Oscar Oscar
Oscar Oscar

@okaoscar25

11 Tweets 2 reads Jun 01, 2023
Je wajua..?
KUTANA NA MTU ALIYEKATAA KUFAA..😁
Violet Jessop alikua ni miongoni mwa watu waliohusika katika ajali tatu za meli ambazo mbili kati ya hizo zilihusisha meli kuzama na moja ikiharibu vibaya meli – lakini katika zote aliibuka akiwa hai licha ya maelfu kupoteza maisha.
Ajali tunazizungumzia hapa nia ajali ya meli ya The Olympic mwaka 1911, ajali kubwa ya Royal Mailship Titanic mwaka 1912 (Titanic) na ajali ya meli ya His Majesty Hospitalship Britanic mwaka 1916. Kupona kwenye ajali zote hizi kulimfanya apewe jina la Miss Unsinkable. Nifuate…
Wakati tumeziangalia historia za meli ya Titanic na The Olympic, nyuma ya meli hizi kuna habari nyingi sana zilizojificha. Moja wapo ni hii ya binti aloitwa Violeth Jessop, ambaye ni mzaliwa ma Argentina lakini alikulia Uingereza ambako ndiko maisha yake yote ya utaftaji hadi
mauti yalimkuta katika nchi hiyo.
Kama mtoto wa kike, Violeth hakua na ndoto ya kwamba siku moja afanye kazi za ubaharia lakini kutokana na ugumu wa maisha na sababu kama kukosekana kwa ajira alijikuta anafanya kazi ya u-nesi katika meli za kampuni ya White star line. Kampuni
hii maarufu imewahi miliki meli kubwa kama The Olympic, RMS Titanic, HMHS Britanic, RMS Majestic na nyingine nyingi.
Mwaka 1911 akiwa anafanya kazi katika meli ya The Olympic, wakiwa safarini ilitokea ajali ambapo meli ya The Olympic iligongana na meli ya RMS Hawke huku violeth
Jessop akiwa ni miongoni mwa watu waliokua ndani ya meli ya The Olympic. Katika ajali hii hakuna mtu aliefariki wala kujeruhiwa lakini meli hizi ziliharibiana vibaya katika baadhi ya maeneo.
Mwaka 1912 akiwa ndio kwanza ameajiriwa katika meli ilokua inafanya safari ambayo
ilikua ni ndoto ya kila mtu duniani - naizungumzia meli ya Titanic. Violeth alikua ni miongoni mwa manesi katika meli ya Titanic na pindi meli hiyo ilipogonga mwamba wa barafu na kuua watu Zaidi ya 1500, Jessop alikua ni miongoni mwa watu 500 ambao walifanikiwa kuokoka katika
ajali hiyo. Kama ilivyodhaniwa na wengi kuwa huenda alitakiwa kuacha kazi mara baada ya kusalimika katika ajali hizo, lakini hapana… HAKUACHA.
Mwaka 1915 wakati usajili na uajiri wa wafanyakazi waliotakiwa katika meli mpya ilokua inaelekea kufunguliwa ya HMHS Britanic, violet
alituma tena maombi na alichaguliwa kwa mara nyingine kama nesi katika meli mpya ya britanic. Miezi michache baadae meli mpya, kubwa na nzuri ya Britanic iligonga bomu la kupandikizwa majini na kusababisha ajali ilopeleka vifo vya watu wengi lakini cha kushangaza Jessop alikua
miongoni mwa atu waliosalimika licha ya kuumia vibaya siku ile.
Tunaweza kusema labda alikua na bahati tu…ila nkufahamishe tu, akiwa kasichana kadogo - Violeth aliwahi kuugua ugonjwa wa TB, ugonjwa ambao kwa wakati huo haukua na tiba lakini cha kushangaza violet aliamka tena
na akaingia mtaani. Yote tisa, kumi - siku zake zilifika akiwa kikongwe wa Umri wa miaka 83. Julieth alifariki kutokana na ugonjwa wa moyo

Loading suggestions...