SIR JEFF⚡🇹🇿
SIR JEFF⚡🇹🇿

@Sirjeff_D

14 Tweets 46 reads Oct 11, 2022
Katika maisha yng sijawahi kufanyiwa job interview,so sijui experience inakuwaje mtu akiwa intervied
Ila, nimefanikiwa kuinterview mamia ya watu,nikimsikiliza mtu kwa dakika 10 tu najua km anafaa ama hafai
Kuna vitu employers huangalia,ukiwa navyo vitakutofautisha na wenzio
🧵
Watu wengi wanaingia kwenye chumba cha interview na fikra potofu.
Wengi wanazungumzia experience zao
Wengi wanazungumzia juhudi na jitihada zao
Wengi wanazungumzia elimu/ufaulu wao
Wengi wanazungumzia qualifications zao
WRONG APPROACH
Utatembeza sana CV!!
Employer anakutana na mamia ya watu wenye elimu, ufaulu, juhudi nk; ili kustand out of the crowd inabidi uwe MEMORABLE & RELATABLE
1. Memorable
First impression matters, simaanishi ukivaa suti utapata kazi ama ukivaa jeans utakosa kazi. HAPANA!
Unatakiwa usitoke kichwani kwa…
Employer. Unabidi ukumbukwe na interviewers siku ya interview na baada ya interview. Unafanikishaje hili?
Master the art of telling YOUR story
Utakumbukwa kwa kuzungumzia story yako kwa umakini, usahihi na uhalisia
Jifunze storytelling utaongeza chance kubwa ya kuwazidi wenzio
Unajua kwa nini hii ni muhimu?
Kwasababu employer anatamani ajue wewe ni mtu wa aina ganinq misingi yako ni ipi, kabla hajaanza kufanya kazi na wewe.
Employer anapenda mtu ambae yupo interesting atakayeweza kubond vzr na teammates.
Ukiacha kuwa Memorable lazima uwe Relatable
Story yako lazima uiblend irelate na story ya employer.
Hapa utahitaji ukusanye taarifa nyingi sana kuhusu hiyo kampuni.
Anza na Webpage yao, soma taarifa zao Google na LinkedIn
Hizi taarifa hazitakusaidia kitu chochote kama huwezi kujua jinsi ya kuzitumia
Wala hukusanyi hizi taarifa ili ujibu vzr maswali utakayoulizwa. Hapana.
Hizi taarifa unazikusanya ili uzitumie kufanya story yako iwe relevant and relatable.
Epuka sana kujibu maswali ya kwenye interview km vile unafanyiwa upelelezi na askari.
We are not interrogating you
Fanya interview as if unafanya tu conversation ya kawaida.
Relax na kuwa confident kama vile unapiga story na employer wako, lkn sasa story yako iwe inaweza kurelate vzr na majukumu ya kazi yako.
Usifanye kosa la kujielezea maisha yako mfn.
Naitwa Jeff, nilisoma SM Mapito, baada ya hapo nikaenda Sekondari Kilifi, kisha chuo nikaenda kusoma blah blah.
TERRIBLE mistake. Hii ni km mwanafunzi anajitambulisha. Hakuna employer atakua interested na hizi story za kitoto.
Kosa la pili ni kusema
-I’m hardworking
-I’m team driven
-I’m passionate
Kila mtu kwenye interview hua anasema hivi, na wewe ukisema hivi unakua boring.
Ongelea vitu vinavyokufanya uwe unique, uwe tofauti na wengine lkn pia onyesha kwanini wewe ni legendary kwa namna yako
Kosa jingine watu wengi wanafanya ni kuuliza irrelevant question.
Mara nyingi employer akimaliza interview anakupa chance ya kuuliza swali.
Watu wengi hua wanasema hawana maswali. Wengine hua wanauliza majibu ya interview yanatoka lini, wengine wanaulizia mshahara.
Hutoboi!
Uliza maswali relevant mfn
-Kwasasa changamoto gani mmezipa kipaumbele cha juu zaidi ktk position uliyoomba kazi
-Yapi matarajio ya kampuni kwa miaka mitano ijayo
-Department gani nitakua nafanya nayo kazi zaidi, na muingiliano wa majukumu upoje.
Kadri unavyouliza maswali relevant ndivyo unaonekana upo serious na hiyo kazi.
Kuuliza maswali relevant haimaanishi uulize ‘when was the company founded’.
Sehemu unayotakiwa kuonyesha userious hutakiwi kuuliza maswali ambayo majibu yake yanapatikana Google in 5 seconds.
Mwisho wa thread ila nawatakia Graduation njema wadogo zangu wa UDSM mnaofanya mahafali leo. Hongereni sana na karibuni mtaani!!

Loading suggestions...