S W A D A K T A.
S W A D A K T A.

@swadakta_

20 Tweets 16 reads Sep 03, 2022
LOVE QUOTE
#____UZI
Waswahili wanasema "Ukiona vyaelewa ujue vimeundwa" wakimaanisha kila kizuri chenye kupendeza kimetengenezwa, hakuna kitu kilichojileta ila vimeletwa
Hata kwenye mahusiano ili yaweze kuimarika na kushamiri inahitaji kuyajenga, kwa kutumia nyenzo ambazo zitazidi kuziteka hisia zenu, na kuikuza bustani ya huba kwenu
Kuna njia nyingi kadha wa kadha ambazo huleta matokeo chanya, kama
-zawadi,
-care,
na zingine nyingi, ila Leo tuoneshe kidogo utofauti kupitia mashairi
Mashairi ni moja ya ujumbe ambazo mtunzi hutumia kuelezea hisia juu ya Jambo fulani. Sio mtalamu wa kiswahili ila mmenielewa😁
Tumia mashairi kuzielezea hisia zako kwake, jinsi mlivyokutana mpaka hapo mlipofika sasa
Hii itasaidia kuongeza upendo kwa mwenza wako, kwani ni dhahiri umezieleza hisia zako na Mapenzi yako kwake, licha ya wao hupenda kusikia maneno mazuri kutoka kwa wenza wawapendao
Niazime muda wako kidogo mpwa, ongeza popcorn kidogo here we go
Mueleze mara yako ya Kwanza kumuona, ilikuaje kwako, ni hisia zipi ulikuwa nazo juu yake👇
Ilikuwa mara ya Kwanza kuonana, pale macho yetu yalipogongana
Nawe ukatamani kuniona, taratibu tulitazamana
Eye contact tukachezeana, ila aibu tukaoneana
Kuumbika kwake👇
Kukuona nilihisi nimebahatika, kwa jinsi ulivyoumbika
Umbile lako mithiri ya malaika, mzuri umekamilika
Muda ule moyo wangu uliuteka, haikuwa rahisi mimi kuchomoka
Kiu yako kumuongelesha👇
Muda sikutaka kupoteza, nikatamani kukuchombeza
Kichezo kikanicheza, nikajiuliza hivi hapa nitaweza
Bado nikazidi kujiuliza, itakuaje Kama nikimpoteza
Like damn hapa nitaweza
Nikatamani sauti yako kuisikia, vile ukiongea
Salamu nikakusalimia, nawe ukaitikia
Ilikuwa nzuri yenye kuvutia, hapo ukazidi zaidi kuniua
Sikua na pakuchomokea, maana nilihisi naongea na customer care
Harufu yake👇
Nilivyozidi zaidi kukusogelea, harufu nzuri waridi ulinukia
Pua zangu zilifurahia, manukato yako sikutaka kunipotea
Kumbukumbu yako ilibakia, akilini nikikufikiria
Mikono yake👇
Hata mikono yako nilipokushikilia, ilikuwa laini Kama malkia
Sikutamani kuiachia, mwingine kukuchukua
Nilihisi nitaumia, ila popote uendapo nitakufatilia
🛑Kwa hapa Leo tutaishia, part II soon tutaendelea😝
Dear Young Generation: Ukishindwa kumpigia kumuimbia, jitahidi ujumbe kumtumia

Loading suggestions...