Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

25 Tweets Dec 08, 2022
#PichaLinaendelea anzia post iliyopita..
CHIMBUKO LA UADUI NA UHASAMA IRAN,SAUDIA NA MAREKANI.
hawakufurahishwaga na uvamizi wa marekani IRAQ kwasabab ulikua unawaweka wote HATARINI especially ujio wa ISIS. Saudia wengi ni wasunni wakati IRAN ni utawala wa SHIA.Lakini nchi
zote mbili hazina lile tatizo la Madhehebu kama lililopo Iraq
Yemen n.k Kwasabab waliowengi ndo wapo madarakani basi hakuna ugomvi,lakini wao kwa wao(Iran na saudia) hawaelewani lakini wote wana mkwanja mrefu unaotokana na utajiri wa 'kitu WESE'(mafuta)
Zamani
miaka ya 80 IRAN na SAUDIA zilikua tawala mbili za kifalme
walikuwa washkaji wanaopigiana simu mara kwa Mara na kuchat insta na whats app ,kutagiana picha za maslay Qeen !KuDAMSHI pamoja na zaidi ya yote walishare sponsor/Danga moja, MAREKANI.Hili danga ndo liliwahudumia wote
wawili na wakabadilishana kwa
mahaba ya mafuta.Ghafla Akaibuka mwanaume mmoja,kiongozi wa kidini aliyeheshimika sana IRAN wa
kuitwa Ruhollah Khomeini,nchi za magharibi zinamtambua kama Ayatollah Khomeini,akaona maisha ya kuchuna buzi sio,akapindua serikali ya #Shaa aliyekuwa
kibaraka wa USA akasimika rasmi DOLA ya kiislam IRAN (hiyo ilikuwa 1979) na kuwaambia wamarekani msituchagulie tuishije,piteni hivi Na
kwa media zenu 'POVU ALLOWED' sisi ndo sisi wengine mafisi.Mkitaka nendeni mkashtaki BASATA.
Baada ya tukio hilo FAMILIA ya kifalme ya Saudia
matumbo joto wakijua hizi harakati
zitahamia kwao na zitawang'oa na hapa ushkaji ukafa. So since hapo yamekuwa ni MASHINDANO ya kusambaza misimamo kati ya IRAN(washia)ambao hawataki
kuskia #UTAMADUNI wa marekani ambao huku bongo umetuzalishia
kina #Countrywize
(a.ka. GADAFI FEKI) wakituambia "BABY TURN UP!" na mambo ya
koneksheni na badala yake WANATAKA misingi ya dini ifuatwe
Upande wa #Saudia wanaona KUTURN UP kidogo si mbaya jmn
lakini msingi ya Uislam ifuatwe.Ndo maana kuna wasanii wa marekani wanaendaga kufanya show Saudia
lakini IRAN weeeee USITHUBUTU KUKUTWA. So kama nilivyokueleza wote wanakubaliana ni waislam lkn Saudia kuna watoto wa kifalme ambao maisha yao tu binafsi ni 'KIPENGELE' yana mazingira flani ya KUDAMSHI too much na wanajua bila mkono wa MAREKANI tunapitishwa hivi vere soon!
Na wameshakoswakoswa mara kibao. So hapa ndipo mbio zinapo anzia za kusambaza msimamo wa kila upande kwa nchi jirani.Kikinuka IRAQ basi Saudia wanatuma silaha na Msaada mwingine kwa wapiganaji wa kiSUNNI na IRAN anaisaidia upande wa SHIA. so ndo maana mwanzoni tukakwambia
vita
zote zinazoendelea LIBYA, IRAQ,
SYRIA,YEMEN Na hata nchi za Africa kaskazini(uarabuni) zinafadhiliwa na hawa mabwana kwa mtindo huu.Nadhani umepata
picha ya kinachoendea kati ya hawa mabwana wawili.Mfano mzuri nikupe senario ya kinachoendelea YEMEN sasa hivi.
YEMEN imetoka kuwa nchi ya kuvutia na kihistoria na sasa ni moja ya nchi maskini zaidi mashariki ya kati!Hii ndio nchi ya asili ya OSAMA BIN LADEN.Baba yake OSAMA alikuwa mfanyabiashara kutoka hapa Yemen aliyeenda kuhustle SAUDIA akiwa na kipaji cha Stive #Nyerere
akajipenyeza hadi kwa wakuu familia ya kifalme,na kwasababu uchawa aliuweza akala mashavu ya tenda za ujenzi na ndipo Osama akazaliwa na kukulia Saudia.Ndo maana alivyoleta ujuaji waka mwambia "Kwanza hatukutambui Shensi sana!"akakimbilia SUDAN!
