Sunday Victor
Sunday Victor

@sundey_fx

21 Tweets 9 reads Feb 05, 2023
Kama umehitimu chuo kikuu na upo home una mchongo wowote wa kukuingizia pesa, njoo nikushauri kitu.
Kama umehitimu chuo 2018-2022, utakua upo kwenye umri wa miaka 20-30 around hapo.
Sijui una degree ya fani gani may be haijaanza kukuingizia pesa sio muda wakukata tamaa
-Uzi-
Kila mwaka wahitimu 500,000+ wanaingia kwenye soko la ajari ila ni 100,000 tu ndio wanapata nafasi ya kuajiriwa na serikali plus private sector.
Swali la kizushi.
Hawa wahitimu 400,000 wanaenda wapi?
Mimi sina majibu ila kama na wewe upo kwenye hili kundi soma huu Uzi.
99.9% ya graduate wameenda shule kwa lengo la kusoma fani flani ili wapate ajira ili kujikwamua na umasiki na kukwamua familia zao.
Yes! Hilo ndio lengo mama,
Ila kwa sasa imekuwa kawaida kabisa kwa graduate kukaa mtaani miaka mi 5+ bila kupata ajari kabisa.
Mambo yamebadilika sana tofauti na enzi za wazee wetu, wao walikua wanapata ajira wakiwa bado wanasoma.
Jana nilikua napiga story na bibi yangu anasema yeye aliajiriwa serikali na elimu yake ya darasa la 4, hakuwa na fan yeyote wala degree.
Sasa hivi mambo hayo hivyo kabisa.
Kama ume hitimu chuo na umeshatembeza CV zako kila mahala ila ngoma bado ngumu, huu sio muda wakukata tamaa kabisa. Never!
Mimi personal nina ushahidi wavijana ambao mwaka wa 5 hawana ajira ila wana maisha mazuri sana, na wengine wapo hovyo.
Tumezaliwa kwenye kipindi Cha bahati sana kuliko vipindi vyote kuwahi kutokea ulimwenguni.
Kiza cha internet (Internet revolution).
Hichi ni kizazi kizuri sana.
kuwepo kwa internet kume rahisisha mambo mengi sana.
Internet imeleta mabadiliko makubwa sana kwenye hii Gene.
Kwa nini nasema imeleta mbadilko makubwa kwenye generation yetu.
Unaweza kutumia internet vizuri kabisa na ukatengeneza utajiri.
Vitu kama,
Financial Market
Cryptocurrency
Social media
Google
Na platforms mbali mbali, ambazo hatuweza kutaja zote hapa.
Huna haja kuanza kulalamikia serikali na kulamu watu, anza kutumia internet au mtandao kujitengenezea kipato chako binasfi.
Unaweza kuchukua miaka 10 unalalmika ila hakuna kitu kitabadilika kwenye maisha yako
Zaidi utaendelea kuisha maisha magumu na muda unazidi kukutupa mkono.
Unaweza kuanza kuamtumia internet kutengeneza ajira yako?
Sasa hapa weka ego yako pembeni, weka vyeti na CV zako kapuni kwanza.
1. Fanya visualization.
Kaa chini chora ramani ya maisha yako miaka 10+ badae.
Hii ni vision au picha unavyojiona miaka 10 mbeleni.
Fikiri vitu ambavyo unatamani kumiliki.
Fikiri nyumba unayotaka kuishi, fikiri familia, fikiria gari unalotaka kuendesha.
Hapa imagine maisha,
Yatakavyokua mazuri endapo uta achieve hivyo vitu unavyo wish kua navyo kwenye maisha yako.
Usiishie hapo tengeneza VISION yako, iandike kabisa kwenye note book.
Mfano 2019 mimi niliandika vision yangu nikaipa jina.
"Vision 2030"
Jichimbie siku nzima Ji assess vizuri.
2. Fanya utafiti ni ujuzi gani unatakiwa kuwa nao ili kufikia vision yako.
Chukua paper andika ujuzi wote unaweza kukuingizia kipato mtandaoni.
Ingia google/YouTube/Quora, search
"10 solid ways to start make money online 2023"
wewe ni graduate so kimombo sio issue kabisa.
Kuna njia zaidi 100 utanikuta na mna ya kuingiza pesa online.
Mimi nilupata bahati ya kufanya hivi nikiwa chuo 2017.
Nilikutana na njia zaidi ya 100+
Nitataja chache tu.
Affiliate Marketing
Digital products
Forex Trading
Copywriting
Freelancing
Blogging
Sale
3. Chagua ujuzi mmoja unaona utakufaa.
Hapa kwenye kuchagua unapaswa kuwa makini sana kuangalia ujuzi unaolipa vizuri na kuendana na personality yako.
Kuna ujuzi unaolipa vizuri ila unatakiwa Kuwa hustler wa ukweli mtandaoni.
Linganisha kati ujuzi na ujuzi.
Then chagua 1 tu.
Unaweza kuchagua kulingana na fani yako au isi relate kabisa na fani yako.
2017 nikiwa chuo mzumbe nikiwa nasoma Sheria nifanya maamuzi magumu ya kuchagua financial markets.
Kwa nini maamuzi magumu?
Sikua najua chochote kuhusu financial markets.
Hakuna mtu wangu wa karibu
Alikua anajua how financial markets works particularly forex trading.
Sasa hapa unaweza kuunganisha na ujuzi unaoendana.
Kuna baadhi ya skillsets ni mandatory aisee.
Mfano, writing, content Creation, copywriting, persuasion, brand and audience building.
4. Anza kwa kujisomea mwenyewe.
Kun watu watakuambia lipia course kwanza, No!
Anza kujifunza wewe ili usiwe mweupe kwenye hiyo skill.
Ingia google YouTube Quora huko kote search skill uliyochugua then pakua haswa.
Tenga masaa 4-6 kwa siku jichimbie kula nondo.
5. Tafuta Mentor.
Sasa hapa haupo mweupe kabisa, wewe una ABC za hyo skill uliyo chagua.
Mentor ni mtu aliefanikiwa kwenye hicho kitu unachotaka kukifanya.
Wengi Wana charge mentorship program, ila sio cost full kama ada ulilipa ku graduate bila kupata ajari.
6. Jiposition sokoni.
Kuna njia nyingi sana zakuanza kujiweka sokoni ila njia rahisi nikitumia mitandao yakijamii.
Anza na Twitter, LinkedIn, Facebook na Instagram, ni bure kabisa, naamini hii mitandao unatumia kila siku.
Anza kushare madini yote uliojifunza free.
7. Tengeneza Skillset.
Skillset ni muunganiko wa ujuzi mbali mbali.
Skillset za muhimu ni hizi hapa;
Sale
Writing
Copywriting
Content Creation
8. Tengeneza huduma au bidhaa anza kuzaa mtandaoni.
Andika ebook, funndisha wengine ujuzi ulionao, uza bidhaa au huduma za watu wengine.
Kosea, Jifunze, Anza upya.
Utakua umefungua biashara yako mtandaoni na kuanza kuingiza pesa.

Loading suggestions...