Isaack Nsumba
Isaack Nsumba

@isaack_nsumba

26 Tweets 98 reads Apr 24, 2023
Viini Vya Dharau Ya Mwanamke Kwa Mwanaume
UZI (Shuka Nao)
Wakati Mwingine Mwanaume Anaweza Pitia Hali Fulani ya Kudharauliwa na Kuchukuliwa Poa Bila Kujua nini Sababu ya Hayo Yoote.
Leo Nataka Nizungumzie VIINI Vya Dharau ya Mwanamke Kwa Mwanaume
Yaani, Mambo Ambayo Yanaweza Kumchochea na Kuichoea Dharau ya Mwanamke....๐Ÿ‘‡
Mwanaume Akiweza Kuyahughulikia Haya Ni Rahisi Kuepukana na HALI YA KUDHARAULIWA.
Kwanza Natamani Kwa Wanaume Woote Ifahamike Kuwa KILA MWANAMKE ana DHARAU, Lakini Hakuna Mwanamke Ambae Anaweza Kumdharau Mwanaume Bila Sababu.
Yaani, Ili Mwanaume Aheshimike Lazima Kuwe na Sababu ya Kwanini Anastahili Kuheshimika...lakini pia Ili Mwanaume Adharauliwe Lazima Kuna Sababu Inayopelekea Kudharauliwa.
Brothers, Ukiyajua Mambo Haya Yatakusaidia Sana Kujua Namna Gani Unaweza Kudeal na Hali ya.....๐Ÿ‘‡
Mwanamke Kukudharau...Tujaghe Ng'wanavane. (Twenzetu Wanangu)
1. Hali ya Mwanamke Kumzidi Mwanaume.
Kisaikolojia, Ni Vigumu Sana Mwanamke Kumuheshimu, Kumtii na Kumnyenyekea Mwanaume Ambae Anamzidi Mambo Kama Elimu, Fedha, Umri, Cheo, Umaarufu na Ushawishi.
Asilimia Kubwa Mwanamke Atakapofika Hatua ya Kuanza Kujihisi "Huyu Mwanaume Kuna Moja, Mbili Tatu Namzidi" Anapoteza Hamasa na Sababu ya Kumuheshimu.
Japo sio kwa wanawake woote, ila tafiti zinaonesha kuwa wanawake walio wengi huwadharau sana wanaume waliowazidi.
Na hii inaonekanaga wazi hata wakati mwanaume anamfukuzia mwanamke, mwanamke akihisi tu kuwa kuna vitu anamzidi mwanaume kuna namna anaanza kumdharau.
Kuzidiwa huko kunaweza tokea ndani ya ndoa, ghafla mwanamke anashika hela, anapanda cheo, anaongeza elimu anaanza dharau
2. Mwanamke Kubeba Gharama za Maisha Kwa Sehemu Kubwa.
Ikitokea Mwanamke Ndiye Akawa anabeba majukumu kwa sehemu kubwa ni mwanzo wa mwanaume kupoteza heshima yake kama mwanaume.
Wapo wanaume wengi tu ambao mara baada ya kufilisika, kuyumba kiuchumi, kupoteza kazi..๐Ÿ‘‡
wanawake zao ndio walianza kubeba gharama za maisha na dharau zilianzia hapo.
Lakini pia, hata kumuacha mwanamke ajihudumie kwa kila kitu ni kukaribisha dharau, mwanamke humuheshimu sana mwanaume ambae anamuwajibikia.
Ikitokea mwanamke akasuka kwa hela yake, kodi akalipa kwa..
hela yake, kama ana gari mafuta akaweka kwa hela yake..ni rahisi sana kumdharau mwanaume.
Tena ikifika point mwanaume akaanza kubebwa na mwanamke ndio kabisaaa, yaani unaenda kwa mwanamke unakula na kulala bila kutoa hela...lazima udharaulike.
3. Being To Nice; Kuwa Mwema/Soft Kupitiliza
Kiuhslisia, Mwanamke Humdharau Mwanaume Ambae ni Mwema Kupita Kiasi, Mwanaume ambae mwanamke atafika hatua ya kuhisi kuwa "HUYU NINAMUWEZA, HANA UJANJA"
Yaani kila atakalosema mwanamke mwanaume anaitikia "SAWA MAMA"
kila atakachotaka mwanamke jamaa anasema "Usijali mama, mi nakusikiliza" mwanaume wa sampuli hii lazima adharauliwe.
Mwanaume hapaswi kuwa soft na mwema kupita kiasi, a man must be gentle and mascular and not nice and desperate to a woman (azima dikshonari)
Sio Mwanaume anakuwa kama bendera, popote upepo utakapivumia yeye yumo humo...Mwanaume lazima awe TOUGH, sio unapelekeshwa-pelekeshwa kirahisi.
