ғɪʜᴀᴠᴀɴɢᴏ
ғɪʜᴀᴠᴀɴɢᴏ

@FihavangoJr

10 Tweets 5 reads Feb 01, 2023
#Jifunze Bure👇
☆VITUFE VYA AC
~Hivi ni vitufe hurusu hewa ya upepo wa baridi au joto kutoka kwenye vents za gari. Vitufe hivi huwa na controller ambavyo unaweza kuongeza kasi ya upepo. Ukiwasha controller bila kubonyeza vitufe hivi utatoka upepo BILA baridi au joto.
☆Kitufe cha AUTO
~Kitufe hiki kinasaidia kuset joto la kwenye gari kwa kiwango flani,bonyeza kitufe hiki kisha set kiwango cha joto au baridi unalotaka,AC itapoza gari lako kwenye kiwango ulichoweka na itakaa kwenye kiwango hicho hicho bila kupunguza wa kuzidisha.
☆Vitufe vya RECIRCULATION
~KItufe hiki kinafanya kazi ya kuzungusha hewa iliyondani ya gari badala ya kuchukuwa hewa nje ya gari, ukibonyeza kitufe hiki ina maana hewa itakayotumika ni iliyo kwenye Cabin. Tumia kitufe hiki kama nje ni Joto kali au kuna unyevu/ Ukungu.
☆Kitufe cha FRESH AIR
~Kitufe hiki kinamaanisha AC yako inachukuwa hewa kutoka nje ya gari na kuiingiza garini kupitia vents. Mfumo huu unatumika kama hewa ya ndani ya gari ni ya unyevu au inajoto kuliko hewa ya nje ya gari.
☆Kitufe cha Defrast:-
~Kitufe hiki maalumu kutoa ukungu,kikibonyezwa kinatoa upepo wa joto kwenye vent za mbele kabisa ya gari chini ya kioo cha mbele (WINDSHIELD)hivyo kusaidia kuondoa ukungu kwenye kioo cha mbele.Kitufe hiki maalumu sana kukijuwa hasa wakati wa mvua/baridi
☆Vitufe vya AIR FLOW:-
~Hivi vAinaitwa MODE CONTROL,hapa unaset sehemu gari upepo unatokea:-
1.Upepo unatokea vent ya Dashboard na vent ya chini.
2.Upepo unatokea vent ya chini.
3.Upepo unatokea vent ya kwenye Dashboard.
4.Upepo unatokea vent ya chini na WINDSHIELD.
Asante kwa muda wako kujifunza Elimu hii👆
Karibu kwa maswali/Maoni/Kazi kutengenezewa gari yako🙏🙏📞
@usedpointTz Asanteni waungwana🙏
@msitapixel Asante kaka somo👆

Loading suggestions...