9 Tweets 2,113 reads Feb 25, 2023
NAMNA YA KUTUMIA CHUMVI YA MAWE KUJISAFISHA KIMWILI.
Unaweza tumia chumvi ya mawe kujiondoa dhidi ya nuksi, vifungo vya kichawi(Sio vyote vyengine unahitaji wataalamu wa kiroho kulingana na imani yako), mikosi na mabalaa ya kiimani.
Unaweza tumia kwa kuogea, kuchoma au kutupa
njia panda...haya yote unayaweza fanya kulingana na tatizo linalokusumbua.
Zipo njia nyingi zaidi za kujisafisha dhidi ya vifungo ila hii imekaa kiwepesi kueleweka kiasi bila utata mwingi na wajuaji😂.
1. KUOGEA.
Hapa utachukua chumvi yako ya mawe kisha utachanganya na maji
yako ya kuogea kiasi cha kijiko kimoja au zaidi kisha utasema lile unalotaka liondoke kwenye maisha yako(kama ni nuksi, mikosi, jini etc)..tumia siku saba au zaidi kulingana ukubwa wa tatizo lako.
Sio lazima uogee bafuni ila ni muhimu sana ikiwa hivo. Chooni mara nyingi dawa
Hupungua nguvu maana ni sehemu chafu zaidi kiroho(fatilia wengi wanaoanguka chooni). Kama huna bafu ni vyema ukaogea nje au kwenye beseni ndani kisha maji ukamwaga nje.
2. KUCHOMA
Hapan utaibeba chumvi yako ya mawe kwa mikono miwili kisha utaanza kuotililisha moton huku ukinena
uyatakayo. Moto uwe wa mkaa au kuni(Usiwe wa gesi).
3. KUTUPA NJIA PANDA.
Hii ni kwenda na chumvi njia panda kisha unaibeba viganjani ukiwa umegeuka upande utakaoondokea kisha unanenea uyatakayo na kuitupa mikono miwili nyuma yako na usigeuke nyuma hadi ufike.
Hii njia nzuri
kama umewekewa tego(wale kawekewa akigonga demu mzigo hausimami😂).
Au kama una majini pia ni nzuri.
Unaweza weka chumvi kwenye hela zako kuzuia chuma ulete(unaweza tumia mkaa au ndulele etc)
Unaweza tumia chumvi kuweka kwenye nyuma yako au pembe za chumba chako kuzuia wachawi
Unaweza tumia chumvi kuweka chini ya kitanda chako kukurahisishia kuwahi kupata usingizi na kutoota ndoto mbaya.
Unaweza tumia chumvi ya mawe kulegeza kifua chako kinachobana kwa kulamba.
Haya ninayoandika ni kwa ufatiliaji wangu tu na sio kwamba mimi ni mganga wala mchawi.
Unakuta umeelezea apa kila kitu afu mtu anakuja DM anauliza yaleyale uliyoandika as if hakusoma au hakumaliza...ukija ntakwambja hilo hadi ulipie😂.
Kama haikufai acha mimi sipo kukuaminisha.
Unaweza mcheki @munno__ anauza chumvi ya mawe nzuri sana kwa matumizi haya au waweza nunua sehemu yoyote ya maduka asilia au masokoni.

Loading suggestions...