Unaambiwa "Kabla hujasema Mapenzi sio pesa jitahidi kwanza uwe na pesa" wengine husema "Pesa ni sabuni ya roho" wengine "Pesa ni mwisho wa matatizo" basi kila mtu na msemo wake
Tupo kwenye ulimwengu ambao ili uweze kuishi(ku-survive) unahitaji pesa, pesa ambayo itakayoweza kuendesha mfumo mzima wa maisha yako
Pesa ambayo itamaliza shida ndogo ndogo zako malazi, mavazi, na vingine vingi kadha wa kadha, hata kuenjoy na mwenza wako inahitaji pesa
Ni utandawazi pekee unaleta taswira ambayo ili uonekane na Mapenzi ya dhati kwa mwenza wako lazima uwe na pesa, vile utakavyom-spoil, unamhonga (sio vibaya), atakacho anapata, popote atakapo mnaenda kujivinjari
Ukiwa na pesa utakuwa na mwanamke yoyote umtamkae, mwenye shape ya kuvutia, mzuri mithiri ya Malkia ni wewe tu, Swali ni kweli utamaliza wanawake wote duniani.? utalala na wangapi.? Faida yake ni ipi.?
"First get the money, then get the power, Respect" ukiwa na pesa utakuwa na nguvu (ya kufanya chochote), ukiwa na pesa utaheshimika (popote), Kama unataka vyote ivo kuwa na pesa
Najua mnamipango yenu tayari, ila naweza sema pesa inamchango mkubwa wa kutupatia wenza ambao si sahihi kwetu, wenza ambao wapo kimaslahi, wenza ambao wanataka luxury Life
Wengi tunachukulia Mapenzi Kama starehe, ila hatuchukulii Kama sehemu ya Maisha yetu, Kama nguzo ya kuandaa future yetu, kuandaa kizazi chetu, kuandaa watoto bora kwetu
Kwa kuwa tunaamini pesa ndio inayomtongoza mwanamke, pesa ndio kila kitu kwa mwanamke, mwanamke akiona pesa hachomoki, basi tunatumia nguvu ya pesa Kama udhaifu wake
Tayari wanaume tunajitengenezea uoga, tunapoteza ile maana ya "Real Men" kutumia uwezo wako wa kuongea maneno mazuri ya kuweza kuziteka hisia za mwanamke
Ukitaka kujua wanaume wa sasa ni waoga, wakitaka kutongoza mara zote wanatumia njia ya simu(text, au kupiga), face to face anapoteana, na akiona unamkazia njia pekee ni pesa
Unaambiwa "sikuizi hatutongozi pesa ndio inayoongea" na hapa ndio watu hupigwa Pesa, ila niwaambie kitu hakuna njia nyepesi ya kumpata mwanamke kama kumtongoza face to face, huwa hana confidence, wanaaibu sana,
Unaambiwa "sikuizi hatutongozi pesa ndio inayoongea" na hapa ndio watu hupigwa Pesa, ila niwaambie kitu hakuna njia nyepesi ya kumpata mwanamke kama kumtongoza face to face, huwa hana confidence, wanaaibu sana,
Kwakuwa ni muoga badala yake unatumia nguvu ya pesa, na huu ni mtego mgumu Sana kwa mtoto wa kike kuukwepa kwasababu ya tamaa(levels)
Wanawake wengi wamejikuta na tamaa za kuishi Maisha ambayo yapo juu ya uwezo(level) zao, anataka luxury Life uwezo hana, kila photo dump ashiriki, basi inampasa awe na mwanaume mwenye pesa
Na mwanaume hashindwi kukupatia pesa, na kukutumia atakavyo kwani anajua udhaifu wako, na hana kitu Cha kupoteza, baada ya kutumika anampasia mwanae "Oya mali ile unajipigia kikubwa kibunda tu"
Hao ndio wanaume, dear Ladies utatumika mpaka lini, kwanini usiridhike na hali (level) ya Maisha yako, kwanini usitafute mkaka mwenye upendo mkajenga Maisha nae, na mkizipata utajivinjari nae, bata nae, party nae
Kwanini uishushe thamani ya mwili wako kisa pesa, zaidi utaishia kudhalilishwa, kuingiliwa kinyume na maumbile, utapata maradhi, hata kuhatarisha Maisha yako, tamaa zenu ndio zinawafanya kuwaona wanaume ni wadhalilishaji
Dear Men, utalelewa mpaka lini, kwanini usitafute mwanamke wa level zako mwenye akili mkajenga Maisha nae, mapenzi utayafanya starehe mpaka lini, walikuwepo kabla yako Leo hii wako wapi, Mashangazi yatakuua, uchi haushibi
Ukitaka kujua Mapenzi na Pesa haviingiliani ndo maana mke wa baharesa hajulikani
Dear Young Generation: Mapenzi bado yanadai pesa, ni muhimu kuwa nazo