JAPHET MATARRA
JAPHET MATARRA

@Eng_Matarra

171 Tweets 41 reads Oct 10, 2021
PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA
#UZI:
💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇
Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo
Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.
Siku hiyo watu fulani hawakutaka kuondoka ili wahudumu wafunge.
#Naam...!!!
Siku hiyo watu fulani hawakutaka kuondoka ili wahudumu wafunge.
Kanali VASSILI, mutu ya pamba kali, Mzee wa kuwaka na mvuvi wa watoto wazuri mjini kama @BarakaSaimon3, basi naye alialikwa ktk sherehe hiyo na alikuwa ametupia nguo za kiraia ukimuona huwezi kumjua.
KANALI VASSILI NI NANI?
#Inshort:Ni kijana mdogo raia wa Urusi, anapenda sana raha, pombe kwake ni kama maji tu.Unaambiwa pia mara nyingi akiwa na gari lake la kivita ndani ya mitaa ya jiji hilo, hujiona km yupo Moscow
Yaani huwa hajali sana vizuizi vya traffic akiwa barabarani
Akiwa na wine yake aligonga glasi kadhaa kufurahia kifo cha Rais IDRISS DÉBY ITNO wa Chad, ambaye alikuwa amefariki siku 02 zilizopita. Wenzake hawakufurahia hali hiyo ingawa hawakuhusika na mauaji yake. Walifadhaika sana na ilionekana ni kukosa heshima kusherehekea kifo chake.
Licha ya kuwa Kanali huyu alikuwa akifurahia hafla hiyo akiwa na marafiki zake, Lkn alikuwa kazini na simu yake ilimkumbusha km mara 02 hivi
Mtu wa kwanza aliyewasiliana naye usiku huo alikuwa Rais FAUSTIN-ARCHANGE TOUADÉRA wa Afrika ya Kati na alitaka kufahamishwa habari fulani
Rais TOUADÉRA alitaka kujua vikosi vya Urusi vilikuwa vimefikia hatua gani kwenye operation zao dhidi ya kikundi cha Coalition of Patriots for Change/Coalition des Patriotes pour le Changement (CPC).
Kikundi hiki cha CPC ni muungano wa vikundi kadhaa vinavyojiita vya wazalendo!!
#CPC ni kikundi cha waasi na kinaongozwa na FRANÇOIS BOZIZÉ YANGOUVONDA, aliyekuwa rais wa nchi hiyo miaka 10 iliyopita (2003/2013).
#BOZIZÉ alimpindua rais wa zamani ANGE-FÉLIX PATASSÉ akiwa ameenda Niger. Mnamo 2013, naye alipinduliwa na waziri mkuu TOUADÉRA aliye madarakani.
Kikundi cha CPC kiliundwa mwaka jana 2020 na kuvuruga uchaguzi mkuu wa 2020/21 nchini humo.
Kanali Vassili ambaye jina lake kamili halijulikani kabisa, ndiye amepewa kazi ya kupambana na CPC na ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya WAGNER yenye Mercenaries na makomando wa kivita.
Kikundi cha CPC nitakielezea baadae kuanzia
📡Kuanzishwa
📡Uongozi
📡Operation n.k
Pia kampuni ya #Wagner nitaichambua kwa undani zaidi kadri tunavyoenda na huu Uzi, #muhimu ni kufahamu kuwa inaendeshwa na Tajiri wa Urusi rafiki na swahiba #01 wa Rais VLADIMIR PUTIN wa URUSI
Kanali VASSILI alikuwa amezoea kuzungumza na TOUADÉRA na haraka alimjibu na kumhakikishia kuwa kikosi chake bado kina nguvu
Aliongezea kuwa, Jeshi la nchi hiyo ambalo mara nyingi ndio huwekwa mbele karibun litasonga zaidi na punde litadhibiti maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao
Kisha baada ya mazungumzo hayo alikata simu na kurudi kunywa wine 🍷 yake
🎼Sherehe ziliendelea ingawa kulikuwa na amri ya kutotoka nje usiku. Yote kwasababu kiongozi huyo wa kijeshi toka Urusi alikuwa maarufu sana kiasi kwamba uwepo wake tu Club hiyo iliruhusiwa kuvunja sheria.
Lkn unaweza ukajiuliza KIJANA huyu ni nani?🤔
💨MTU ambaye anaogopeka kwa karibu watu wote Jijini Bangui mpk sheria zinavunjwa!!
📡Kijana ambaye ana mawasiliano ya moja kwa moja na rais, na ni kiongozi wa ngazi ya juu wa Kampuni ya WAGNER huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.!!
📡Je, ndiye BOSS wa WAGNER huko Afrika ya Kati? kampuni ambayo kwa mujibu wa vielelezo inaonekana haina LEGAL STATUS huko Urusi!
💨#Wagner ni nani?
💨#Kanali VASSILI ni nani?
💨#Wagner imefikaje nchini humo, kufanya nn?
Maswali yote hayo + mengine tutapata majibu hapa chini👇
#Inshort:WAGNER iliingia nchini humo miaka 03 iliyopita
Kwann ina nguvu sana serikalini?
Ni Kwa7bu ilipenyeza watu wake ktk nafasi za uongozi ndani ya nchi hiyo
Sasa kabla hatujaenda huko...
📡Tuingalie kwanza mauaji ya Rais IDRISS DÉBY (Chad) & connection na #Wagner (Putin)👇
MAUAJI YA RAIS IDRISS DÉBY (CHAD)📌
💨Usiku wa kuamkia Jumanne ya Trh 20 Aprili 2021, huko nchini Chad ulikuwa mbaya kwa wakazi wa nchi hiyo.Taarifa za mbaya zilioghofya mioyo yao.Hata waliokuwa wanakula daku kuendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan hamu iliisha GHAFLA!!
Hii ni masaa kumi na moja nyuma kabla ya hizi sherehe hizi ulizoona Kanali VASSILI raia wa Urusi, MTU wa karibu sana na Rais TOUADÉRA wa Afrika ya Kati anayeogopeka Jijini Bangui alikuwa amealikwa👇
💥Kulikuwa na nini?
💨Taarifa hizo mbaya zilisema kuwa Rais IDRISS DÉBY ITNO wa taifa hilo akiwa ktk mapambano dhidi ya vikosi vya waasi huko ktk maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo amejeruhiwa vibaya na kupelekea kifo chake🤔
Sio eti yupo ICU anapumlia mashine..NO ameshafariki😢
💨Simple simple tu..au? BIG NO!!
💨Ilikuwaje SASA..?👇
📡Rais Idriss Déby Itno (IDI) almaarufu 'Marshall IDI', siku Tatu nyuma kuanzia Aprili 11, alipata taarifa kuwa waasi wa kikundi cha FACT wamevuka mpaka na kuingia nchini wakitokea LIBYA na sasa wamekaribia mkoani KANEM.
Hazikuwa taarifa nzuri, kwa7bu kutoka Mji wa MAO makao makuu ya mkoa huo hadi ilipo Ikulu ya nchi hiyo Jijini N'DJAMENA ni umbali wa 309KM sawa DAR - PANGANI.
Pia mpaka Waasi kufika hapo inamaana Tyr kuna kambi nyingi zimeshatekwa!!
Tangia hiyo siku Rais Déby hakupata usingizi💣
Kulingana na Intelijensia ya Jeshi la nchi hiyo na Ufaransa, vikosi vya FACT vilikuwa na kundi kubwa la wapiganaji zaidi ya watu 1500.
Marshall IDI kusikia hivyo, aliamua kutuma wanajeshi zaidi ya 1,000 ili kuongeza nguvu na kuwazuia waasi wasifike mjini yalipo makazi yake.
📡Lakini kutokana na waasi kuwa na mafunzo mazuri, silaha nzito, magari ya kisasa ya kivita tena yaliyotengenezwa nchini Urusi, unaambiwa bado hali ilikuwa mbaya sana kwa wanajeshi wa nchi ya Chad.
