Mjasiria Habari
Mjasiria Habari

@Mjasiriahabari

31 Tweets 2 reads May 25, 2021
Ktk kusherehekea siku ya Afrika #AfrikaDay2021 tumeona tuje na uzi maalum ukichambua historia ya bunge la Tanzania lilivyoanza ikiwemo masuala ya msingi ya uhalali wake
Lengo ni kujaribu kuona nini haswa ndio kikwazo cha maendeleo ya Afrika kwa ujumla wake kwa kupitia Tanzania
Ikimbukwe Tanzania ni moja ya nchi zilichangia upatikanaji wa uhuru kwa mataifa mengi barani afrika, kwenye uchambuzi wetu pia tutajaribu kutizama juhudi hizi za Tanzania zilisukumwa na nini? Je Tanzania ilkuwa inasambaza uhuru maalumu au ilisambaza mfumo wa uhuru wake?
Fuatana nasi kwenye #UziZindushi
👇
"Uhuru wa bendera ni hatua ya kwanza tu katika ukombozi wa Afrika. Hatua ya juu kabisa ni umoja kamili wa bara la Afrika. Hapo tu ndipo bara linaweza kufikia uwezo wake kamili, kufikia maendeleo ya maana na ustawi. "Afrika lazima iungane au iangamie". - Kwame Nkrumah
Kati ya vitu ambavyo vinaweza kuwaamsha Waafrika ni kujua historia yao, kujua wapi wametoka na wapi wanaelekea. Kila mwanaafrika anapaswa kufahamu kiunagaubaga asili ya nchi, serikali na watawala waliopo na wapi wametokea.
Ni jukumu la kila mwaafrika, Wtznia wakiwemo kujua historia ya viongozi wao wanaoambiwa ndio waasisi wa mataifa, wanaoitwa waasisi na wapigania uhuru. Kujua hadhi na majina yalitokea wapi, nani aliwapa na kwa sbb gani?.
Huwezi kuzungumzia maendeleo ya Tanzania au Waafrika ikiwa hujui, hujawahi kufuatilia historia, kujiuliza haya au yanayohusiana. Huwezi kujiita mwanaharakati au mwanamabadiliko au mfuasi wa siasa za mageuzi ikiwa hujui historia ya mifumo inayotawala na ilipoanzia au kutokea.
Vivyo hivyo ukiwa ni kiongozi au mfuasi wa siasa za vyama mbadala na hujawahi kujiuliza na kujielimisha asili ya chama chako, viongozi na waasisi, agenda na sera husika ikiwemo sabb na historia yake ni wazi utashindwa kuisaidia jamii yako na hata chama chako na taifa kwa jumla.
Msingi wa mtazamo huu ni pale nilipomsikia spika wa bunge la JMT akiwa anamuapisha katibu wa bunge mteule, kwenye kutaka kueleza historia aliuliza kuhusu historia ya bunge la Tanzania lilianzishwa lini?
Hali iliyotokea pale mpaka kupatikana kwa majibu ilituachia maswali zaidi sisi wengine kuliko historia yenyewe. Hilo spika kutojua mwaka ambao bunge lilianzishwa tulichukulie ni utu uzima na kusahau zamani alikuwa anakumbuka!
Kipande kilichonishtua ni kusikia kuwa bunge hili linanza nyuma zaidi kuliko tarehe na mwaka ambao tumepata "kinachoitwa" Uhuru 9 Desemba 1961. kihistoria na kisheria linaanza tarehe 18 June 1926 ambayo ndio siku sheria hiyo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali Tanganyika.
kwa mujibu wa historia bunge hili lilianzishwa na wakoloni wa Kiingereza chini ya sheria iliyotungwa na bunge la Uingereza na wakati huo lilitambulika kama "Baraza" ambalo lilipewa "mamlaka" ya kutunga sheria kwa ajili ya Tanganyika wakati huo hatukua na kinachoitwa Tanzania.
Sheria hiyo ilitangazwa katika gazeti la Tanganyika mnamo tarehe 18 Juni 1926.
Tarehe 7 December 1926 liliundwa Baraza la mwanzo likiwa na wajumbe 20 chini ya Uenyekiti wa Gavana wa Tanganyika, Sir Donald Cameron.
Na ilipofika 1953 Spika wa kwanza aliteuliwa kuchukua nafasi ya Gavana kama Mwenyekiti wa Baraza. Na hii ikawa Ofisi ya Spika wa kwanza mnamo 1 Novemba 1953.
Uchaguzi wa pili wa Baraza ulifanyika mnamo 1960.
Chaguzi hizi zilikuwa sehemu ya maandalizi yaliyofanywa kuifanya Tanganyika kuwa taifa huru.
Wanachama wote walioteuliwa na Gavana walifutwa na watu wa Tanganyika waliruhusiwa kuchagua wajumbe wote wa Baraza.
