S W A D A K T A.
S W A D A K T A.

@swadakta_

16 Tweets 9 reads Aug 24, 2022
HOME & MARRIAGE II
#____UZI
Akili hujenga maarifa, maarifa hujenga mitazamo na mitazamo hujenga fikra na fikra chanya hufanya utambuzi wa mamuzi sahihi
Mamuzi sahihi huleta matokeo mazuri, japo moyo hupenda ila akili huamua, katika Maisha jitahidi sana ufanyaji kazi wa Moyo na akili uwe wenye kushabihiana, hasa kumchagua mwenzi mwema kwako
Ndio maana Uzi uliopita nilielezea vitu gani vya kuzingatia wakati wa kumchagua mwenza wako, tukaangazia awe
Msiri wako, hii itakufanya uwe sehemu salama kupitia yeye, kwani atakuwa ni mwenye Moyo mfano wa ukuta, yale madhaifu pamoja na mapungufu yako yatabaki kifuani kwake hatokuwa tayari kukuvinjia heshima yako
Leo tutaendelea kuangazia vitu gani vya kuzingatia wakati wa kumchagua mwenza wako, ongeza popcorn kidogo here we go
Wakufanana nae, kuanzia mawazo pamoja na mitazamo hata ile mipango yenu na mafanikio yenu hatakuwa mropokaji kwa mashoga zake, hata wale asiewajua kumbe ni maadui zake
Baraka huongezeka zaidi pale unapoifanya Siri, kwani si kila mmoja anapenda mafanikio yako, licha ya kuwa ni mwenye kifua mfano wa ukuta baraka kwenu zitaongezeka kila kukicha
Mwandani wako, umbile lake ni la binadamu ila Moyo wake ni wasimba na kifua chake ni ukuta, ni mwenza ambae ulieshibana nae, hata pale mkitofautiana ni rahisi zenu tofauti ardhini kuzizika
Si mwepesi tofauti zenu social media kuzileta, si wa kwa mwenye kiti wa mtaa kukimbilia, wala mashoga zake kuwadithia, wala mashati na ngumi kukunjana, ila kujishusha ndio kitu kabarikiwa
Mpambanaji, akikuona umeanguka atakuwa mstari wa kwanza kuhakikisha umeinuka, hivi itakuaje unakuwa na mwenza kila kitu anataka umkamilishie
Hata pant anataka umnunulie, vocha umuekee ila haimanishi usimnunulie, Kuna vidogo mwenye anatakiwa amalize na sio kila kitu chake ni wewe, hii itakufanya akupunguzie mzigo
Romantic, kubarikiwa mwenza ambae yupo romantic, kwako atakuwa ni stress remover au pain killer au tabibu wa maradhi ya Moyo wako
Ni vitu vidogo vidogo ila vinaongeza faraja, haijalishi tozo ni kubwa kiasi ganiπŸ˜† ila ukiwa na stress remover unasahau shida
Na asipokuwa romantic anakupea vitu kama hizi, hivi hii ni kitu ya kumpea mtu kweliπŸ˜†
Dear Young Generation: Chagua kilicho bora

Loading suggestions...