💨Ilipofikia hapo Marshall IDI aliamua kuingia vitani kuwasaidia majeshi yake.
Ikawaje TENA..?
📡Kwa kuwa Rais Idriss Déby ni Commando💣 round hii aliona acha awaonyeshe vijana wake mwenyewe kwamba He's a 'MARSHALL' km alivyowaonyesha mwaka 2020 kule Ziwa Chad lilipotokea jaribio la mapinduzi, lkn pia kuwaongezea nguvu na kuwatia moyo wanajeshi wake.
Hebu kabla hajaingia uwanja wa mapambano tupate historia yake japo kwa ufupi.
💨#Inshort:Rais DÉBY aliingia madarakani kwa mapinduzi mnamo 1990. Hivyo mpk hapo alikuwa ametawala kwa miaka 30. Alimpindua mtawala wa zamani Dikteta HISSÈNE HABRÉ aliyefariki karibuni kwa #COVID19
Alivyoingia madarakani hakupata upinzani sana kwa sababu alimuondoa Dikteta.
💥Lakini ilipofika mwaka 1995, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi zamani Jenerali MAHAMAT GARFA, alichukua jeshi kutaka kumpindua akisaidiana na mpwa wake MAHAMAT NOUR ABDELKERIM. Jaribio hilo pia lilizimwa!!
Mnamo 2005 & 2008, kulitokea majaribio mengine yaliyoongozwa na MAHAMAT NOUR ABDELKERIM, nayo pia yalizimwa.
💥Kuanzia 2018 ndipo mapambano mazito yalipoanza baada utawala wa MUAMMAR GADDAFI (Libya) kuanguka na vikosi vya FACT vilishinda vita na kuchukua udhibiti wa mkoa Tibesti
💥BILA nadhani unajiuliza kwanini TIBESTI.
#Inshort:Chad & Libya zina mgogoro wa muda mrefu ktk border ya AOUZOU toka enzi za mkoloni. Libya imechukua eneo la Chad ndio maana haifukuzi waasi wanaokaa hapo.
#PILI:Mkoa huu upo ktk milima yenye utajiri mkubwa wa madini ya Dhahabu!
Tuendeleee sasa
KIREFU CHA "FACT" NI NINI?📌
📡#FACT = Front pour l’Alternance et la Concorde au Tchad (Kifaransa) au Kiingereza ➠ "Front for Change and Concord in Chad"
📡Unaweza kutizama hapa chini muundo, mapambano na viongozi wake, ukimaliza njoo nikupeleke VITANI...!!👇
Kwahiyo Marshall IDI aliamua kuingia ktk mapambano.
💥Mnamo Aprili 16, muda wa saa 10 za jioni alichukua gari lake la kivita lililotengenezwa na kampuni ya TOYOTA moja kuelekea vitani.
🚔Msafara wake uliongozwa na mdogo wake na mke wake (shemeji) anayeitwa KHOUDAR MAHAMAT ACYL.
Mwanae MAHAMAT IDRISS DÉBY @GmahamatIdi, aka "Kaka" ambaye sasa ndio Rais wa mpito wa Chad pamoja na kipenzi cha moyo wake 1stLady Bibie HINDA DÉBY ITNO @HindaDebyItno walibaki kumsubili Ikulu.
Wkt huo Majenerali TAHER ERDA & MAHAMAT CHARFADINE ABDELKERIM wakiwa wameshatangulia.
#Convoy ya Rais DÉBY ilikuwa inaelekea Mjini Mao, ambapo kikosi cha wanajeshi karibu 3,000 kilikuwa kimeweka kambi kilomita chache nje ya mji huo wakimsubilia
📸Wakiwa njiani giza likiwa limeshaingia, alisimamisha msafari kusikilizia hali na maendelea ya mapambano huko anakoenda
📡Alishuka kwenye gari akiwa na viongozi kadhaa wa kijeshi, kisha akafanya mawasiliano!! Baada ya kupokea taarifa alirejea barabarani tena kuendelea na safari.
🌄Baada ya safari ndefu, asubuhi ya Aprili 17, alifika NOKOU eneo mapambano yalipokuwa takribani 40Km toka Mjini MAO.
#Marshall IDI aliingia, na kuomba kuonyeshwa mchoro mzima jinsi maadui wake walivyoweka kambi.
💨Kisha akahamasisha jeshi lake.
💥Waliokuwa mbele waliposikia naye ameingia vitani, walipata moyo wakaongeza mapambano, unaambiwa waasi walikiona cha moto mpk wakarudi 4.6Km nyuma.
Mwanzoni mapambano yalionyesha Jeshi la Chadi linaelekea kuwazidi maadui wake, lkn baada ya saa 1 tena upepo wa mapigano ulibadilika!!
💥Kadri muda 🕞 ulivyoenda wapiganaji wa Waasi walisogea, hali ya mapigano ikaendelea kuwa mbaya zaidi hasa upande wa vikosi vya Jeshi la Chad.
🚔Ikabidi kijana wake aliyebaki Ikulu @GmahamatIdi aje kuongeza nguvu, huku msaada mwingine ukitoka Jeshi la Ufaransa wakawasambaratisha wakarudi nyuma!!
Ufaransa wao walijikita ku📡track kambi za kikundi cha FACT kwa kutumia Rada za angani na kuwambia jeshi wa Chad.
Tizama..👇
Kumbe, wapiganaji wa FACT walivyorudi nyuma walikwenda kujipanga.
Mercenaries kutoka kampuni ya #Wagner ndipo waliingia vitani rasmi.
Mapigano makali tena zaidi ya mwanzo yakaanza mpk viongozi wa jeshi waliokuwa mstari wa mbele walipata hofu ya kuzidiwa. Wakaanza kurudi nyuma!!
Taarifa zikamfikia Rais DÉBY, akakasirika sana + baadhi ya maneno ambayo majenerali walianza kumwambia kama kumshauri kwamba aondoke rudi Ikulu.
MTOTO wake na wanajeshi wa Ufarasansa nao walimshauri, kwamba itafutwe namna aondolewe eneo la mapambano sababu imeshakuwa hatari..!💣
💨Akaona wanamfundisha uoga, akaamua kuingia mwenyewe vitani kuwaonyesha!
📡Ilipofika mchana Marshall IDI, aliingia ktk gari, akamuamuru dereva wake ampeleke ktk kikosi cha wanajeshi cha mwanzo kabisa.
💥Walinzi wake walimfuata ili kumlinda na kujibu mashambuli yatayomlenga!!
Kumbuka Rais DÉBY ni #Marshall cheo kikubwa sana jeshini hicho, alikuwa haogopi.
Alivyoingia tu, Top-mercenaries from #Wagner Group na watalaam wa kulenga shabaha wakaingia
#Kwa muda mfupi, Rais DÉBY, alipigwa risasi ya kifuani na SNIPER, risasi ambayo ilikwenda mpk kwenye Figo
Damu zilimtoka nyingi ikabidi atolewe pale haraka sana.
Rais Déby alikimbizwa ktk kambi yao iliyokuwa umbali wa 23Km hivi na madaktari bingwa wa majeshi yote (Chad & Ufarasansa) waliitwa kwenda kumtibu.🤔
Huku wanajeshi wakiongozwa na kijana wake MAHAMAT wakimcover asidhurike
💨Marshall IDI aliumizwa sana lkn hakuna aliyefahamishwa, isipokuwa watu baadhi. Ikafanywa siri ili kutowavunja moyo wanajeshi wake.
Medical Helicopter iliitwa haraka sana kumpeleka Mji mkuu N'Djamena. Bahati mbaya nayo ilichelewa, Rais DÉBY akafariki dunia hapo hapo kambini🤔
Licha ya kufariki haikuwekwa wazi bado. Kikao cha dharula kikaketi. Lengo ni kupanga namna ya address msiba na nani anaenda kushika nchi.
Hata kijana wake @GmahamatIDi hakuambiwa..!!
Usiku ule ule APRIL 17, mwili wa Marshall IDI ulichukuliwa na Helicopter na kupelekwa Ikulu.
