Martin Maranja Masese
Martin Maranja Masese

@IAMartin_

6 Tweets 4 reads Apr 01, 2022
Carol Ndosi kaenda Clubhouse, kapigwa mawe, akaanzisha tena room na wenzake kuanza kujadili tweet yangu niliyosema tupate katiba mpya ili mtu kama Bashite asije kuzuia biashara yake ya Nyama Choma. Carol anasema nilikuwa wapi wakati anafilisika hadi kupeleka watoto kwa bibi yao?
Carol, anasema anashambuliwa kwa sababu ana influence kubwa na watu wengi nyuma yake na kwanini haimbi wimbo wetu.
Carol, nani amewahi kukuomba ujiunge na harakati zao? Wao wanakushambulia ukianza kushambulia hashtag zao tu, usijipe umuhimu usiokuwa nao.
Acha kutafuta huruma!
Ndiyo, tunajua, Ulikuwa mwanachama wa ACT, ukaondoka huko, sasa hilo la kutokuwa na chama siyo sababu ya watu wasikupige spana wakiona inafaa haswaa ukianza kuzuia harakati za wao kudai katiba mpya. Tunajua, ume' mute hashtag zote za katiba mpya, ume' block wengi na hatujali.
Unasema tulikuwa wapi wakati unafilisika hadi kushindwa kupata chakula cha watoto wako? Kwamba tulikuwa wapi wakati timu yako inakosa chakula, Nani alikufilisi? Serikali ya CCM ambayo sasa inazuia mchakato wa Katiba Mpya sawa na wewe unavyozuia na kuzipinga hashtag za katiba Mpya
Aliyezuia tamasha lako la Nyama Choma lisifanyike ni mkuu wa mkoa wa DSM, Makonda. Hizo lawama za kukufilisi unatakiwa kumpa yeye, siyo sisi. Ndiyo maana tunapigania katiba mpya ili asijitokeze Bashite mwingine na kukufilisi tena ukapata 'depression'.
Carol Ndosi, hakuna aliyekutuma kwenda huko Clubhouse ukapigwa spana, hadi ukafungua room nyingine ili kushusha hasira. Hasira zako hazina msingi. Tuungane kama wananchi tufanye mambo mawili (ili wanao wasishinde njaa tena kama ulivyosema), tuitafute katiba mpya kwa nguvu ya umma

Loading suggestions...