๐‘ฉ๐’‚๐’ƒ๐’‚ ๐‘พ๐’‚ ๐‘ฝ๐’Š๐’‹๐’‚๐’๐’‚ ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ|๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡บ
๐‘ฉ๐’‚๐’ƒ๐’‚ ๐‘พ๐’‚ ๐‘ฝ๐’Š๐’‹๐’‚๐’๐’‚ ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ|๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡บ

@KamigakikuMbise

20 Tweets 683 reads Apr 05, 2022
KWANINI MAOMBI YETU HAYAJIBIWI?
UZI/THREAD๐Ÿงต
~Bwana Yesu asifiwe, najua wengi wetu tumekumbana na hali hii ya kuomba lakini maombi yetu yasijibiwe.
~Leo nitaandika sababu 10 za kwanini tunapoomba wakati mwingine maombi yetu hayajibiwi ili tujifunze kupitia hizo na tuombe...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
Maombi yenye tija na uhakika wa kupata majibu toka kwa Mungu.
1) DHAMBI.
~Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie....๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
tulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu.
๐Ÿ‘‰๐ŸพTwajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
โ€˜Yohana 9:31 SUV
โ€™
๐Ÿ‘‰๐Ÿพlakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
โ€˜Isaya 59:2 SUV
โ€™
(Zaburi 66:18, Amos 5:22-23)
~Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.
2) KUKOSA IMANI.
Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao.
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
โ€˜Ebrania 11:6 SUV
โ€™
~Hapa ni mchezo wa akili yako na nafsi yako juu ya...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
Mungu unayemuomba na kile unachomuomba. Wakati Yesu alipokuwa anaponya watu, mara nyingi sana aliwaambia โ€˜Imani yako imekuponyaโ€™(Luka 17:19) kwaiyo imani ndio msingi wa majibu ya maombi yako kwa Mungu.
~Kiwango cha imani yako ndio kitaamua kiasi cha majibu yako kwa Mungu...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
3) KUKATA TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
~Kuna wakati unaweza kusikia mtu akisema, nimeomba vya kutosha Mungu hanisikii, labda Mungu hanioni. Kauli zote hizi za kukata tamaa hufanya tushindwe kupokea majibu ya maombi yetu. Habakuki aliambiwa โ€˜njozi ni kwa wakati ulioamriwa, na...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
ijapokawia aingojee.
๐Ÿ‘‰๐ŸพHabakuki 2:2-3
~Na muda mwingine majibu yetu yanakuwa yamebeba vitu vikubwa hivyo hukumbana na upinzani mkali, bila kukazana kuomba basi hushindwa kutufikia. Maombi ya Daniel yalizuiliwa kwa siku 21 na mkuu wa anga wa uajemi, kama angekata tamaa basi...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
asingepata majibu ya maombi yake.
๐Ÿ‘‰๐ŸพDaniel 10:12-13.
4) KUJIKWEZA/KUJIHESABIA HAKI.
~Kuna baadhi ya watu hujiona kama vile wao ni zaidi ya watoto wa Mungu na wana haki zote na hawana dhambi na ni lazima wapewe kila wanachokiomba. Kama una tabia hiyo, my friend Mungu hatokaa..๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
ajibu maombi yako, maana Biblia inasema ajikwezaye atashushwa.
๐Ÿ‘‰๐ŸพLuka 14:11
~Yesu aliwahi kutoa mfano wa mfarisayo na mtoza ushuru, mfarisayo alikihesabia haki alafu mtoza ushuru akajishusha na kujiona mdhambi. Yesu anasema mtoza ushuru alihesabiwa haki kuliko mfarisayo...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
๐Ÿ‘‰๐ŸพLuka 18:10-14.
5) KUOMBA BILA KUFANYA KAZI.