Kwanini wajadili kuhusu nani ashike utawala baada ya kifo chake?
#Sababu: Wiki moja iliyokuwa imepita yaani mnamo April 11, 2021, kulifanyika zoezi la upigaji kura wa kumchagua Rais.
Hivyo, Tume ya Uchaguzi ilikuwa bado haijamaliza kujumlisha kura na kutangaza matokeo.
Kulikuwa na uwezo wa kutangaza hivyo hivyo, lkn ugumu ulikuwepo kwa sababu, nchi ilikuwa ktk vita TENA 300Km toka makao makuu na baadhi ya wagombea walikuwa wamesusia kura hizo.
Hivyo endapo wangetangaza kifo cha kabla ya matokeo pengine machafuko yangeibuka mjini N'DJAMENA.
Kijana @GmahamatIdi aliitwa arudi Ikulu, wkt huo Tume ya Uchaguzi ikisubiliwa ijumlishe matokeo angalau ¾ ya vituo vyote.
Lkn kulikuwa na ugumu wa kurudi kw7bu bado wanajeshi walikuwa vitani kule NOUKOU ikabidi wampe taarifa akiwa huko huko, lkn mke wake Rais DÉBY hawakuambiwa.
📡Kumekucha Jumapili April 18, vikao viliendelea na mke wake akaambiwa, lkn ktk mazingira ambayo hawezi kushtuka sana na wakampa pia taarifa kwamba mwanae ndio muda atatangazwa kuwa kuwa kiongozi wa mpito.
Jumatatu mchana April 19, ndio uvumi wa kifo chake ulianza kusambaa MJINI
Mchana huo @GmahamatIdi alirudi N'Djamena.
Majadiliano yalianza kuhusu kpnd cha mpito, ambapo baadhi ya maafisa wa ngazi za juu na watu wa ukoo wa Zaghawa walitaka waongoze nchi, lkn baadaye makubaliano yalifikiwa kuwa Baraza la Mpito la Kijeshi liundwe litaloongozwa na yeye.
Majira ya saa 03 Usiku, Tume Ya Uchaguzi, ambayo pengine wajumbe wake hawakujulishwa kuhusiana na kifo hicho na kilipangwa kitangazwe kesho yake mida ya saa 5 Asubuhi, ilitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais, kuwa IDRISS DÉBY ITNO ameshinda kwa 79.32% ya kura.
Kwasababu kila kitu kilikuwa planned hawakutaka kurahikisha
📡Mnamo April 20, 2021 SAA 11:18 alfajiri Jumanne kupitia runinga ya taifa (Tv Chad) ndio kifo cha Rais DÉBY kilitangazwa. Ht Media nyingi mfano @bbcswahili, @VOAAfrica na huku kwetu zilitangaza kifo hicho asubuhi hiyo.
"The president of the Republic, Head of State, Supreme Head of the Army, IDRISS DÉBY ITNO, has just breathed his last while defending the territorial integrity on the battlefield. It is with deep bitterness that we announce to the Chadian people,
"..the death this Tuesday, April 20, 2021 of the Marshal of Chad. The funeral of the Marshal will take place on Friday 23 April in N’Djamena, before the body of the deceased is transported to his village of Amdjarass, where he will rest."~ Msemaji wa Jeshi AZEM BERMANDOA AGOUNA
💨Ukilinganisha na Rais DÉBY alikuwa ni Muislamu na kufariki siku 03 Tatu nyuma ndio maana ilipangwa hata kama matokeo hayajatangazwa kesho yake saa 05 kifo chake kitangazwe.
Sasa wakashtukizwa Matokeo ikabidi wasubili ili watangaze alijeruhiwa jana yake ila Mungu kampenda zaidi
Kulikuwa na uwezekano wa mwili kutunzwa siku 05 kwa ajili ya kuagwa lkn Tyr una siku 03 nyuma + hizo walizotangaza kuuzika JUMLA siku zinafika 07 hivyo isingewezekana wazidishe hapo.
KIFO chake kilitekelezwa na #Wagner nitaelezea mbele kwa undani
💨BILA SHAKA UMEPATA CHOCHOTE?
Hivyo ndio alivyouawa IDRISS DÉBY ITNO aka Marshall IDI.
Sahivi mtoto wake ndio kashikilia nchi ya Chadi.
Lkn Familia hiyo inaendesha kampuni mbalimbali za serikali ikiwemo Société des Hydrocarbures du Tchad (SHT) inayozalisha mafuta na @GmahamatIdi ndiyo CEO since 2019!!
Tuendelesee
#WAGNER ni kampuni isiyo rasmi inayojihusisha na ulinzi binafsi yenye uhusiano wa karibu sana na Rais VLADIMIR PUTIN wa Urusi.
Kampuni hii imesambaa Mashariki ya Kati, America & Afrika.
Headquarters kwa Afrika ni SUDAN
Lkn inajificha ktk utoaji mafunzo na ulinzi📌
Ktk uchunguzi nilioufanya nimepata siri mbili na nitachimba kwa Afrik mtandao mzima (footprints)
Hivyo ndio maana ndani ya #Uzi huu umeona nimeanzia huko kugusia operation za siri ilizofanya, lkn nitaangazia PESA waliyonayo na mtandao wao nje ya nchi & unavyotekeleza mission
JE, WAGNER ILIPATEJE NGUVU NA KUENEA NCHINI A.KATI?
Mnamo Sept 2017, Ufaransa ilisema itapeleka KALASHNIKOV 1,500 huko A. Kati, kw7bu jeshi lake la majini lilitumia mwaka 1 na ½ kuichukua Pwani ya Somalia. Ingawa lilikuwa chini ya UN, na hupitishwa na Baraza la Usalama la UN.
Hivyo Urusi ilipiga kura ya 'veto' kupinga suala hilo.
NAJUA unajiuliza 'KALASHNIKOV' ni nini?
#KALASHNIKOV ni bunduki almaarufu sana #AK-47.
Ilibuniwa na mvumbuzi raia wa Urusi anayeitwa MIKHAIL KALASHNIKOV. Kuna matoleo tofauti ya bunduki hizo.
ILA zamani zilitengenezwa nchi za Kisovyeti pekee. Kwa sasa zinatengenezwa nchi nyingi duniani.
#Inshort:Kutokana na madhara ya WWII, Jeshi la USSR liliamua kutengeneza bunduki mpya ambayo inaweza kufyatua risasi moja-moja kwa wingi mithili ya bunduki za rasharasha (Gatling).
Hivyo lilitangazwa shindano la mvumbuzi atakayeweza kubuni bunduki ya kufanania hivyo
Shindano lilitangazwa ndani ya jeshi na MIKHAIL KALASHNIKOV ndiye aliyeshinda. Alikamilisha uvumbuzi wake mwaka 1947 na bunduki hizo zilianza kutengenezwa rasmi mnamo 1948.
Kifupi cha #AK-47
AK-47 = "Avtomat Kalashnikov 1947"
Kwa Lugha huko = "Автомат Калашникова складной образца 1947 года".
Ni bunduki ambayo ni hatari sana. Inasemeka imeondoa maisha wanadamu wengi kuliko silaha yeyote na inafanya kazi vizuri ktk mazingira yote. Imesambaa sana
Tuendeleee sasa....!!👇
Ili kuondoa kizuizi hicho, Ufaransa ilitumia akili. Ilifanyaje? Kwanza ilimshauri Rais Touadéra (Afrika ya Kati) aitetea ktk case hiyo dhidi ya Urusi.
Mnamo Oktoba, 2017, Rais TOUADÉRA alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi SERGEY LAVROV huko Sochi
Baadae serikali ya Urusi ilikubali kuondoa kura ya turufu (veto) ndipo ikatumia fursa hiyo kuleta kampuni hii ya #Wagner nchini Afrika ya Kati.
Waziri LAVROV alipendekeza makubaliano ambayo yaliongeza ugumu zaidi wa kuondoa kwa urahisi hiyo kura ya turufu au unaweza kuita Veto.
