Adellah Tillya
Adellah Tillya

@AdellaTillya

12 Tweets 91 reads Apr 15, 2023
Tunapoongelea Wanandoa kugawana mali tunaongelea Talaka. Hakuna Mgawanyo wa Mali zilizotokana na Ndoa bila ya kuwepo Talaka.
:
Kisheria Talaka inapotoka, hatua inayofuata ni mgawanyo wa Mali na Mustakabali wa Watoto kama wapo ikiwa ni pamoja na Matunzo yao.
Tunapoongelea Wanandoa kugawana mali tunaongelea Talaka. Hakuna Mgawanyo wa Mali zilizotokana na Ndo...
Mali siyo lazima magari na nyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo Vitanda, Makabati na Samani navyo ni mali kwa mujibu wa Sheria
:
Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika ni ule wa nusu kwa nusu, (50 kwa 50). Huo si mtazamo wa Sheria ya Ndoa,
1971 Sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho 2002 bali ni Mtazamo wa Mtaani
:
Sheria tajwa imeweka Msingi Mkuu wa Mgawanyo wa Mali ambao ndiyo hutumika Mahakamani kutoa maagizo ya kugawa mali baina ya Wanandoa Kifungu cha 58,60 (a) na 61 vyote vya Sheria husika vimeelekeza jambo hilo
Msingi uliowekwa na Sheria tajwa hapo juu ni kiwango cha mchango wa Mwanandoa katika kupatikana kwa Mali bishaniwa. Katika suala hilo kiwango alichochangia Mwanandoa katika kupatikana kwa mali ndicho kitakachokadiriwa kuwa ndicho anakachostahili kupata.
Mfano; Kama ni nyumba ya vyumba 6 mmoja anaweza kupata 1 na mwingine 5 kutegemea na mchango wa kila mmoja
:
mchango siyo lazima iwe leta ni lete au Shilingi kwa Shilingi bali hata kazi za nyumbani anazofanya Mama/Mke au Baba/Mume wa nyumbani ambaye hana kipato nazo huhesabika.
KATIKA KUTENGANISHA MALI HUWEKWA KWENYE MAKUNDI MAKUU MATATU
:
KWANZA
Mali ambazo Mwanandoa alikuwa nayo kabla ya kuoana au alikuja nayo wakati anaingia kwenye Ndoa. Mfano: Mwanamke au Mwanaume ameolewa au kuoa akamkuta tayari ana nyumba hiyo haitachukuliwa kuwa ni Mali ya Ndoa.
KUNDI LA PILI:
:
Mali ambazo zimepatikama wakati wawili hao wakiwa tayari, ndani ya ndoa. Mfano: Ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja kwa taratibu wakaanza kujenga nyumba na kuikamilisha. Vifungu vya 59 na 60 (b) vya Sheria ya Ndoa, vinahusika.
KUNDI LA TATU:
:
Mali ambazo zimepatikana kwenye ndoa lakini hazina uhusiano wa kindoa. Mfano: Mmoja wa wahusika kurithi au kuzawadiwa mali fulani. Kifungu cha 61cha Sheria ya Ndoa kinaelezea.
KABLA NA BAADA YA NDOA:
:
Mali iliyopatikana kabla ya ndoa na ikaendelea kuwapo kipindi cha ndoa inaendelea kuwa ya huyo mmliki, bila ushirika wa mwenza wake, kwa mujibu wa kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa.
Kama ni nyumba mwanamke alikuwa nayo kabla ya kuolewa au ni mwanaume,
alikuwa anamiliki basi inaendelea kuwa ya kwake peke yake na haihusiki katika mgao pindi itakapohitajika kufanya hivyo
:
Hata hivyo Mali husika inaweza kuingizwa katika mgao ikiwa kuna mchango wowote wa kuiendeleza uliotolewa na mwenza (Mke au Mume) au kwa mhusika kuamua mwenyewe
bila kulazimishwa, mali ihusishwe kama mali ya familia au Mali ya Ndoa
:
Mfano: Kabla ya ndoa Nyumba ilikuwa na vyumba viwili lakini ktk kipindi cha ndoa imeboreshwa na kufikia vyumba vitano (5) au ilikuwa haina uzio, au madirisha kabla ya ndoa lakini baadaye vitu hivi vikawepo.
Hali kama hiyo itatakiwa iingizwe ktk mgao na kutazama kiwango cha mchango wa kila mmoja ktk uendelezaji, mchanganuo utafanyika ili kila mmoja apate haki kutokana na kiwango cha mchango wake Ikiwa hakuna uendelezaji nyumba inabaki ya Mwanandoa mmoja ambaye ndiye mmiliki wa awali

Loading suggestions...