Babuu | Hisa
Babuu | Hisa

@BroBabuu

4 Tweets 6 reads May 07, 2024
1/4
Dividend Yield ni nini?
Ni uwiano wa kifedha unaowaonesha wawekezaji ni kias gani kampuni inalipa kama gawio kila mwaka ikilinganishwa na bei ya hisa zake
Hesabu hufanywa kwa kugawanya gawio la kila hisa kwa mwaka /bei ya hisa na kuonyesha matokeo kama asilimia
#BabuuHisa
2/4
Si lazima Dividend Yield yako ifanane na ya mwingine.. Hii husababishwa na bei ya mwanahisa aliyonunulia hisa zake
Aliyenunua hisa wakati bei zipo chini miaka ya nyuma leo yield yake itakua kubwa tofauti na anayenunua leo
Tazama mfano unaofata kuelewa zaidi
#Babuuhisa
3/4
Aliyenunua CB ikiwa 100/hisa alitumia 1 Mil na kwa gawio la June mwaka huu atapata 500k sawa na yield 50%
Aliyenunua CB ikiwa 560/hisa anatumia 5.6 Mil na kwa gawio la June mwaka huu atapata 500k sawa na yield 9%
Wa awali alitumia 1 Mil kuwekeza na leo inamuingizia 50%
4/4
Ila aliyewekeza leo amelazimika kutumia 5.6 Mil ili kuweza kupata 500k sawa na 9% ya uwekezaji wake.
Hii ndo sababu nashauri kabla hujawekeza hakikisha unawekeza ukiwa na malengo ya muda mrefu na sio kutafuta faida kubwa kwa miezi miwili au mitatu ukaishia kupoteza

Loading suggestions...