Serikali ya Urusi ilikubali na kuweka uzito wake wote nyuma ya kizuizi hicho, ambacho Afrika ya Kati ilitarajia kwa muda mrefu kuwa ipo siku kitapunguzwa.
Kwa mabadilishano, Urusi wao walijipanga kurudi kwa njia ya uwekezaji, ILA nyuma yao wakijua wanachofanya.
Moja ya masharti ktk makubaliano hayo, ambayo hayakuwekwa wazi kwa wakati huo, ilikuwa kwamba ama kampuni ya uchimbaji madini kutoka Urusi ifunguliwe huko Afrika ya Kati au raia wa Urusi waruhusiwe kuendesha uwanja wa ndege (usio wa kibiashara) ktk mkoa wa Ouadda.
Mnamo Januari 2018, ndege ya kubwa ya shehena ya ILYUSHIN #76 ilipeleka silaha za kwanza. Ikafuatiwa na Kalashnikovs (AK-47) 6,200, bastola aina ya Marakov 900, rocket launchers 270 na silaha 20 za kushambulia ndege, ambavyoo vilitolewa ndani ya miezi miwili.
Licha ya hivyo watu waliojiita washauri masuala ya kijeshi walitia timu nchini humo na kampuni 02 zilipata mikataba yao ya kwanza.
Kampuni hizi zilikuwa ni LOBAYE INVEST, iliyoundwa mnamo Oktoba 2017 na kampuni yake ndogo SEWA SECURITY SERVICES, inayohusika kuihakikisha usalama
Mnamo Juni na Julai 2018, Waziri wa Madini wa Afrika ya Kati, LÉOPOLD MBOLI FATRAN, alitoa vibali vya utafiti wa madini kwa kampuni ya LOBAYE INVEST ktk mikoa ya Yawa na Pama. Vibali vingine vilitolewa baadaye kwa mikoa ya N'Délé, Bria, Birao na Alindao.
📸Kwahiyo URUSI imejikitia mizizi Africa kupiti #wagner na inaendelea kujitanua na sio CENTRAL AFRICA pekee Wapo pia.....👇
📡 Sudan
📡 Guinea
📡 Guinea-Bissau
📡 DRC- Congo
📡 Libya
📡 Zimbabwe
📡 Madagascar
📡 Rwanda
📡 Botswana
📡 Lesotho
📡 E-swatin
📡 Msumbiji
Waingia kwa mbinu zile zile, kwamba wao wanatoa Support na kupinga Ukoloni Mamboleo (Neo Colonialism) lkn kwa group mambo ni TOFAUTI..!!!
Mambo ya kufahamu
Wanafanya vipi Operation zao
Ngapi zimefanikiwa na wapi na wapi wametaget...!!!
📌Je! Kuna uhusiano gani kati ya SEWA SECURITY SERVICES, LOBAYE INVEST na kampuni ya #WAGNER & Rais PUTIN?
💨Pesa walizonazo
💨Mauaji (ukiwafuatilia)
💨Migodi ya Uranium (Africa)
💨Mapigano na Waasi (CPC)
💨Mizizi (Rwanda, Mali, Botswana nk)
📡Inaendelea
RT🔄 Follow @Eng_Matarra
KUNA UHUSIANO GANI kati Ya KAMPUNI hizo & WAGNER?📌
#Iko hivi, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lobaye, anaitwa YEVGENY KHODOTOV ni mtu ambaye hapendi sana kujionyesha ktk vyombo vya habari nchini humo.
KHODOTOV ana miaka 57 na alikuwa Afisa Polisi huko St. Petersburg nchini URUSI
Hivyo anafanya kazi kwa usiri mkubwa akishirikiana kwa karibu sana na mwenzake VALERY ZAKHAROV, afisa wa zamani wa ujasusi wa jeshi la Urusi (GRU) ambaye amekuwa akimshauri Rais Touadéra tangu Juni 2018.
KHODOTOV pia anaongoza kampuni ya M-FINANS, inayofanya kazi kwa niaba ya kampuni ya CONCORD iliyoko Urusi na inayochukuliwa kuwa kitovu cha shughuli zote za YEVGENY PRIGOZHIN anayemiliki makampuni nyingi, mojawapo iliyowahi kutuhumiwa na USA kuingilia Uchaguzi Mkuu mwakw 2026.
Tajiri PRIGOZHIN ni swahiba mkubwa wa Rais PUTIN wa Urusi.
📡Yaani ile wanasema pete na kidole 👣
Ndiye aliyemtangaza kupitia migahawa yake mikubwa ktk miaka ya 1990 na kumfanya Rais PUTIN akaingia ndani ya Ikulu ya Kremlin, na anahusika na kampuni nyingi ktk sekta ya ulinzi🔫
Bosi huyu wa zamani wa Fast food kama bibie @amina_hafidh alipata utajiri wake kwa kuuza vitafunio aina ya 'Hot dogs', aliwahi kuhukumiwa kwa ulaghai na kujihusisha na masuala ya ukahaba mnamo 1981, lkn miaka 09 baadaye aliachiliwa huru.
Anafahamika sana kama PUTIN'S CHEF.
Pia amekuwa akipata mikataba minono (mikubwa) yenye faida nyingi na anao utajiri unaokadiriwa TRILIONI 3.4 Tshs za Kitanzanania kutokana biashara ya kampuni zake zinazohusika na masuala ya ulinzi na Usalama.
Kwahiyo tajiri YEVGENY PRIGOZHIN ndiye mfadhili mkuu wa kampuni ya #Wagner, iliyoanzishwa kati ya 20132014 na mara nyingi amekuwa akihusishwa na jamaa yake Luteni Kanali DMITRY UTKIN, aliyekuwa mpatanishi wa mfuasi wa siasa za Kinazi na mkuu wa Special Forces na GRU.
Mwanzoni mwa 2018, huko Quai d'Orsay, Paris nchini Ufaransa, yalipo makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya na Masuala ya Ulaya, zilivuma habari nyingi na zenye kuonyesha wasiwasi juu ya ukaribu mkubwa uliopo baina ya kampuni hizo na Rais Touadera wa Jamhuri ya Africa ya Kati.
Wasiwasi uliongezeka sana baada ya ZAKHAROV kuonekana akiwaita baadhi ya mawaziri na kuzungumza nao nje ya mji kwa kivuli cha Mshauri wa Rais + kupatiwa ulinzi na walinzi kutoka SEWA SECURITY.
Baada ya Ufaransa kuona hivyo, licha kuwa na historia ndefu na nchi hii, #ILIJIONDOA!!
Ndio wakati huo vikosi vya tajiri PRIGOZHIN vilipondelea kuwa karibu na Rais Touadera.
Hivyo ZAKHAROV na wafuasi wake walitumia nafasi hiyo kuipinga Ufaransa kwa propaganda na wakatengeneza uhasama baina yao kwa lengo la kunufaika zaidi na kampuni zake zilizowekezwa nchini humo.
Na ili kupata uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa, waliamua kwenda Sudan, ambaye ni jirani yake mkubwa.
Kumbuka OMAR AL-BASHIR alikuwa na mgogoro na Marekani na alikuwa wanted na ICC.
Wakaweka Headquarters huko.
Wakatafuta namna ya kumuondoa Bashir asijekujisalimisha akawaumbua.
Uhasama wake na Marekani, ulianza baada ya Sudan Kusini kujitenga na ilivyojipatia uhuru (2011), USA iliwapa support kubwa.
Na tokea uhuri Sudan ilifunga mpaka wa kuingia Sudani Kusini mpk Leo!!
📡Kwahiyo WAGNER na PRIGOZHIN walitumia Sudan km Daraja la kuingia Afrika ya Kati.
Mnamo Agosti 2018, kulifanyika mkutano mkubwa wa wadau wa madini na ulisimamiwa na Luteni Jenerali JAMAL ALDIN OMAR na viongozi wa #Wagner walialikwa.
