17 Tweets 60 reads Feb 23, 2023
NAMNA SAHIHI YA KULIPIA SPONSORED ADS INSTAGRAM.
UZI 🧡🧡🧡🧡🧡🧡🧡🧡🧡
Uenda ulijifunza tu namna ya kulipia lakini ukaishia kua unapoteza tu pesa yako bila kupata matunda basi soma hii mpaka mwisho.πŸ‘‡πŸ‘‡
Hakikisha kwanza akaunti yako ina bio/wasifu/profile nzuri.
Pia akaunti iwe na post nyingi za bidhaa au huduma unayotoa.
Wateja lazima watachungulia akaunti yako kuona cha Ziada na wakakikuta ueleweki imekula kwako.
Mfano wa bio/wasifu mzuri wa akaunti πŸ‘‡.
Basi twende sasa kwenye kutengeneza tangazo letu kwaajili ya malipo.
Hatua ya kwanza post picha/video nzuri unayotaka kutangaza.
Waka caption nzuri ya kushawishi wateja.
Kisha baada ya kupost bofya neno boost post/chagua Lengo.
Bofya create your own yaani tengeneza mwenyewe.
Watu wengi ukimbilia kwenye automatic yaani Instagram ndio ikuchagulie watu wa kuona.
Audience name wabatize mwenyewe jina lolote wateja wako
Baada ya apo bofya location.
Kuna namna mbili za kuseti location kulingana na mipaka pia huduma za biashara yako.
Regional ni maeneo makubwa mfano mikoa/nchi.
Utasearch mkoa mwenyewe na kuseti na unaweza ongeza zaidi ya mmoja.
Usipo fanya hivi ni sawa na kutangaza offer za Zantel mtwara badala ya zanzibar .
Local ni mipaka ya karibu na ww yaani yenyewe unaset automatic kwenye eneo la....
Biashara ni 30 km kwa duara lkn.
Local ni kwaajili ya wafanyabiashara ambao Biashara au huduma zao azivuki mipaka mikubwa.
Mfano unatangaza huduma ya Choo cha kulipia karibu na soko la karume mm umeacha hadi watu wa mwanza tunaona ni matumizi mabovu ya pesa yako
Interest chagua watu wa aina gani unataka waone bidhaa yako kupitia vitu wanavyopenda mtandaoni.
Kwa kawaida mitandao ukusanya taarifa zetu kila siku kama watumiaji kupitia search,page tunazotembelea,watu tunaowafollow ,hata dm ndo zinatumika na insta kukuletea interest.
Mfano unaweza ukawa unapiga story sana za mazoezi whatsapp na wadau wako.
Harafu ukiingia Instagram unakutana na matangazo ya GYM au fitness sababu ni taarifa zako za interest zimeuzwa kwa Mfanyabiashara.
Baada ya apoπŸ‘‡πŸ‘‡
AGE & gender yaani umri na jinsia.
Watu upuuzia kuseti na kuacha 18 mpaka 65.
Jiulize wazee wa miaka 65 wakiona jinsi ya michaniko unayouza watanunua πŸ˜…??
Ni wangapi wenye umri wa miaka 18 Tz wanaweza kununua nyumba unayouzaπŸ˜…??
Usitupe pesa bure seti umri na jinsia pia ....
Bofya iyo βœ” apo juu kuendelea.
Bofya next kwenda kwenye malipo.
Ikifunguka kwenye malipo utaseti kulingana na budget yako mfukoni.
Msatari wa juu ni kiasi cha pesa kwa siku moja ...mfano mimi apo nmeweka dola 1 kwa siku.
Msatari wa chini ni idadi ya siku tangazo kuonekana. Mfano nmeweka siku 6.
Kupata jumla ya pesa ni dola mara sku 6= na dola 6 ambayo ni sawa na 7500tshs.
Bonyeza next kuendelea.
Bofya payment method,.
Add payment method.
Chagua visa card/Master card.
Jaza taarifa za kadi.
1.Jina la kadi yako
2.namba ya kadi yako
3. MM/YY ni Mwezi na mwaka wa kadi yako ku expire mfano 18/23
4.CVV namba 3 zipo kwenye card yako zmeandikwa cvv
Bofya save.
Itakurudisha hapa bonyeza boost
Watakwambia sbr wana review tangazo lako kisha baada ya masaa kadhaa letapostiwa.
Karibuni kwa maswali.
Kuhusu master card ya simu soma huu uzii
Sorry kwenye hesabu za dola 6 nimeweka rate ya dola 3 kikubwa mmeelewa tu.

Loading suggestions...