OPTIMIST ⚔️
OPTIMIST ⚔️

@abbycool2_

15 Tweets 11 reads Apr 01, 2023
Siku ile napita mitaa ya kati uswahilini,.. Si kuna washkaji wamekaa kama mtu 8 hivi..
Basi kuna mdada naye alikuwa anakatisha pale maana hakukuwa na njia nyingne.. Ni pisi flani hivi ya kwenda..
Si unajua washkaji hatutakagi kupitwa au kuonekana si kitu.
Basi msela mmoja akajipindua kuiita ile pisi.. Psiii psii we mrembo.. pisi haikuwa na nongwa wala nini si ikageuka ikasogea😁.. Si ameitwa bana, Kasogea mpk walipo washkaji, jamaa aliyemuita ghafla akanywea😃 Mwamba hana cha kuongea....
Demu kamkazia mshkaji,, wewe hapo umeniita aya niambie, mshkaji anazuga tu ooh sijakuita mara sikumaanisha jamaa anatetemeka washkaji nao wanamchora tu jamaa wameacha mtu mbili ziongee, mwisho demu kasepa mwamba akapata ahueni 😁😁
Sasa hii kitu si mara moja naiona kuna ile upo katikati ya washkaji ndo unajikuta mwamba unaita pisi ili uonekane tu sio mvivu ila kiuhalisia ukiwa mwenyewe hauwezi kumsemesha...oya sasa ngoja nikwambie..
🔨Haijarishi pisi ni ya moto kiasi gani.
🔨Haijarishi ana maringo kiasi gani
🔨Haijarishi ana nafasi gani..
🔨Haijarishi una wasiwasi kiasi gani
🔨Ondoa hofu ya kukataliwa..
Mtafutie target mfate, msemeshe usioneshe nia ya kumtaka kiviile..
Usimuone tu ukamfata kuomba namba... We sio wakala msajiri bro😀
Njia rahisi ya kumuwin msichana ni kumfanya avutiwe na wewe😃 hujaelewa!!
Unaongeaje!... Una nini cha tofauti!.. Unaonekanaje!!
Usioneshe kumtaka kupita kiasi au kumuangalia kwa kumuona..
Yeye ni bora kuliko wengine..hiyo hali aliyonayo ishusha muweke awe wa kawaida then then chukua attension yake ..
Mwanaume ameumbiwa kushawishi, Mwanamke ameumbwa kushawishiwa..
Ondoa hofu, kukataliwa kunaanzia akilini mwako..kataa nafsi ya kukataliwa, nguvu ya kushindwa, nguvu kukusukuma chini..Jiamini mfate mwambie.. Akikataa, tafuta njia nyingine mwambie akizingua achana nae focus na mambo yako..
The way unaongea na wasichana wengi..the way kujiamini kunaongezeka japo mtu kama sisi ma introvert tunajikutaga kina nani sijui😬...hatutakagi kuwapa airtime mademu.. Ata tukiwapa ni katika ile low key,
Ok sasa kwenye kumshawishi usijiweke katika hali ya chini wala juu sana, usijiweke katika hali ya kuonewa huruma do just for your own sake..
Ngoja nikupe katrick mwanangu ka kitaalamu zaidi....
Unapoomba namba usianze na maneno kama , naomba namba yako. Au nipe namba yako, at unaweza nipa namba yako!!
Oy fanya hivi..mpe simu ukiwa umeanzisha 0.. Then niandikie namba yako
Au unamwambia tu namba yako ni 0.. Oy sasa akishakutajia una 0718819246..
Badala ya 6 mwisho we mzingue..ooh mwisho 9 hapo atakurekebisha..hapo umesha mvuruga atension yake sasa ..me sio mbobevu hapo ni kwa mujibu wazee wa hizo kazi akina Casanova au mwamba @isaack_nsumba 😀
Ngoja masaa ata 24 yapite then mtext sms moja kausha never overtext her au kupandishia sms juu ya sms ambayo haijajibiwa..
Anza kumvuta taratibu aone we ni bonge la kampani muda anaokuwa hana mood..
Ila sasa...usiwe unapatikana kila muda, yaani sio kila muda atakao kutext au kukucall akupate.. Jaribu kuwa hadimu muda mwingne..kuna kathamani tu utakaongeza
Usionekane huna majukumu ata kama ni jobless😃 usionekane kiasi akuhamu,
Sio mtaalamu mimi, fanya uazime ata mashairi ya shakespere, au gabriele au ata mwanangu @heisbixen Au @isaack_nsumba
Ni hayo tu.
Grab it or pita hivi!
#Firstmate was here!
@abbycool2_

Loading suggestions...