Baada ya miezi kadhaa, vikosi vya OMAR viliwasiliana na viongozi waasi wa Africa ya Kati akiwemo NOUREDDINE ADAM na ALI DARASSA.
Huyu Lt Gen. OMAR 📌alikuwa ni Mkuu wa Majeshi wa zamani wa Sudan. Alifariki mwaka jana mwezi Mei akiwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.
🔕Alifariki mjini Juba, kutokana na mshtuko wa moyo, wkt akiwa ziarani kuhudhuria kikao cha kutafuta suluhu baina ya nchi yake na Sudan Kusini.
Baadae zilionekana Helikopta kadhaa zikifanya safari kati ya SUDAN na AFRIKA Ya KATI
#ForYou:Ktk mkutano ule, Lt Gen. OMAR alipendekeza Afrika ya Kati, kufanya mazungumzo na viongozi wa waasi kuleta amani ktk biashara wanayotaka kuifanya na Morocco iliunga mkono pendekezo hilo.
Suluhu ilikuwa inatafutwa kwa sababu waasi walikuwa vimeshikilia maeneo mengi yenye migodi mikubwa ya madini
#Wagner target yao ni madini ya Uraniam na Almasi inayopatikana kwa wingu nchini humo. Lkn pia kule Morocco wamefungua kambi ya mafunzo ya jeshi kwa vikosi vya nchi hiyo.
Kuanzia 2013, Urusi ilikuwa ikiisaidia sana Sudan. Vikosi vyake vilirespond kazi zote vilipohitajika. Hata ktk maandamano waliitwa kutoa msaada.
📡Vilevile zaidi ya Wasudan 300 waliajiriwa na M-FINANCE, kampuni iliyowahi kuingia mkataba na Urusi kuingiza ndege za Kijeshi Sudan.
#WAGNER ndio wako nyuma ya wanaoendesha hizo kampuni 03:
📡M-Finance,
📡M-Invest &
📡Meroe Gold.
📌Hii ya mwisho ndio inayoendesha migodi nchini humo
M-INVEST & M-FINANCE km ilivyo Africa ya Kati, zimeunganishwa na Concord kupitia kampuni ya MEGALITE ambayo pia ni ya PRIGOZHIN.
KHODOTOV ndiye amefungua hizo kampuni huko Sudan na kumweka mtu wake kutoka Urusi aitwaye MIKHAÏL POTEPKIN (@M_potepkin) kuwa Mkurugenzi.
Hapa chini 👇 unaweza kuona kwa namna gani anavyohusiana kutokana na muingiliano na kampuni kivuli zilizofunguliwa.
KHODOTOV ameonekana kuwa na uhusiano wa karibu na ANNA BOGACHEVA, aliyekuwa anajihusisha na masuala ya utafiti na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya "Protection of National Values", iliyo na muingiliano na kampuni za PRIGHOZIN na amekuwa akitafutwa sana na FBI.
Mnamo Agosti 2018, MIKHAÏL (@M_potepkin), alionekana ktk Ofisi makao makuu ya Jeshi mjini Khartoum.
Inasemekana popote alipooneka ktk mji huo, alikuwa na walinzi wasiovaa sare wasiopungua 10. Pia akisafiri na ndege nchini humo, husindikizwa ndege zingine 2 kwa usalama wake.
Mnamo Feb 05, 2019, kulifanyika Mkutano wa makubaliano ya amani yaliyoitwa 'Khartoum Agreement', na Rais TOUADÉRA, FIRMIN NGRÉBADA (W/Mkuu), MARIE-NOËLLE KOYARA (W/Ulinzi) na viongozi wa waasi kwa pamoja walitia saini chini ya SMAIL CHERGUI (@AU_Chergui) Kamishna wa Amani wa AU.
Baada ya makubaliano mwakilishi wa Urusi na kampuni hiyo, walibakia Central Africa na #Wagner ikaendelea kuwa na nguvu zaidi.
📡Waliimarisha uhusiano wao na Rais Touadéra na waziri mkuu Ngrébada, huku wakijitangaza ktk mataifa ya nje kwamba, wamefaulu ambapo wengine wameshindwa.
Kiongozi wa usukani alikuwa VALERY ZAKHAROV, mshauri mkuu wa Rais TOUADÉRA akiwa na mdogo wake DMIITRY SYTYI.
Wote wawili wanamwakilisha Tajiri PRIGOZHIN ktk kampuni ya WAGNER huko Central Africa.
Kipindi cha nyuma walijifanya wasemaje wa serikali ya nchi ktk mitandao ya kijamii
DMIITRY SYTYI ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 32 na mhitimu wa masomo ya biashara, masoko & uchumi kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Catalonia (Spain), na amekuwa akifanya kazi na ofisi ya habari na mawasiliano, chini ya kitengo kinachosimamiwa na Rais Touadera.
Ofisi aliyokuwa anafanya kazi ilikuwa inaongozwa na mmoja wa watu wa karibu na waaminifu sana kwa Rais Touadéra, waziri wa mambo ya ndani MICHEL NICAISE NASSIN, kabla hajateuliwa uwaziri.
📡Kazi yao ilikuwa ni kutangaza vizuri mahusiano ya muungano wa Urusi na Afrika ya Kati.
📜OFISI hiyo inachofanya ni kuchapisha habari zinazoonyesha baadhi ya wanasiasa ni maadui wa serikali kwa shutma mbalimbali
Aka #MUSIBA wa Afrika ya Kati👆
Kampuni ya LOBAYE imepanua shughuli zake za madini na kuongeza wafanyakazi & Wagner iliendelea kuwa na ushawishi serikalin
📜KUIBUKA KWA KIKUNDI CHA WAASI (CPC)📌
📡Katikati ya Desemba 2020, mvutano uliongezeka kwa wiki kadhaa nchini humo, ambapo upinzani ulipinga kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao. ILA serikali iliendelea kusisitiza kwamba uchaguzi huo uliokuwa umepangwa Desemba 27, 2020 utafanyika.
Baadae Mahakama ya Katiba ilitangaza FRANÇOIS BOZIZÉ, hana sifa za kugombea. Ingawa alikubaliana na maamuzi hayo na kusema atamuunga mkono ANICET-GEORGES DOLOGUÉLÉ wa upinzani, baadae Bozize aliongea na waasi waliosaini makubaliano ya 'Khartoum Agreement' ili kuzuia uchaguzi huo.
Mnamo Desemba 17, viongozi 06 wa waasi wakiongozwa na BI SIDI SOULEYMANE almaarufu ABASS SIDIKI pamoja na Ali Darassa, Mahamat al-Khatim,, Adam, Mexime Mokom na Diedonne Ndamante, walitangaza kuundwa kwa CPC. Siku mbili baadaye walisema kuwa wataandamana kuelekea mji mkuu Bangui.
Mnamo Desemba 27, 2020, FRANÇOIS BOZIZÉ alitangaza kuungana na waasi. Akamsaliti mgombea mwenzake wa upinzani ANICET DOLOGUÉLÉ na akatangazia wanachama na wafuasi wake wasipige kura.
Ikapelekea Jumuiya za Kimataifa kulazimika kumuunga mkono Rais Touadéra dhidi ya waasi.
Jumuiya za Kimataifa (AU, UN na ECOWAS) zilitangaza kumtetea Rais Touadera kwa sababu tu viongozi wa waasi walikuwa wamevunja makubaliano ya "Khartoum Agreement".
Hapo ndipo Kampuni ya WAGNER ilipata nguvu kwa kutoa ulinzi kumlimda Rais Touadera wa nchi hiyo dhidi ya waasi.
#HIVYO, tangu Desemba 2020 mpk Januari na Februari mwaka huu, vikosi vya SEWA SECURITY vimekuwa vikipigana na kikundi cha CPC, ambao baada ya kushindwa kuudhibiti mji mkuu wa Bangui walikimbilia maeneo ya mipakani.
ZAKHAROV alitangaza rasmi vita na CPC mnamo Februari 11, 2021.
