na Mengi hawajafunga ndoa.
Wosia ulioletwa mbele ya kikao cha familia ulimrithisha mali zote mke wa marehemu Jack pamoja na wanawe mapacha, huku ukiawaacha watoto wakubwa wa marehemu bila kitu chochote. Baada ya siku kadhaa watu waliojinasibu kama wasimamizi wa mirathi waliotajwa kwenye wosia wa marehemu
walifungua shauri la mirathi lililopewa namba 39 la mwaka 2019, likawa chini ya Mheshimiwa Jaji Mlyambina. Watu hao ni Benson Benjamin Mengi, William Onesmo Mushi, Zoeb Hassuji na Sylvia Onesmo Mushi. Kama ilivyo kawaida,w walitakiwa kupeleka tangazo kwenye gazeti ili kuwapa
watu wote wenye pingamizi waweze kulileta mahakamani. Hazikupita siku, watoto wakubwa wa marehemu wakiongozwa na Abdiel Reginald Mengi na Benjamin Abraham Mengi waliweka zuio mahakamani, wakiitaka mahakama isiendelee na shauri hilo la kuwateua kina Mushi na wenzake kama
wasimamizi wa mirathi ya marehemu Mengi kwa sababu kuu sita zifuatazo.
1. Wosia siyo halali na sahihi iliyoko kwenye wosia haifanani na sahihi za marehemu Mengi (fake signature)
2. Wosia haukushushudiwa na ndugu yeyote wa marehemu au mke wa marehemu (Jackline).
3. Marehemu hakuwa

na uwezo wa kutengeneza wosia kama ulivyoletwa mahakamani, kwani kwa hicho kipindi ambacho inadaiwa marehemu alitengeneza wosia hakuwa timamu kiafya na kiakili (17/8/2017)
4. Wosia umewanyima haki ya kurithi watoto wa marehemu kinyume na tamaduni za kichaga na bila kuwahusisha
4. Wosia umewanyima haki ya kurithi watoto wa marehemu kinyume na tamaduni za kichaga na bila kuwahusisha
wanafamilia. Ili kuweza kuisikiliza na kuamua hii kesi mahakama ilitengeneza hoja za msingi ili kuiongoza kufikia maamuzi sahihi. Hoja hizo ni
1. Kama wosia uliotengenezwa tarehe 17/8/2017 ni wosia halali
2. Kama wosia uliandaliwa ipasavyo
3. Kama waleta maombi wapewe mirathi au
1. Kama wosia uliotengenezwa tarehe 17/8/2017 ni wosia halali
2. Kama wosia uliandaliwa ipasavyo
3. Kama waleta maombi wapewe mirathi au
waliokweka zuio ndo wapewe barua ya usimamizi wa mirathi. Mahakama ilianza kuwasikiliza waleta maombi na kwa kuanza Silivia Mushi alisema alianza kufanya kazi na Mengi mwaka 2007 na alikuwepo siku wosia uliposainiwa na marehemu. Kwamba wosia huo ulimteua yeye kama msimamizi wa
mirathi japo hakujua kilichokuwa kimeandikwa kwenye huo wosia, kwa sababu wakati Marehemu Mengi anasaini, yeye hakupewa nafasi ya kuusoma huo wosia. Kwa updande mwingine watoto wa Marehemu, waliiomba mahakama iutupilie mbali wosia ulioletwa mahakamani, kwa sababu haukidhi matakw
ya kisheria na hivyo kuwachagua wao kuwa wasimamizi wa mirathi ya marehemu baba yao. Ili kuweka usawa, mahakama iliamua kumuita mke wa marehemu pamoja na aliyekuwa daktari wa Marehemu kutoa ushahidi. Kwa upande wake Jack alikiri kuwa mke wa ndoa wa marehemu na kwamba marehemu
alianza kuugua mwaka 2016 alipopatwa na stroke, akapelekwa kwenye matibabu Afrika ya Kusini na alikuwa ameanza kurejea kwenye hali yake ya kawaida, aliongeza kuwa Marehemu hakuwahi kupoteza uwezo wa kumbu kumbu, hivyo aliiomba mahakama iupokee wosia kwani uliandikwa kipindi akiwa
timamu, kwa upande wa daktari aliiambia mahakama kwamba Marehemu alikuwa anasumbuliwa na magonjwa makuu matatu ikiwemo pressure. Aliongeza kuwa Marehemu hakuwahi kuwa na tatizo la akili. Baada ya mchuano mkali wa hoja na vielelezo mahakamani uliodumu kwa takribani mwaka na nusu,
Mahakama ilitoa maamzui kwamba wosia ule ni batili kwani haukukidhi matakwa ya kisheria, ikiwemo kutorithisha watoto wa marehemu bila sababu, kutoshuhudiwa na ndugu wa marehemu, pamoja na kugawa mali zisizokuwa za marehemu.
Mahakama iliamua kuwateua bwana Abdiel Reginald Mengi na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya marehemu, na kuutupilia mbali wosia ulioletwa mahakamani na wlaioitwa (Strangers) yaani watu wasiokuwa na maslahi kwenye mali za marehemu
Ikumbukwe kwa walioleta shauri hilo ni pamoja na mtu wa mapokezi wa kampuni ya IPP, Msaidizi binafsi wa marehemu, Karani wa Kampuni ya IPP pamoja na Mpwa wa Marehemu. Hawa wote kisheria hawawezi kusimamia mali za marehemu ikiwa, marehemu ameacha watoto, mke au mume na ndugu wenye
akili timamu kama ilvyokuwa kwa Mengi.
NINI HATMA YA JACK?
Kimsingi Jack hajapoteza bado, Jack bado mahakama imeendelea kumtambua kama mke halali wa marehemu, lakini pia watoto wake wametambulika kama watoto halali wa marehemu, hivyo basi bado ana haki zake kama mke wa marehemu

na atarithi kadri kama mke wa marehemu, kitu pekee alichopoteza ni kwamba hawezi kurithi mali zote peke yake kama woisia ulivyokuwa unasomeka.
JE JACK ANAWEZA KUKATA RUFAA?
Hapana Jack hawezi kuyakatia Rufaa maamuzi haya kwa sabbu yeye hakuwa miongoni mwa wadaawa(parties) kwenye
JE JACK ANAWEZA KUKATA RUFAA?
Hapana Jack hawezi kuyakatia Rufaa maamuzi haya kwa sabbu yeye hakuwa miongoni mwa wadaawa(parties) kwenye
kwenye kesi ya msingi, hivyo kama anajihisi kutoridhika na maamuzi ya mahakama anazo nafasi kuu mbili za kudai haki yake nazo ni;
1. Marejereo (Revision) Mahakama ya Rufaa, hii ni haki anayopata mtu yeyote ambaye hakuwa mdaawa(party) kwenye kesi ya msingi, lakini maamuzi ya kesi
1. Marejereo (Revision) Mahakama ya Rufaa, hii ni haki anayopata mtu yeyote ambaye hakuwa mdaawa(party) kwenye kesi ya msingi, lakini maamuzi ya kesi
ya kesi hiyo yamemuumiza au yanagusa maslahi yake
2. Haki ya pili, ni kusubiria mirathi igawiwe na walioteuliwa na mahakama ndani ya miezi 6 kuanza tarehe 18/5/2021, ikitokea akapewa mgawo ambao atakuwa hajaridhika nao, basi Jack anayo haki ya kuwafungulia kesi ya madai,

wasimamizi wa mirathi (Personally) walioteuliwa kwa kushindwa kugawa mali za marehemu kiutaratibu au kwa kutompa kiasi anachostahiki.
Loading suggestions...