ClassMonitor👩‍⚕️
ClassMonitor👩‍⚕️

@DaktariWawatoto

16 Tweets 1,390 reads Jun 15, 2021
Fahamu ugonjwa wa Masundosundo au Kuota Vinyama Sehemu za Siri na Sehemu Mbalimbali za Mwili
(GENITAL WARTS)
⚕️MASUNDOSUNDO / GENITAL WARTS
NI vinyama Laini Vidogovidogo Vinavyoota Kwenye Ngozi au Kwenye Utando Laini Unaozunguka Maeneo ya Sehemu za Siri,vinyama Hivyo Vinaweza Kuwa Kwenye Uume,Uke,Mrija wa Mkojo(Urethra), Maeneo Yanayozunguka Sehemu ya Haja Kubwa,
na Sehemu Mbalimbali za Mwili Kama Usoni,Miguuni,Mkononi na Sehemu zingne
🚨CHANZO CHA TATIZO HILI
💉Ugonjwa Huu Husababishwa na Virusi Waitwao HUMAN PAOILOMA VIRUS(HPV)
✳️Kuna Aina Tofautu za HPV Virus lakini Kwenye Masundosundo za Sehemu za Siri Husababishwa Zaidi na Aina Mbili za Virusi (HPV-6 na HPV-11) japo Kuna Aina zaidi ya 100.
Maana sio wote wanasababisha tatizo hili Kwani kuna ambao Wanasababisha masundosundo sehemu tofauti kama vile mkononi,mguuni,mgongoni,n.k na Pia HPV virus huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazikwa wanawake na pia Husababisha kansa ya haja Kubwa Me na Ke
⚕️WATU WALIO HATARINI KUPATA UGONJWA HUU
1.watu wenye wapenzi wengi 2.wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo na haja kubwa,
3.wajawazito
4.watumiaji Wakubwa wa SIGARA na Pombe
5. Watu Wenye Upungufu wa Kinga Mwilini
⚕️DALILI ZA MASUNDOSUNDO SEHEMU ZA SIRI
✳️Pamoja na kuwa Vinyama Havina Maumivu, Vinaweza kuwa kero kwa sababu ya sehemu Vilivyopo, ukubwa wake na miwasho. Ukubwa huwa kama milimeta moja mapana yake hadi sentimeta moja ya mraba
Huweza Kuota Sehemu Zaidi Ya Moja
NOTE
Mwanaume huwa anachelewa kupata dalili na huwa na uwezekano mkubwa wa kuambukiza mwenza wake (wapenzi au mpenzi)
✳️Kwa Wanaume, Genital Warts Huweza Kutokea Kwenye Mrija wa mkojo, Uume, au kwenye Eneo la mkundu. Zinaweza kuwa kama vijinyama laini vilivyovimba visivyo na mkwaruzo (juu ya uume) au kama vijidole vinavyoning’inia (kwenye eneo la haja kubwa)
Masundosundo nyingine zinaweza kuwa na umbo la kukwaruza na zenye rangi nyeusi. Wakati mwingine hujificha kwenye unywele au zika ndani ya govi la mtu ambaye hajatahiriwa.
Kwa Wanawake Huwa kwenye sehemu zenye unyevu za mashavu ya ndani (labia minora) au kuzunguka tundu la Uke.
🚩MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU
Matibabu ya tatizo hili hupatikana kiurahisi iwapo tatzo halijachelewa kupatiwa tiba,hutolewa kwa kufuata utaratibu wa majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali matibabu hayo huweza kuwa kuviondoa kwa kufanya operation au Dawa
Kuna dawa zinazotumika kutibu Tatizo Hili na unaweza kuzitumia kama mbadala wa tiba nyingine.
💊Podophyllum resin ni dawa inayotolewa na mtaalamu wa tiba
💊Podofilox (Condylox) ni dawa unayoweza kuitumia nyumbani na ina uwezo mkubwa wa kutibu kuliko podophyllum resin.
💊5-Fluorouracil (Efudex) hutumika kama cream, huchukua muda mrefu kutibu, na ina madhara mengine mengi ya kiafya
💊. Imiquimod (Aldara) hutumika kama cream na maumivu wakati ukipaka hutokea
🍿wenza wote kupata matibabu n muhimu hata kama atajihisi hana Dalili zozote ni vyema zaid mgonjwa kufanya vipimo ili kujihadhari kabla ugonjwa haujaleta madhara zaidi
⚕️ KUJIEPUSHA NA UGONJWA HUU KWA KUFUATA YAFUATAYO
🚯kupata CHANJO ya HPV
🚯Epuka kuwa na Wapenzi wengi na Tumia Kinga
🚯Epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile
🚯Acha Kunyonya Uke/Uume
🚯Kula Vizuri na Fanya Mazoezi
NOTE🔨
Ndugu ugonjwa huu una madhara makubwa unaweza kusababisha kansa ya kizazi,kansa ya uume,kansa sehemu ya haja kubwa, NK
⚡Hivyo Hakikisha unapata matibabu ya uhakika iwapo una tatzo hili Usitumie Dawa Yoyote Kabla Ya Kuonana na Daktari
Ahsante
#Daktariwawatoto

Loading suggestions...