Kuanzia hapo #Wagner ikawa na udhibiti wa serikali. Makao makuu yao yapo Berengo Camp, tangu April 2018, ilipoingia nchini humo.
Maamuzi yeyote yanayotolewa na Rais kwanza lazima yawafikie WAGNER kisha hutumwa Urusi kupitia mwakilishi wao Gen. OLEG POLGUEV kabla ya kutangazwa.
Vikosi vya SEWA SECURITY na WAGNER vimepewa makazi ya kuduku mjini Bangui maeneo yalipokuwa makazi ya Ikulu ya BOKASSA mtawala wa zamani wa nchi hiyo
📡Sehemu ya majengo hayo imetengwa kwa ajili ya kufundisha wanajeshi wa Afrika ya Kati na ina uwanja wa ndege✈️wenye urefu wa 2Km
Eneo hilo la mjini Bangui wanalokaa zamani lilikuwa chini ya udhibiti wa Ofisi ya wizara ya ulinzi ILA sahv linalindwa usiku na mchana na wanajeshi wa Urusi.
#ForYou: JEAN-BÉDEL BOKASSA alimpindua mwasisi wa taifa hilo DAVID DACKO mnamo 1965.
Alitawala miaka 10 kati ya (1966/76), kisha akajitangaza mfalme wa kudumu. Hakukaa sana, kwa msaada wa Ufaransa 1979 alipinduliwa DACKO akarudi madarakani (Operation Caban & Baracuda)
DAVID DACKO alikaa mpk 1981 baada ya Mkuu wa Majeshi Gen. ANDRÉ-DIEUDONNÉ KOLINGBA kumpindua.
KOLINGBA naye alitawala km miaka 09.
👣Kuelekea mwisho wa Vita Baridi aliambiwa aandae Uchaguzi Mkuu wa Rais na alianguka. Aliyekuwa waziri mkuu wake ANGEL-FELIX PATASSÉ ndiye aliyeshinda.
Mnamo 2003, akapinduliwa na FRANÇOIS BOZIZÉ, ambaye alitawala takribani miaka 10 hivi,
Hivyo mwaka 2013 ndipo FRANCOIS BOZIZÉ alipinduliwa na huyu Rais aliyepo madarakani sasa TOUADERA.
BILA shaka hapo, umepata kahistoria kafupi kuhusu nchi hiyo ninayoizungumzia hapa.
Tuendeleee sasa..👇
MTOTO wa mtawala huyo anayeitwa JEAN SERGE BOKASSA, karibuni alipokuwa akienda kuzuru kaburi la Baba yake alizuiwa mpk kukawa na mgogoro mkubwa sababu eneo la makazi ya Mzee wake kupewa SEWA SECURITY & WAGNER.
Kuna kpnd walitengeneza picha za uongo kuonyesha kaburi linatunzwa!!
Baada ya kuzuiliwa na kutopatikana kwa kaburi la mzee wake mnamo Novemba 03, 2020, aliitaka serikali kumlipa pesa kila mwaka kama malipo kwa ajili makazi ya baba yake.
Mwanasiasa huyo ambaye anaishi huko Koyara ingawa hakuwa na madhara yeyote alinyamazishwa kwa kupewa uwaziri.
Mwezi Aprili 18 mwaka huu, Urusi ilikubali kuwa ilipeleka wakufunzi 532 nchini humo, lkn vyanzo vingine vya habari viliripoti inakadiriwa watu 2,000, ukiachilia karibia 1,000 waliopo Kambi ya Berengo, wameingia nchini humo na wengi 80% wanazungumza kiarabu kutoka Syria na Libya.
WAGNER imejiimarisha sana unaambiwa hufanya chochote na serikali ipo kimya. Wamejenga viwanja vya ndege mikoa ya N’Délé, Birao na Ouadda. Huko Ouadda, LOBAYE INVEST inafanya kazi na ZAKARIA DAMANE, kiongozi mmoja wa kikundi cha waasi aliyekuwa na ushawishi mkubwa ktk mkoa huo.
WAGNER imesambaa sehemu nyingi.
#Mfano; ipo Yawa na Ndassima huko Ouaka, ambapo kuna mgodi wa dhahabu unaotegemewa nchini, na unaendeshwa na MIDAS RESOURCES yenye uhusiano na Urusi. Pia ktk Kambi ya Roux kuna helikopta 17 bila kujumuisha ndege za Antanov zinazotua Mpangu Airport
Mnamo Januari 23, 24 & 25, 2021 ndege mbili za Antanov zilizosajiliwa Sudan ziliendeshwa na Jeshi la Anga la Sudan hadi Mpoko Airport kupeleka silaha, risasi na vifaa vya kijeshi.
Hiyo ni kulingana na ripoti ya hivi karibuni iliyowasilishwa UN na Baraza la Usalama mnamo June 29.
Kwahiyo, Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, sasahv kwa kiasi kikubwa haina nguvu ya udhibiti ktk maamuzi yanayotolewa na WAGNER.
Uwezo na nguvu ya kampuni hizo mpk sasa haijulikani lkn inasemeka wanajeshi wake hulipwa kiasi cha Rouble 50,000 sawa na Tshs. 1.5M za Kitanzania.
#Inavyoonekana kuachia nchi hiyo sio leo kwa sababu jumla ya vikundi vya waasi anavyongoza FRANCOIS BOZIZÉ vipo 18, kwa pamoja ndio huunda CPC.
Unaweza kutizama hapa uone jinsi vikundi hivi vya waasi vilivyoungana..⇊⇓⇓⇓👇
Mnamo Mei 14, 2021, watu wengi maelfu kwa maelfu walikusanyika katika uwanja wa mpira wa BARTHÉLÉMY-BOGANDA uliopo Jijini Bangui nchini humo.
Hawakwenda kutizama mechi ya mpira BALI kuangali filamu maalum inayoitwa Touriste. Hakukuwa na kiingilio cha pesa isipokuwa miguu yako tu
Tumeshaona #Wagner ilivyo na uhusiano na Rais Vladimr Putin. Wameshamuua Rais Deby (Chad) wameshaidhibiti Sudan & Central Africa
📡Mei 14 kilitokea nini?
📡Wamehamia nchi nyingine, ni ipi hiyo?
Kwa #muendelezo huu
💨Easy Do It👇
RT 🔄 this Thread & Follow me @Eng_Matarra🙏
Urusi imekuwa ikiendelea na agenda zake barani Afrika kwa mgongo inapingana na ukoloni mambo leo.
Ripoti za karibuni zinaonyesha mbinu mpya iliyokuja nayo, ni kufadhili tasnia ya Sanaa, vyombo vya habari na kuendesha kampeni za propaganda kupinga mabeberu ktk mitandao ya kijamii
Mnamo Mei 14, 2021, watu wengi maelfu kwa maelfu walikusanyika katika uwanja wa mpira wa BARTHÉLÉMY-BOGANDA uliopo Jijini Bangui nchini humo.
Hawakwenda kutizama mechi ya mpira BALI kuangali filamu maalum inayoitwa "TOURISTE". Hakukuwa na kiingilio cha pesa isipokuwa miguu yako
Filamu hii iliigizwa nchini humo kwa maudhui ya tamaduni za Urusi na Afrika ya Kati. Lengo lilikuwa kuwapongeza viongozi na Wakufunzi wa jeshi kutoka Urusi wanaounga mkono Rais Touadera, ambaye alichaguliwa ktk uchaguzi (Desemba 2020) na kushinda muungano wa waasi CPC wa BOZIZÉ.
Filamu iliangazia matukio ya vitani, ambapo upande mmoja Warusi waliigiza km Waasi. Silaha zilizotumika sana ni bunduki aina ya Kalashnikov (AK-47) na baadae askari mmoja aliyekuwa amejeruhiwa anaibuka shujaa ktk Vita huku akiwa amekamilisha mission yake.
