BAD NUMBER🥷🏿
BAD NUMBER🥷🏿

@ByDurahRich

11 Tweets 51 reads Feb 21, 2023
KWANINI MUNGU ALIKATAA DHABIHU YA KAINI NA KUIPOKEA YA ABEL?
Mpaka ikawa Chanzo cha Kaini kumuua nduguye Abel…..👇👇
Kwanza tuangalie kamusi neno dhabihu ni nini?
Dhabihu kwa jina lingine ni “kafara”, zilikuwepo sadaka za kafara na vile vile zilikuwepo zisizo za kafara.
Katika agano la kale, kafara zilizokuwa zinatolewa kwa Mungu ni kafara za wanyama, kama kondoo, mbuzi na ng’ombe.
Ambapo, mtu binafsi au Taifa zima litamsogeza huyo mnyama mbele za Bwana katika hema yake,
na kuhani atamchukua huyo mnyama kama ni ng’ombe,
au mbuzi au kondoo na kumchinja na kutwaa damu yake na kufanya upatanisho kwa huyo mtu au kwa Taifa,
na kutwaa baadhi ya viungo na kuvichoma juu ya madhabahu.
Sasa sadaka ya namna hiyo ndiyo inayoitwa dhabihu.
Zilikuwepo sadaka nyingine ambazo hazikuwa dhabihu.
Kwamfano sadaka za unga, sadaka za mazao, sadaka za fedha, sadaka za nguo, za malimbuko n.k hizo hazikuitwa dhabihu..
Dhabihu ni sadaka ya kafara inayohusisha mnyama kuchinjwa na damu kumwagika.
Leo hii tumezoea kusema “tunaenda kumtolea Bwana dhabihu tukimaanisha sadaka zetu za fedha”..
lakini kiuhalisia hizo sio dhabihu tunazotoa bali ni sadaka tu!. Na zina baraka zake kubwa tu!,
Lakini haziitwi dhabihu, ingawa hatutendi dhambi pia kuziita hivyo.
Haya Sasa turudi kwa Kaini na Abel kusummarize kidogo;
Adam na Hawa walizaa watoto wawili nao ni Kaini na Abel, Abel akawa mchungaji wanyama na Kaini akawa mkulima.
MWANZO 4
“Baada ya muda, Kaini alileta baadhi ya mazao ya shambani ili ayatoe kuwa dhabihu kwa Yehova.
4 Lakini Abeli alileta baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake, pamoja na mafuta yao.
Yehova alipendezwa na Abeli na dhabihu yake, 5 lakini hakupendezwa hata kidogo
na Kaini na dhabihu yake. Basi Kaini akawaka hasira kali na kusononeka”
KIKAWA KISA CHA KAINI MUUA NDUGUYE ABEL
“Baada ya hayo Kaini akamwambia Abeli ndugu yake: “Twende zetu shambani.” Basi walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.
9 Baadaye, Yehova akamuuliza Kaini: “Yuko wapi Abeli ndugu yako?” naye akajibu: “Sijui. Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
10 Basi Mungu akasema: “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia kwa sauti kutoka ardhini.
11 Na sasa umelaaniwa kwa kufukuzwa
kutoka katika ardhi ambayo imefungua kinywa chake ili kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako”
Kwa sababu ya Kaini kufanya hivyo juu ya nduguye Mungu alimlaani, lakini bado kaini kati ya uzao wake alizaliwa Enoko aliyeenenda mema na kunyakuliwa na Mungu.
SWALI: Kuna jamaa kupitia hiki kisa akaniuliza,
Ni kwanini Mungu alikataa dhabihu ya Kaini ikiwa alikua ni mkulima na ndio ilikua stahiki yake?
Pia ikiwa alilaanika na kizazi chake mbona Enoko alifuata njia za Mungu mpaka kutokufa kama wengine bali kunyakuliwa na Mungu?

Loading suggestions...