Kila mtu anapenda kupendwa, kwani hakuna kitu kizuri Kama ukihisi unapendwa, na upendo huanza na kujali, kadri unavyozidi kuzijali na kuzizingatia hisia za mwenzio ndio Mapenzi hupatikana
Kama hutajali basi hutakuwa na Mapenzi ya kweli, wengi tunatamani kupata wenza sahihi, wenza ambao watakufungulia ulimwengu mpya wa Mapenzi moyoni kwao, akupatie huba la upendo wao
Skuizi kupata mwenza sahihi, imekuwa Kama kutafuta hazina iliojificha kwenye kina kirefu cha bahari, huku ikizungukwa na maji na kufunikwa na miamba migumu na imara yenye kuhitaji ufanisi ili uweze kuifikia
Inahitaji uwe na uvumilivu, imani na kuwa na Vifaa imara na madhubuti utakavyoviamini vitakavyoweza kupasua miamba migumu ilioificha hazina ili uweze kuipata
Tumewekeza hisia zetu kwa wenza ambao tulihisi ni sahihi kwetu, wenza ambao tulihisi wataipa faraja mioyo yetu, wenza ambao tuliwekeza hisia zetu kwao, ila tuliambulia maumivu Kama mshahara wetu
Wengi wenye mioyo yenye Mapenzi ya dhati wanabati ya kukutana na watu ambao sio sahihi kwao, hawakufungua mioyo yao kuyapokea Mapenzi hayo, ila wali-fake na kujifanya kuwa pamoja nao
Waliambulia maumivu na kukosa Imani na Mapenzi tena, na kujitengenezea Imani mioyoni kwao bora kupiga unatembea "hit and run"
Jamii ya watu wa Hit and Run ni watu ambao si kwa kupenda kwako kuwa ivo, ila walibadirishwa na aina ya watu ambao walikutana nao kwenye Safari ya mahusiano yao
Kipi kiliwafanya kuwa kwenye jamii hiyoรท
Uwekezaji, pale utakapopenda ni rahisi kuwekeza, kwasababu unatengeneza mazingira ya muonekano ambao kila unapomtizama unasikia raha moyoni, kwani ndio pumziko lako, ndio pambo lako
Japo kuna aina tofauti za uwekezaji, wengine wamewekeza kwa kusomesha, wengine kumpendezesha, wengine kumfikisha, wengine kumpatia muda, wengine kupata familia
Unajitahidi kufanya kila njia ili uridhishe nafasi yake, ahisi upendo wako, upo pale kwa ajili yake ili tu apate kila hitaji la moyo wake, ila bado hakuona thamani yako
Malengo, ni ndoto ya Kila mtu kuwa na malengo na mtu ambae anahisi ataenda nae safari moja ya maisha, kesho awe Mama watoto wake, kesho awe baba watoto wake, akupatie familia bora
Utakapowekeza hisia zako basi hapo ndio una malengo napo, kila mtu anatamani kuzeeka na pacha wake (maana mkiishi muda mrefu mnaanza kufanana), ila wengi mipango yao haikuzaa matunda
Ukweli humfanya mtu kuwa huru ni vyema Kama huna mpango nae, mueleze asiwekeze kwako wala asiwe na malengo juu yako
Dear Young Generation: kabla hujawekeza muulize mipango yake