Ujumbe wa propaganda hii ya filamu ni mahususi kwa ajili ya wanajeshi waliopo ktk kingo za Mji wa Ubangi, lkn hawakuonyesha mienendo yao mibovu ktk nchi hiyo. Kulingana na vyombo vya habari vya Urusi, filamu ya TOURISTE ilifadhiliwa na YEVGENY PRIGOZHIN mkuu wa kikundi cha Wagner
Tangu nchi hizo ziwekeana saini ya makubaliano ya ulinzi mwishoni mwa 2017, Urusi imekuwa ikitangaza ajenda yake nchini humo. Kampuni ya madini ya "LOBAYE INVEST" inayoongozwa na Raia wa Urusi YEVGENY KHODOTOV, ambaye ni mtu wa Tajiri PRIGOZHIN ndiye muongozaji mkuu wa mipango.
Kampuni hiyo imekuwa ikifadhili kituo cha redio cha "LENGO SONGO" kwa sababu ktk nchi hiyo chombo kikubwa cha mawasiliano ya habari kwa wananchi ni Radio Lengo Songo pamoja na LA FEUILLE VOLANTE du PRÉSIDENT, gazeti la serikali ambalo haliuzwi na hutolewa mara moja kwa wiki.
Pia LOBAYE INVEST ilidhamini shindano la warembo kwenye mashindano ya "Miss Central Africa", lililofanyika mnamo Desemba 2018. Kampuni hii haijaacha mahala. Pengine ni ktk upande wa elimu. Imechapisha vitabu vya kufundishia mashuleni.
Moja ya vitabu, kinaelezea katuni moja iliyopo YouTube, inayoonyesha namna Dubu (mnyama) wa Urusi anatokea ktk majani na kuwaokoa wanyama wengine wasiliwe na fisi. Hii ni wazi kwamba PUTIN anatumia mbinu zinazoonekana hafifu kujitangaza lkn WAGNER ikiendelea kujiimarisha Afrika.
Mwanzoni mwa mwaka 2010, Tajiri PRIGOZHIN alianzisha kituo cha "The Internet Research Agency (IRA)" huko St. Petersburg,
kinachotoa habari, lkn sehemu kubwa ya habari hizo huwa ni propaganda.
Dhamira yake ilikuwa ni kuendeleza propaganda za kuunga mkono serikali ya PUTIN
Mnamo 2014, IRA ndio ilikuza mgogoro wkt wa vita nchini Ukraine na kupendelea vitendo vya mauaji vilivyokuwa vikifanywa na majeshi ya Urusi.
Miaka miwili baadaye (2016), kilichangia @Trump kuingia Ikulu na kufanya vichwa vya habari kwenye media mbalimbali kutikisa dunia.
Ndio hao hao walipelekea FBI kutangaza kuwa Tajiri PRIGOZHIN ni "most wanted", kwa shutma za kuingilia uchaguzi Marekani.
Pia ndio wamechangia mgogoro wa rais BASHAR AL-ASSAD wa Syria, pamoja + uongo huko Brexit.
#Inshort:IRA wanaeneza ujumbe wowote ambao bosi wao anataka.
Ktk miaka ya karibuni matajiri wengi wa Urusi akiwemo PRIGOZHIN wamejulikana sana maeneo mbalimbali ya dunia kutokana na kituo cha IRA.
Sema wengi wamejificha ktk kivuli cha ufadhili na wanaiona Afrika kama kisiwa cha kuchota pesa nyingi kutokana na rasilimali nyingi tulizonazo.
Urusi inawaaingia viongozi wa Waafrika kwa kiini macho kupinga 'Neo-Colonialism na kujionyesha wao ni mbadala wa mataifa km USA kwasababu nchi sio washirika wake. Ukitazama vizuri wanautofauti kidogo na CHINA, ambao hukutamanisha kwanza ukiingia tu basi wanajenga uchumi wao.
Warusi wamekuja Afrika basically kutafuta madini
Kwa rekodi ya dunia matajiri wenye pesa, kutoka Urusi haimo ht kwenye Top 20. Lkn ukiingia sekta ya madini wanaongoza. Top 10 ya matajiri ktk uwezekezaji wa madini duniani 03 wanatoka Urusi. Hivyo mchuano ni mkali hasa nchini mwao
Ktk kufanikisha hilo PUTIN hujiimarisha na kiongozi yeyote asiyeendana na yeye huondolewa madarakani.
#Mfn;Okt 23 & 24, 2020, aliandaa mkutano mkubwa (Sochi Summit) na viongozi wa Afrika, ambao ulifanyika Black Sea.
Ktk mkutano huo alitumia wake kuziyaponda mataifa ya magharibi.
Rais Putin alionyesha mipango yake ktk nchi za Afrika, kuwa yupo tyr kuisaidia Afrika ktk masuala mbalimbali ikiwemo biashara na mambo mengine
Mara baada ya mkutano huo kumalizika @Facebook ilitangaza kuwa itavunja mikataba na mitandao yenye inayomiliki na raia wa URUSI ambayo..
ilifanya janjajanga wkt wa uchaguzi ktk nchi 08 za Afrika, ambazo ni CAR, DRC, Côte d'Ivoire, Cameroon, Madagascar, Libya, Msumbiji na Sudan!!
Mtandao ulionyooshewa kidole hapa ni IRA wa kwake Tajiri PRIGOZHIN swahiba wake PUTIN.
#Sababu ilitokana na mifumo ya mitandao inayomilikiwa na Urusi kutumika kwa manufaa nje ya lengo la kanuni na taratibu za habari. IRA ina wadukuzi (hackers) zaidi ya 4300...
..ambao husaidiwa na wafanyakazi wa mashirika ya mawasiliano ya umma kutoka nchi mbalimbali.
Hata hivyo, bado kampeni ya Urusi kujitangaza kwa propaganda mbalimbali haijakoma, na mpk sasa kuna zaidi ya account 750,000 katika mitandao mbalimbali ya kijamii zenye kazi ya moja tu kuitangaza.
“They typically posted global and local political information, including topics such as Russian politics in Africa, elections in Madagascar and Mozambique, election monitoring by a local non-governmental organisation and criticism of French and US politics,” ~ @Facebook
Mnamo Desemba 2020, PALO ALTO ilitangaza kuwa itavunjia mikataba na mitandao yote ya Urusi na Ufaransa, ambayo inafanya udanganyifu ktk nchi kadhaa za Afrika hasa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Wkt huo ilikuwa kipindi cha #COVID19, kutarajiwa kufanyika uchaguzi wa nchi hiyo.
#ForYou:PALO ALTO ni Multinational Cyber Security Company, wakali wa firewalls za aina zote, na zimesambaa kote duniani. Makao makuu yake ni Santa Clara, California.
Watalaam @TOTTechs na @JemsiMunisi wanaweza kuielezea zaidi ikiwa ungependa kufahamu hizo "firewalls" ndio nini..
Moja ya malengo makuu ya wadukuzi wanaounga mkono Urusi ni nchi ya Ufaransa na USA #sababu yao ni ile ile, kuchochea kampeni za kuwapinga kwa kivuli cha ukoloni.
Ktk mkutano huo PUTIN alisema "Waafrika kuweni macho na mataifa ya magharibi, wanawaletea ukoloni kwa mara ya pili".
"Attack Western symbols
Prigozhin and his lieutenants rely on anti-imperialist activists, some of whom are well-known, to feed this anti-French discourse. They identify influencers in the countries they are interested in and pay them off,” ~said French diplomat, Kemi Seba.
Hotuba ya Rais Putin aliituhumu USA na Ufaransa na waandaaji wa mkutano huo alikuwa yeye na Rais al-sisi wa Misri.
Jumla watu 3,000 walihudhuria, ambapo marais kutoka Afrika ni 34 pamoja wawakilishi kutoka nchi 06 akiwemo Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA alituwakilisha.
Kulingana na intelinjesia ya Ufaransa, Urusi ilikutana na ADAMA BEN DIARRA, kiongozi wa harakati ya Yerewolo na mwanachama wa Baraza la mpito la Mali/Conseil National de Transition (CNT), na kumwambia aongoze mapambano nchini kwake watamsupport.
