SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

12 Tweets 542 reads Feb 21, 2022
Ujinga ni nini? Madhara ya ujinga na matibabu yake.
Huu ni uziđź§µ
1/ Watu wengi hua wanakosea kudefine ujinga au mjinga.
Wengi hua wanahusisha ujinga na kiwango cha elimu, fedha, uelewa, nafasi, nk
Wengine huchanganya tabia za mtu na ujinga. Mfn ucheshi, uzungumzaji, nk
Jamii yoyote ile ina makundi manne ya watu;
2/
i. Watu wazuri: Hawa husaidia watu wengine bila wao kunufaika
ii/ Watu werevu: Hawa husaidia wengine huku wao pia wakinufaika
iii/ Watu waovu: Hawa huwaumiza watu wengine ili wao wanufaike
iv/ Watu wajinga: Hawa huwaumiza watu wengine huku na wao wakijiumiza pia
3/ Ujinga unahusisha kufanya vitu;
-Vya ovyo na hatari
-Visivyo na maana
-Vinavyokera watu
-Vinavyoepukika
-Vinavyotisha
-Vinavyopoteza muda
-Visivyotegemewa
Huku akijua wazi hanufaiki na kitu chochote, kwa namna yoyote
Huu sasa ndio UJINGA ama mtu anaye-qualify kuitwa MJINGA
4/ Tatizo la ujinga hauna manufaa yoyote kwa mtu na ktk jamii. Lkn una madhara kwa watu na jamii
Mara nyingi ni ngumu kumtofautisha mjinga (stupid) na mtu asiye na uelewa (ignorant)
Pia ni ngumu kumtofautisha mjinga na mtu anayejifanya mjinga (playing stupid)
Utamjuaje mjinga?
5/
i. Hawajali kuhusu madhara watakayosababisha
ii. Hawajali hisia za watu wengine
iii. Hawataki kujifunza/kubadilika
iv. Wanapenda kujikweza/kuwa juu
v. Hawaoni mbali; hawawezi kuona vitu kabla havijatokea
vi. Wanaona watu wengine ndo wajinga; ila sio wao
6
vii. Hawakubali kushindwa ktk lolote
viii. Wanajua kila kitu kuhusu kila kitu
ix.Hawana utulivu especially kwenye kufikiri, kusikiliza na kuzungumza
x. Hawana aibu
xi. Wasumbufu
xii. Wana-criticize kila mtu na kila kitu
xiii. Wanadiscuss watu na matukio
xiv. Wanapenda kuonekana
7/
xv. Hawana mipaka
xvi. Hawafikirii kabla ya kufanya
xvii. Mara zote wana hasira
Ni rahisi sana kumtambua mjinga online kuliko offline. Pia ni rahisi kumkwepa mjinga online kuliko offline.
8/ Njia rahisi ya kuukwepa ujinga; soma huu uzi, japo niliuandika kwa kingereza.
9/ Njia ngumu; chagua kuwekeza nguvu, muda na attention yako yote kwenye vitu vya muhimu zaidi kwenye maisha yako.
Hapa tunasema “ignorance is bliss” as far as mambo yako yanaenda vzr, huna haja ya kujishughulisha na vitu vingine.
It’s risky, but it works.
10/ Madhara ya ujinga ni mengi kuliko faida
i. Mjinga hujisababishia kujichukia, kuchukiwa na kuchukia watu
ii. Ujinga huleta hofu
iii. Ujinga husababisha uharibifu
iv. Ujinga hukwamisha mipango mema
v. Ujinga hutenganisha watu ktk jamii
11/ Sijui kama tupo tayari kudiscuss topic pana kama hizi; lkn nia ya uzi ni kukukumbusha kukwepa ujinga na kuwakwepa watu wajinga.
Awareness is cure. The earlier the better!

Loading suggestions...