Kama nilivyokwambia episode za
kwamba story za PICHALINAANZA zinaungana so tutakuletea upande wa OSAMA BIN LADEN na alifikaje alipofika kwasababu ni story inayo jitegemea baada ya hii. so Nini kimetokea YEMEN?Kuna jamaa anaitwa ALI ABDULLAH SALEH
ndiye alikua Rais wa YEMEN mpk 2011 km unafuatilia utakumbuka
utakumbuka yale maandamano ya nchi za uarabuni yaliyoitwa ARABSPRING,(kimbunga cha uarabuni) ndiyo yalimng'oa huyu jamaa cz alikuwa mmoja wa viongozi waliochokwa!Alikaa miaka 20 madarakani tangu 1990.kifupi
aliingia madaraka wakati maslayQueen wengi wanao tusumbua insta
hawajazaliwa!Ukiachana na FIDQ aliyesema "USUPASTAA MZIGO WA MIBA" Huyu jamaa SALEH aliwahi kusema "Kuiongoza Yemen ni sawa na kudance juu ya vichwa vya
nyoka!" nadhani kwa punchline hii FIDQ kafunikwa!So baada ya kumng'oa Saleh kwa maandamano ,WaYemen wakahisi sasa 👇
"MAMBO YAMESHAKUWA MAKUBWA na YAJAYO YANAFURAHISHA!lakini mpaka tunavyopeana madini hapa, kati ya watu Milioni 26 waliopo Yemen
milion 24 wanahitaji msaada wa kibinadamu.yaani HALI ni mbaya!hali ni tete.Utauliza WHATS GOING On?au what happened? jibu ni tunarejea Mchezo uleule
niliokueleza wa IRAN na SAUDIA. how?Kuna kitu kwa kifupi kinaitwa GCC yaani GULF COOPERATION COUNTRIES. Hizi ni nchi zinazound umoja flani wa kushughulikia matatizo yao MASHARIKI ya kati kama unavyoona huku kwetu SADC ,jumuiya ya africa mashariki n.k .Na Hawa ndio walifanya
mazungumzo kutuliza 'mori' wa maraia waliokuwa na mizuka kumng'oa Saleh (aliyekua rais wa Yemen) na GCC wakamwambia "mzee baba SALEH usitujazie nzi!,jumba bovu lishakuzidi hili kubali yaishe,Pita hivi Amani irejee!".NDUGU SALEH akaamua kuwa 20percent akajiweka pembeni kuepusha
Alipoondoka wakamuweka aliyekuwa makamu wake Abdu Rabu Mansour Hadi, akawa Rais.Hilo jina lake Mansour linafanana kama MANSULII so acha tumuiche bwana MANSULII.Ndani ya kipindi kifupi tu ,wayemen waligundua kumbe waliruka mkojo na kukanyaga
maNIAJE NIAJE, Kwasabab Yemen
Yemen iliendelea kusuffer zaidi na mwisho wakajua wale #GCC walituyeyusha tu,na ndipo kikaibuka kikundi cha wapiganaji kaskazini mwa Yemen kinajiita HOUTHI(WAHUTHI) wakaanza kukinukisha DHIDI YA serikali ya bwana mansulii.HASHTAG MANSULII ASHUKE JUKWAANI. SO wakamtaka
wakamtaka bwana MANSULII- kina kirefu atupishe!ameshindwa kazi
Na ndicho chanzo cha MABOMU ya Saudia Arabia yanayo dondoshwa YEMEN hadi leo na kuua mamia kwa maelf ya raia. Nini kilitokea? Hawa wahouthi ni jamii ya waislam wa SHIA(Kama WA IRAN) ambao
walishikiri sana...🥴👇
kukinukisha wakati wa maandamano(2011) ya kumng'oa SALEH,so wakati GCC wana wakutanisha waandamanaji na serikali ya SALEH,walikubaliana kuunda serikali ya pmj,so Saleh akaondolewa lkn watu wake walibaki Serikalini na jeshin na wahouthi pia wakapewa mashavu kadhaa Serikalini.
Kwahiyo baada ya serikali kuundwa na RAIS mpya SINZA star wao Mansulii akaendeleza undava wake,wale wafuasi wa Saleh waliobaki jeshini,wakaungana na wale waHOUTHI(kifupi maadui wa zamani waliungana)wakachukua silaha wakaingia town na kuuteka mji Mkuu wa Yemen, SANAA
hii Ilikuwa 2014.Sasa mji Mkuu ushatekwa wewe ungekuwa bwana# MANsulii ungesubiri nini? CHAP kwa harak UndergroundKing
MANSULII, akakwea pipa hadi SAUDIA ARABIA.kwanini alikimbilia Saudia?Kwasabab ule umoja wa nchi za GCC niliokuelezea kiongozi wao ni SAUDI ARABIA.
So ukawa ni mzigo/jukumu la saudia na washirika wake wa GCC kuhakikisha bwana MANSULII anarudi madarakani hata kwa mbinde!Lakini hapa IRAN ilishaanza kutajwa!I told you hawa wahouthi ni WASHIA.....
#PichaLinaendelea post ijayo tunamalizia kabisa.

Loading suggestions...