📡Mei 2021, BEN DIARRA aliandaa maandamano kadhaa mjini Bamako ambapo waandamanaji walifika zilipo ofisi za Ubalozi wa Urusi kuishinikiza Ufaransa iondoke nchini humo,ingawa alishawahi kukanusha kupokea ufadhili wowote wa nje.
“I have never had any contact with a Russian.
"Not a diplomat, not a businessman, not a soldier, not even a journalist. All our actions are financed by membership fees. There is no external funding, except for money sent by the diaspora. Everything that is organised by Yerewolo is financed by Yerewolo,” ~Ben Diarra.
Pia, Serikali ya Urusi hutugemea sana nguvu yao nyingine ktk mitandao na vyombo vya habari.
#Mfano;Mjini Paris kuna Ofisi moja ya wahariri inayoitwa @5putniko inayotoa habari kufunika taarifa zote mbaya za Urusi dhidi ya Afrika
Nchini Cameroon kuna Television inayoitwa Afrique Media TV, imelipwa US$ 1M kuisafisha Urusi nchini humo. Kabla hawajaingia makubaliano na Urusi kiongozi wake JUSTIN B TAGOUH alipata ufadhili wa kuendeleza kutoka kwa Marais TEODORO NGUEMA (Equitorial Guinea) na IDRISS DÉBY (Chad)
Wkt TAGOUH akiwa Paris, mtoto wa Rais wa Equitor-Guinea ambaye pia ni Vice-president, TEODORÍN NGUEMA OBIANG MANGUE, alikuwa akishtakiwa kwa ufisadi nchini Ufaransa
Hivyo, TAGOUH alipewa pesa kumsafisha
Kwa Deby aliiona runinga yake inavyosifia Ufaransa kwa kupambana na ugaidi.
MAUAJI YA RAIA & WAANDISHI📌
UN imekuwa ikipokewa ripoti nyingi za mauaji yanayoendelea nchini Afrika ya Kati
Na kutokana na shinikizo la Jumuiya za Kimataifa, baadhi ya waandishi wa habari walijitosa.
#MFANO; Mnamo Julai 2018, kesi za mauaji ya waandishi 03 raia wa Urusi waliokwenda kufanya uchunguzi wa shughuli zao ziliripotiwa kutekelezwa na vikosi vya WAGNER.
💨Mnamo Feb 21, mtu mmoja akiwa hana silaha alipigwa risasi na kufariki papo hapo huko Ippy.
💨Mnamo Jan 13, walemavu 02 walipigwa risasi na kufariki karibu na Paoua na Grimari.
💨Machi 8 pia, wengine wawili kutoka kabila la Fulani waliuawa huko Gotchélé kwa kuhisiwa ni waasi
Mnamo 2017 & 2018, chanzo kimoja cha usalama kilisema: "Putin anataka kumzidi alama Rais Emmanuel Macron (Ufaransa), kwa sababu alikuwa amechaguliwa tu. Ukizingatia ardhi nzuri yenye rasilimali nyingi WAGNER anacheza mchezo wa kuvizia huku akimpiga Rais Touadera."
"Hata serikali ya Urusi ikikataa kuwa haihusiki na yote yanayofanywa na WAGNER nchini humo bado Ikulu yake imeweka mizizi ktk miji mikubwa ya nchini hiyo kibiashara, kijeshi na kisiasa." Kinasena chanzo hicho.
HISIA ZA WAGNER KUHAMIA MALI
Kwa wiki kadhaa sasa vikosi vya WAGNER vimeripotiwa kupungua mjini Bangui. Inasemekana pia ht Kiongozi Mkuu wa kampuni hiyo, ZAKHAROV, amesimama kutumia akaunti zake za mitandao ya kijamii na hatembelei mara nyingi mji huo km ilivyokuwa awali.
Inasadikika Rais PUTIN amemwambia ZAKHAROV kujichimbia ili kupunguza mvutano uliopo baina ya nchi yake, Ufaransa na Baraza la Usalama.Pia siku za karibuni kikosi cha usalama wa Rais Touadera, kimeonekana kuundwa na Waafrika tofauti na zamani ambapo wengi walikuwa Warusi.
Hata mwezi June alipoondolewa madarakani Mh Ngrébada, waziri mkuu wa nchi hiyo, imetokana na shinikizo kutoka Ufaransa, kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa karibu sana na serikali ya Urusi lkn ni kufix tu na ground mambo ya PUTIN yanaendelea.
📌Je! Tajiri wa Urusi YEVGENY PRIGOZHIN anaangalia upeo mwingine?
#Ripoti zinasema watu wa Wagner walionekana mjini Bamako (Mali) mwishoni mwa 2019, wakitaka kuanzisha biashara ili kuweka upinzani na Ufaransa, walisema wataendelea kutoa huduma zile zile walizotoa Afrika ya Kati
Tangu Kanali ASSIMI GOÏTA alipochukua madaraka nchini Mali ilibainika kuwa alioshirikiana kufanya mapinduzi, Mfn MALICK DIAW, Mwenyekiti wa Baraza la serikali ya mpito (Conseil National de Transition), SADIO CAMARA (waziri wa ulinzi) wote na GOÏTA walifundishwa nchini Urusi.
Kulingana na vyanzo vya jeshi la Mali, DIAW na CAMARA walipewa mafunzo huko Moscow kutoka Januari hadi Agosti 2020, siku chache tu kabla ya kufanyika mapinduzi. Pia kuna kampuni moja ya Ufaransa iliyotoa mawasiliano yaliyofanywa na wasaidizi wa Kanali GOÏTA kwenda nchini Urusi.
Ufaransa ilipoteza ushawishi kwa serikali ya Afrika ya Kati baada ya Operesheni Sangaris kuisha. Nchi hizi mbili sasa zina tofauti kubwa sana, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba hali hiyo inaweza kufanyika nchini Mali mara baada kumalizika kwa Operation Barkhane nchi za Sahel.
Ufaransa ina wasiwasi zaidi hasa nchi jirani ya Chad.
#Kw7bu Kampuni ya WAGNER imejiimarisha sana huko LIBYA na ipo karibu sana na kiongozi wa nchi hiyo KHALIFA HAFTAR. Zipo taarifa zinasema kampuni hii ya kijasusi tyr imeshaanza kufanya mawasiliano na viongozi waasi wa Chad.
Kifo cha Idriss Deby kilitekelezwa na waasi wa FACT ila silaha, magari na Sniper walitoka kampuni ya Wagner ya Urusi.
Emmanuel Macron na kijana wake Mahamat Idriss Déby, karibuni walijadili juu ya uhusiano kati ya waasi wa Chadi na Wagner mwanzoni mwa Julai ktk Ikulu ya Élysée
Mnamo Mei 30, 2021, wanajeshi 05 kutoka nchini Chad walikamatwa kisha kunyongwa ktk mpaka baina ya nchi hiyo na Afrika ya Kati. Ilisemekana walitekwa na mercenaries wa #Wagner ili kupata taarifa nyeti za serikali ya Idris Deby. Kisha wakawaachia ktk mikono ya waasi na kupelekea.
BILA shaha A, B, C kuhusu kampuni ya #Wagner sasa imeshakuijia
Naam ndio WAGNER wenye kampuni yake PRIGOZHIN swahiba wa Rais Putin.
Imetekeleza matukio kadhaa, na bado inazidi kutanuka. Ktk nchi 39 zilizohudhuria #SochiSummit nchi 12 zimekubali Russia kuleta ulinzi ja vifaa.
END___🙏
Nikupongeze uliyefuatilia Uzi kutoka mwanzo mpk mwisho
📜Dondosha comment ikiwa una lolote
SOURCES:
1. Scanner Project @munscanner
2. Scope (scopedata.org)
3. CNN (edition.cnn.com)
For more Threads....
💨 Easy Do It👇
RT🔄 Follow me @Eng_Matarra

Loading suggestions...