Leyla Mohamed
Leyla Mohamed

@LeyAllyie

16 Tweets 8 reads Oct 30, 2021
Waswahili wenzangu wanasema, "Mcheza kwao hutunzwa", nimepokea kwa furaha mno nafasi hii adimu ya kuendesha kipindi cha #ElimikaWikiendi kuwaelimisha vijana wenzangu kwenye mada husika!!
Basi Usikose kuungana na mimi ndani ya #ElimikaWikiendi mapema kesho 4:30- 5:00 ASUBUHI
Kama mfanya biashara unachotakiwa kufahamu,ni namna sahihi ya kutumia mitandao ya kijamii ili kupata matokeo chanya kwenye biashara,
Ungana na mimi tuchambue ndani ya #ElimikaWikiendi
Iwe ndio unaanza kufanya biashara ya mtandaoni, au tayari unafanya biashara
#ElimikaWikiendi
1. Matumizi ya Hashtag
Tayari tumeona namna ambavyo hashtag zina nguvu hapa @Twitter hivyo hivyo kama kwenye platform nyingine ambazo zinaruhusu matumizi ya hashtags mfano mzuri ni kama #Twittergulio na nyinginezo
Tumia Hashtag ambazo ziko mahsusi kwa kwako, photo: @socialcut
Tumia hashtag zinazotrend,ili post zako ziwafikie watu wengi zaidi hata wasio kufollow,pia tumia hashtag mazungumzo kuizunguka biashara yako,kwa kuongezea tumia hashtag ambazo zina uhusiano na post yako ila sio lazima zihusiane moja kwa moja na brand yako #ElimikaWikiendi
2. Takwimu zinaonyesha wateja asilimia 19% ya wateja hughairi kununua kutokana kukosa uaminifu wa tovuti za kufanyia manunuzi wakiwa kwenye kuwasilisha taarifa za kadi ya benki(Credit card) au kufanya muamala wa kifedha,
Nini kifanyike kuepuka hili?
#ElimikaWikiendi
Tengeneza au post maudhui yanayoonyesha,hakiki za wateja waliowahi kununua bidhaa zako, waweza post shuhuda za walowahi nunua kutoka kwako,au hata Blogpost kutoka kwa wateja wa awali,pia hivi karibuni kumekuwa na umaarufu kwenye kutumia washawishi (influencers) #ElimikaWikiendi
3.Himiza wateja wako waweze kushare mrejesho wa safari zao za manunuzi na kueleza walitumia njia gani kuweza kuondokana vikwazo kwenye kufanya malipo
Wahimize wateja wako kushare mrejesho wao kwa kupost mtandaoni
Wape wateja misimbo ya punguzo (discount codes)
#ElimikaWikiendi
4.Tengeneza Maudhui ila usiyafanye yakawa ya Kimauzo kupitiliza au ya kusukuma/kulazimu wateja kununua
Unapotengeneza maudhui ya kimauzo kupitiliza itakupunguzia ushiriki katika post yako ya mauzo, kumbuka mitandao ya kijamii haipo mahusisi kwa mauziano, zaidi #ElimikaWikiendi
5. Tumia mtandao wa @LinkedIn mahususi kwa ajili ya uhamasishaji wa bidhaa, ushirikiano wa kimkakati na kampuni zingine, kuzalisha miongozo (generate leads), na kujenga ufahamu (Build awareness) kwa njia mbali mbali kama kuwa na LinkedIn groups,LinkedIn Display Ads.... ⬇️⬇️⬇️
Pia kwa kutumia LinkedIn Sponsored Inmail, kwa kutumia hii yapaswa kutengeneza ujumbe wenye mashiko ya kimauzo kama utashindwa kufanya hivi mwenyewe ni lazima upate mtaalamu kama @NyandaAmosi ili akusaidie kufanya hivyo
#ElimikaWikiendi
6. Tumia matangazo yanayolipiwa (Paid Ads)
Kupost maudhui mara kwa mara au kujibu comments za wateja wako haitoshi kuongeza mauzo,moja wapo ya njia sahihi ni kutumia kwa usahihi mitandao kufanya matangazo yanayolipiwa.
#ElimikaWikiendi
7.Tumia Shoppable Tags kwenye @instagram stories
Kama una E Commerce store yako hii itakusaidia sana ku drive traffic kwenda kwnye bidhaa zko ni wakati sasa mambo yahamie mtandaoni 😊 kutengeneza E Commerce store ya bidhaa zako si gharama tena.Tupunguze Ubahili #ElimikaWikiendi
8. Matumizi ya washawishi wa mitandao ya kijamii.(Social Media Influencers)Hii ni moja ya njia zangu pendwa
Washawishi wa mitandao ya kijamii ni watu ambao wana number kubwa ya wafuasi(followers) mitandaoni, katika Karne hii watu huamini washawishi kuliko ndugu #ElimikaWikiendi
9. Tumia machapisho ya muingiliano (interactive) kuelimisha na kuwasisimua wateja,
Tofauti na juhudi za kawaida za kutafuta masoko, kutafuta masoko mtandaoni,ni tofauti kabisa😊,
Wafuasi wako wa mtandaoni (followers) wanahitaji maudhui ya kuwaburudisha #ElimikaWikiendi
10. Tambua Soko Lengwa lako (Target market) na Jukwaa lipi wanapenda kutumia,
Hii ni muhimu mno kwa wafanya Biashara kuzingatia.
Kuna platform kwa kila bidhaa..
Namna ya kujua ipi ya kutumia ntazungumzia kwa kina zaidi kipindi kijacho. #ElimikaWikiendi
Kwa nyongeza ningependa kuwajuza wafanya biashara wote kuwa njia hizi zote hufanywa kwa ufanisi na kuzingatia muda, kila platform ina ambavyo italeta matokeo kulingana na muda,
Kwa kukazia kuna msemo unasema huwezi kuwapa wanawake 9 ujauzito na kutegemea mtoto ndani ya mweziπŸ”₯

Loading suggestions...