Uwe na uwezo wa kusimamia misimamo na mipaka yako bila kupepesa macho (kama unajihisi uko sahihi)
kuwa mwanaume unaewezekanika lakini isiwe wakati woote.
4. Mwanaume Mwenzako
Nadhani umewahi sikia msemo unasema "ukiona mbwa wako anakubwekea basi ujue kuna mtu anampa mifupa mizuri" huu msemo una maana kubwa sana.
Wakati mwingine kiini cha wewe kudharauliwa ni mwanaume mwenzako ambae amekuzidi kete, yaani tayari ameshauteka moyo
wa mwanamke wako na amempa sababu ya kumuheshimu yeye na kukudharau wewe.
Kiuhalisia kama sio wewe uliyesababisha kudharauliwa basi kuna mtu amesababisha wewe udharauliwe na yeye aheshimiwe....hii ipo na inawatokea wengi tu.
Upendo wa mwanamke umeambatana na heshima, siku upendo wake ukihamia kwa mwanaume mwingine anahamisha na heshima +attention huko upendo ulikohamia.
Na hakuna dharau mbaya kama dharau inayorokana na mwanaume mwenzio, yaani kuna mtu ambae anamfanya mwanamke wako akudharau wewe.
5. Kutokukupenda.
Nimewahi Kusema Kuwa "Upendo Wa Mwanamke Umeambatana na HESHIMA, UTII na UNYENYEKEVU" yaani mwanamke akikupenda vizuri...
Atakupa Heshima, Atakupa Usikivu na Unyenyekevu kama BONUS...na Asipokupenda hivyo vitu vitatu hautaviona...๐Ÿ‘‡
kwahiyo dharau wakati mwingine huashiria KUTOKUPENDWA.
Yawezekana asikupende kabisa, au yawezekana aliwahi kukupenda lakini hivi sasa hakupendi tena..kama aliwahi kukupenda manake aliwahi kukuheshimu.
Kama hivi sasa hakueshimu manake hakupendi,
yeees...si tumekubaliana kuwa upendo wa mwanamke unaambatana na heshima...upendo ukitoweka na heshima nayo inajisepea.
Ni rahisi namna hiyo..hi hesabu sio ngumu hata kuielewa (upendo wa mwanamke=heshima)
6. KUTOKURIDHIKA WAKATI WA TENDO.
Hii Nimeona Niiandike Kwa Herufi Kubwa Kabisa Ili Uibebe Kiuzito...Mwanaume Unapaswa Kuhakikisha Hauna Matatizo Yafuatayo๐Ÿ‘‡
1. Kuwahi Kumwaga (Premature Ejaculation) 2 kushindwa kurudia Tendo/Kukosa Hamu ya Kuendelea (Low Libido) Kusimamisha Kiulegevu (Erectile Dysfunctioning)
Hii ni Kwa sababu, matatizo niliyoyataja yanakupunguzia uwezo wa kiutendaji kitandani (Reducing you perfomance during sex)
Na uwezo wako ukiwa mdogo ni wazi kuwa hautakuwa ukimsugua vizuri mwenzi wako..na kama usipomsugua vizuri ni wazi kwamba hatoridhika na kama hatoridhika ni wazi kuwa ITAATHIRI HESHIMA YAKE KWAKO.
Hivyo ni eneo la kuwa nalo makini sana!
Niliwahi Fundisha Somo Katika Semina ya Wanaume linaitwa "THREE MAIN PILLARS OF MANHOOD" (Mihimili Mikubwa Mitatu ya Uanaume)
Yaani Mambo ambayo yanaupa uanaume HESHIMA na THAMANI...na Nikasema ni Uwezo wa Kubeba Majukumu, Uwezo wa Kusimamia na Kuongoza na Uwezo wa Kupeleka Moto
Hivyo, Ni Muhimu Kuwa na Fedha, ni Muhimu Kuwa na Uwezo wa Kumuongoza Mwanamke na Ni Muhimu Kuwa na Uwezo wa Kuipiga Fresh๐Ÿคญ
Its me, Isaack Nsumba
Na kama Unahitaji Kujifunza Zaidi Kupitia Mimi, Nashauri Ujiunge na Wengine Wengi Katika Channel Yangu ya TELEGRAM.
Unachotakiwa
Kufanya ni kudownload telegram katika simu yako kisha bonyeza link ifuatayo
t.me
t.me
baada ya hapo bonyeza neno โ€œSUBSCRIBE/JOINโ€ na Kama Tayari Umeshafanya Hivyo Basi HONGERA SANAA!
@isaack_nsumba

Loading suggestions...