S W A D A K T A.
S W A D A K T A.

@swadakta_

14 Tweets 5 reads Dec 29, 2022
WEEKEND NA COMPANY
#____UZI
Weekend huonekana ndefu zaidi hasa unapokuwa mwenyewe, upo wewe Kama wewe, mpweke, huna company, huna mwenza, weekend zako zote zinaisha ukiwa ndani Kama balbu
Ikiwa Kama ndala zinakuja pair iweje wewe uwe single, najua ni muda mrefu Sana upo single, si kwamba unapenda Hapana kwani hakuna Furaha ya kuwa single
Ni muda wako sahihi wa kutafuta mwenza wako, utajiuliza huyo mwenza tampata wapi, Leo takupa machimbo na baadhi ya maeneo muhimu utaweza kumpata mwenza wako
Licha ya kuwa na week ngumu yenye purukushani huko maofisini, mara nyingi watu hutumia weekend kurefresh, kujichanganya na watu wapya, hata kujenga urafiki mpya ili kupata mawazo mapya, Wengine hupendelea kwenda
Beach, Kama unavyojua kila mtu na hobby yake Wengine hupenda kuogelea, basi huchukua Muda wao kukata maji, kupunga upepo kidogo, kupunguza stress za Maisha
Ukipata chimbo la mtoto yupo mwenyewe jisogeze taratibu ukimfikia anza Kumsifia
Mfano "Aliekuumba kakupendelea"
"Nguo zako za kuogelea zinakufanya unavutia zaidi"
Kisha utamchombezea "Naweza kupata company yako Madam.?"
AF msikilizie atakujibu Nini
NB:Punguza wenge
Cinema, Huku utawapata wapenda movie chagua siti yako Moja yenye utulivu aliyokaa mtoto Mmoja safi msogelee kisha msifie
Mfano "Manukato yako yanakufanya unanukia vizuri" Kisha muombe ukae pamoja nae AF msikie atasemaje
NB: Akikataa usilazimishe
Point(Juice, Ice cream, Kahawa n.k), Muda mzuri wa kutembelea hizi point ni mida flani ya jioni ivi, Kama unavyojua watoto wanapenda vitu vidogo vidogo hizi ni sehemu zao pendwa kuwepo
Ukishapata point yako, mpwa unawaka kwanza, Kisha unapulizia unyunyu wako wa afu sita unatokea maeneo. Kanuni yetu ni ile ile unamtupia sifa kidogo Kisha unaomba company
Mfano "Gauni lako la blue limekukaa vizuri mwilini kwako"
"Hereni zako zinakufanya unavutia zaidi"
"Macho yako mazuri"
NB: Sifa utakazomsifia hakikisha anazo
Najua mtasema tafuta hela wanawake sio wagumu, ila ukweli ni kwamba unaweza kuwa na Hela bado ukakataliwa
Dear Young Generation: Ongeza Juhudi Weekend zisikupite kizembe

Loading suggestions...