Katika mwaka huo huo, jina la Baraza lilibadilishwa kuwa Bunge. Mabadiliko yaliyofanywa mwaka huo yalikuwa ya lazima kikatiba ili kumruhusu Rais wa Tanganyika kuidhinisha sheria zote zilizopitishwa badala ya Malkia wa Uingereza.
Kwa ufupi hii ndio historia ya @bunge_tz na kwa ujumla wake ndio msingi uliojengwa kuelekea kuanzishwa kwa nchi ijulikanayo kama Tanganyika na baadaye kama lilivyobadilishwa baraza na kuwa bunge ndivyo hivyo hivyo Tanganyika ikabadilika kuwa Tanzania kupitia sheria za bunge hilo
Ili twende sawa hapa chini tutaanza uchambuzi na maoni ya kisheria juu ya historia, muundo, na uhalali wa bunge lenyewe na kisha kinachoitwa uhuru ambao uliridhia kuanzishwa kwa nchi ya Tanganyika
Japokuwa hatuna koti na kilemba cha #Uanasheria kwa maana inayotumika kuhalalisha ukosoaji na maoni ya kisheria bali tunafanya kupitia wa kibali cha uchangiaji wa maoni ya kisheria kwa kuzingatia sheria ya kuwatambua wanasheria inatokana na msingi wa bunge husika......
Bunge ambalo uchambuzi huu unalenga kupima uhalali wake kabla ya kutambua uhalali wa sheria ilizotunga.
Kwa lugha nyingine uchambuzi na maoni ya kisheria tunayotoa ni zaidi ya sheria na wanasheria kwa sbb tunachambua kile kinachowapa uhalali kabla ya kuwepo wao na hata sheria
Kwenye kuanza uchambuzi tutaangalia mambo ya msingi yafuatayo ili kuweka msingi wa maoni yetu.
➡️ Kauli ya spika inabeba ujumbe gani?
➡️ Bunge likiwa lilianza kabla ya Uhuru nini maana yake kwa uhuru tunaoambiwa?
➡️ Je watanganyika walihusika kuamua mustakbali wao?
➡️ Je sheria ambazo zilikuja kuizaa Tanzania na ambazo bunge lilirithi kutoka baraza la wakoloni zinapaswa kufuatwa na watanganyika?
➡️ Je uhuru ni kweli?
➡️ Nani mwenye mamlaka ya Tanzania tulionayo hivyi sasa kwa mujibu wa sheria?
Haya ni baadhi ya maeneo ambayo tunalenga kujikita ktk uchambuzi wetu huu ambao utakuwa na shemu tatu au zaidi kulingana na mada zitakazoibuka kwenye uchambuzi wenyewe.
Swala la msingi kulielezea ni juu ya historia iliyotamkwa na spika kuwa bunge letu Tanzania linaanzia 1926 kwa kutamka hivyo spika maana yake anatuambia kisheria bunge hili ni la mwaka 1926 kabla ya uhuru.
Pili kauli hiyo ya spika ni kutuambia sheria zetu hazianzi pale tulipopata uhuru 1961 bali nyuma zaidi karibu miaka 36 kabla ya uhuru.
Tukianza na kauli ya spika, inayotukumbusha kuwa @bunge_tz lilianzishwa mwaka 1926 kama msingi wa uchambuzi hatuna budi kukubali kuwa zipo sheria, kanuni, taratibu na mifumo inayotutawala inayotokana "UKOLONI".
Ikiwa ndivyo, hii ina maana moja kubwa, Bunge lilianzishwa na wakoloni, sheria na taratibu zilizotungwa na bunge hilo ni za kikoloni na hakuna namna tunaweza kubadili sheria hizo na mifumo kuwa sheria na mifumo iliyotungwa na watu huru.
Hatuishii kwenye sheria pekee yake bali hata uendeshaji wa kinachoitwa serikali nao una walakini wa uhalali wake zaidi ya kusema bado tunatawaliwa na #Wakoloni kwa kupitia mkono wa nyuma uliowaweka #manyapara kwa niaba yao.
Sababu ya pili inayopaswa kutizamwa. Ikiwa bunge ambalo ndio mhimili wa utungaji sheria sio bunge lililoanzishwa na watanganyika huru, sheria na kanuni zilizoanzisha zilitungwa na wakoloni haiwezekani tukawa na serikali huru na ya halali itokanayo na ridhaa ya watanganyika huru.
Huu ndio mtazamo na maoni ya kisheria juu msingi wa kuanzishwa bunge ambalo baadaye lilikwenda kuizaa serikali ya Tanganyika na kisha serikali hiyo ikapewa mamlaka ya kuwatawala watanganyika.
Na baadaye tena serikali hiyo ikajibadili na kuanzisha serikali nyingine iliyoitwa Tz
#SehemuyaKwanza
Kama tulivyosema awali UziZindushi utakuwa mrefu na wenye sehemu tatu au zaidi kulingana na mahitaji na mada zitakazoibuka hii ni sehemu ya kwanza.
Ikiwa umesoma mpaka hapa tunasema.
#HappyAfricaDay2021

Loading suggestions...