#TOTTechs
#TOTTechs

@TOTTechs

6 Tweets 17 reads Jan 03, 2023
Kubadili CPU kwenye computer yako haina tatizo na computer inakuwa sawa tu.
Kitu cha msingi na cha kuangalia pindi unabadili CPU ya computer ni cooling system, ukiweka CPU yenye TDP rating kubwa (Thermal Design Power) kuliko mfumo wa cooling wa computer (stock OEM cooler) 👇
Kitakachotokea hapo ni kwamba mfumo uliopo utashindwa kuipoza CPU na itachemka na kutofanya kazi ipasavyo hulazimu kujipoza (downclock to keep itself cool)
kama unabadili CPU na unaweka yenye ubora wa juu kwenye computer hiyo hiyo (CPU is from a higher end model of the same PC)
Mfano ulikuwa na DELL computer yenye Intel Core i5 unaweka Core i7 of the same model hizi huwa zinakubali maana ziko designed ku-fit TDP (Thermal Design Power) ya CPU ya juu yake.
Kama unabadili CPU na unataka kutumia OEM Cooler (Original Equipment Manufacturer)..
Ya computer hiyo hakikisha unasafisha thermal paste iliyokuwepo na kuweka thermal paste nyingine.
Thermal paste zinasaidia sana kupunguza joto kwenye CPU
Namna ya kubadili thermal paste litakuwa somo jingine...
Pia unashauriwa ku-download hardware monitoring tool kama CPU-Z kwa ajili ya kuangalia CPU temperature, CPU temperature inatakiwa kuwa angalau 40°C - 50°C na pia isizidi 90°C kwenye utendaji kazi (processing power) ikizidi hapo ujue kuna tatizo angalia cooling system
Kama CPU inafanya kazi na ikachemka kuliko kawaida, computer yako itajizima yenyewe (Thermal shutdown) ili kuzuia kuunguza CPU basi ikitokea computer yako inachemka sana na kujizima angalia cooling system ya computer yako haiko mounted ipasavyo.
ASANTE.

Loading suggestions...