bongotech2⁵5🎮🎧🛜
bongotech2⁵5🎮🎧🛜

@Bongotech255

11 Tweets 1 reads May 10, 2023
Safari ya password inafikia mwisho
Safari ya mwanzo na mwisho ya password kwenye simu zetu inawadia, hatimaye Google wameleta feature mpya ya kuweza kutoa / kuingia kwenye program au akaunti zetu za Google bila kutumia passwordi.
Uzi unaendelea chini kazi kwako 🙈
Kwa muda mrefu Google walikua wanatafuta njia rahisi Zaidi ya kutumia email akaunti zetu bila kuweka password au kufungua email zetu bila kuandika password.
Mara nyingi password zilikua zikitumika kwa muda mrefu lakini inaonekana sio salama maana watu wengi usahau password inawapa ugumu kuingia kwenye email zao pia ni njia rahisi ya kudukuliwa akaunti zao ikitokea mtu ambaye sio mzuri akijua password yako.
Ndipo Google wameamua kuleta mfumo mpya wq kuingia kwenye email yako bila kutumia password unatumia Passkey ?? Je Passkey ni kitu Gani ?
Ebu subiri kwani ukini follow utapoteza nini boss 🙄!! Follow basi @Bongotech255 tujifunze maujanja mengi Zaidi
Passkey ni njia mpya ambayo itakusaidia kuweza kuingia kwenye tovuti na app zako sio lazima uweke password sijui jina lako , mwaka wa kuzaliwa, au password123 nk.
Badala yake utatumia mfumo wa passkey kuweza kuingia kwenye mitandao ya kijamii au kwenye tovuti mbalimbali utatumia ku scan uso , kutumia fingerprint au skrini lock kuingia kwenye akaunti yako bila kutumia password.
Passkey wameweka ili kuwalinda watu dhidi ya uhalifu wa mitandaoni online ivyo inawafanya watu kuwa salama kuliko kutumia Ile njia ya kupokea ujumbe wa code kwa mfumo wa message.
Unaweza kuipata Sasa hii feature kwa kuingia kwenye hii tovuti kupitia Google akaunti yako 👇
g.co utafanya setting zake kwa urahisi sana.
Itachukua muda kidogo huu mfumo kuanza kutumika moja kwa moja ila kwa Sasa Iko kama option ya kuchagua muhusika utumie Nini passkey au password kwenye email yako
Pia unaweza kuingia kwenye Google akaunti yako >> kisha security>>passkey utaweza ku enable hii feature kwenye simu yako.

Loading suggestions...