~Unakuta mtu anaomba Mungu ampe kazi alafu anashinda nyumbani tu bila kutafuta kazi. My friend, Biblia inasema asiyefanya kazi na asile, kwaiyo kama hufanyi kazi hata kama unamuomba Mungu hawezi kukubariki/kukujibu maana Mungu...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
anabariki kazi za mikono yetu.
๐Ÿ‘‰๐ŸพZaburi 128:2, 2Thesalonike 3:10
Sasa atabariki nini kama hufanyi kazi?
~Kuna wakati siyo kuomba tu, lazima kuambatane na kutafuta na kubisha, ili uweze kuona na kufunguliwa.
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Luka 11:9
6) KUTOSAMEHE.
~Ndiyo! Kutosamehe waliokukosea ni..๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
sababu mojawapo ya kuzuia majibu ya maombi yako. Maana ili Mungu aweze kukusamehe na kukusikiliza inapaswa kwanza uwasamehe wengine kama Yeye anavyokusamehe.
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Efeso 4:32, Mathayo 6:12-15
7) KUOMBA NJE YA MAPENZI YA MUNGU.
~Kuomba nje ya mapenzi ya Mungu ni kuomba nje ya...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
utaratibu wa Mungu au kuomba nje ya mipango ya Mungu aliyokuwekea juu ya maisha yako. Utajuaje kama unaomba nje ya mapenzi ya Mungu? ( Tuombe uzima Mungu akinipa kibali nitaandika)
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ1Yohana 5:14.
8) KUTOAMBATANISHA NA SADAKA.
~Siku hizi ukigusa ishu ya sadaka tu, watu....๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
wanakuwa wakali kama pilipili.๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… Lakini hiyo haiondoi ukweli wa kuwa sadaka ni muhimu sana katika maombi yako.
๐Ÿ‘‰๐ŸพAkupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. โ€˜Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.โ€™ Akujalie kwa kadiri ya haja...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.
Zaburi 20:2-4
~Na ukisoma kwenye Biblia sadaka ni kitu cha lazima, ili kuonyesha utii wako mbele ya Mungu.
Lakini hamaanishi basi ukiambatanisha na sadaka unajibiwa, kumbuka sadaka ya mtu mwovu ni chukizo mbele za Mungu...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
๐Ÿ‘‰๐ŸพMithali 15:8
~Japokuwa sadaka ya kwanza ni moyo wako, na ya pili ni Damu ya Yesu. Hivyo kama huna sadaka unaweza tumia hizo mbili na Mungu akajibu maombi yako kwa wakati na bila shida.
9) KUTAKA KUTUMIA KWA TAMAA.
~Wakati mwingine hatupokei majibu ya maombi yetu kwa kuwa..๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
lengo letu tukipata ni ili kumtambia fulani, kumuumiza fulani, kufanyia anasa za dunia nk. Sasa ukiwa na nia hiyo moyoni mwako Mungu hakujibu ng'o.
๐Ÿ‘‰๐ŸพYakobo 4:3
10) KUTOMKUMBUSHA MUNGU.
~Kumkumbusha Mungu haimaanishi kwamba Mungu anasahau, bali kuna wakati anapenda Uungu....๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
wake uheshimiwe kwa sisi kumkumbusha ahadi yake kwetu na siyo kukaa tu na kusubiri majibu.
๐Ÿ‘‰๐ŸพUnikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
Isaya 43:26
~Huenda maombi yako yako mlangoni pako, ni kiasi tu cha kwenda mbele za Mungu kumkumbusha na...๐Ÿ‘‡๐Ÿพ
kumshukuru nawe utapokea.
๐Ÿ‘‰๐ŸพShukrani sana kwa kuusoma uzi huu, ukikupendeza tafadhali RT kule juu ili ufikie na wengine wapate kujifunza. Ubarikiwe sana.
๐Ÿ‘‰๐ŸพPia unaweza kusoma Nyuzi nyingine nilizoandika kwa kubonyeza link hii hapa chini. ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

Loading suggestions...