Martin Maranja Masese
Martin Maranja Masese

@IAMartin_

13 Tweets 15 reads Apr 30, 2022
Ni ushauri, unaweza usiuchukue pia. Lakini ni ushauri muhimu kwa wanasiasa wa upinzani.
Ukiwa mwanasiasa wa upinzani ambaye watu wanakutazama kama alama ya upinzani, jitahidi kuwa wa mwisho sana kumwaga sifa/pongezi kwa washindani wako kisiasa. Nitawaeleza kwanini kwa mifano. 👇
Unaweza kuwa na mtazamo wako binafsi kuhusu mambo kadhaa yanayofanywa na serikali, lakini zingatia, wewe ni mwanasiasa wa upinzani ambaye lengo la kwanza la chama cha upinzani ni kuongoza dola kwa kuwaeleza wapiga kura udhaifu wa serikali ili wachague chama chako 👇
Ukiwa kiongozi ndani ya chama cha siasa, wafuasi wako wanakuamini na kukufuata na wapo tayari kukutetea. Umefungamanisha fikra zako na wao. Hivyo tambua, kuna mstari mwembamba sana unaoweza kutenganisha mawazo yako binafsi na msimamo wa wafuasi wako kisiasa katika Jambo fulani 👇
Ukiwa kiongozi wa taasisi ya kisiasa kuna uhuru wako fulani unalazimika kuupoteza, ikiwa ni pamoja na Uhuru wako binafsi wa maoni. Hii ni kulinda hadhi ya taasisi yako unayoongoza na hadhi yako mwenyewe pia, kulinda maoni yako binafsi yasiumize mtazamo wa kitaasisi unayohudumu 👇
Pia, kiongozi wa chama cha upinzani, hupaswi kuwa mtu wa kwanza kumwaga pongezi hadharani kwa watawala hata kama kuna masuala kadhaa wanakufurahisha na unaridhiana nao. Unaweza kutafuta njia ya kukubaliana nao kwa kutokubaliana nao. Hii inaweza kukuweka salama zaidi. 👇
Watawala wapo madarakani kwa sababu wewe haupo madarakani. Ukianza kuwapongeza hadharani, utakwenda tena kuwaeleza nini wapiga kura wasimchague mtawala wakati ulisema eneo hilo amefanya vizuri? Huwezi kuwa mbadala wake tena kwa sababu wapiga kura watamchagua aendeleze mazuri 👇
Mfano, unaunga mkono jamii ya Maasai wa Ngorongoro kuhamishwa kutoka ndani ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (ambao ni msimamo wa serikali), unadhani utakwenda kwa hawa watu uwaombe kura na wakupe? Watakuwa radhi wamchague shetani kamili (mtawala) kuliko wewe. Ndiyo. 👇
Kumwaga pongezi nyingi kwa mpinzani wako ni kumuongezea nguvu, na kumpa silaha ambayo ataitumia kukumaliza nayo. Tazama, watawala wa Tanzania, CCM, ikitokea mpinzani wao (CHADEMA) amemwaga pongezi, watatenheneza hadi vipeperushi kwa pongezi hizo. Hiyo ni silaha umewapa. 👇
Pongezi ni silaha dhidi yako. Zitatumika kukuchapa sana na kukichapa chama chako. Na utashindwa kumkosoa mshindani wako kwa sababu tayari ulimwaga sifa nyingi kwake. Pongezi zako watazifanya rejea ukianza kuwakosoa au kuwapinga na wafuasi wako watakuachia hiyo vita mwenyewe 👇
Mnakumbuka sifa wapinzani wa CCM walizokuwa wakimwaga kwa John Pombe Joseph Magufuli akiwa waziri wizara mbalimbali? Baadae Magufuli akawa mgombea wa CCM (na wakati mgombea wa upinzani ni Edward Lowassa) aliyeitwa fisadi hadharani na alijiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND 👇
Nini kilitokea? Wapinzani wa CCM (UKAWA) walikuwa na kazi mbili. Moja, kuhakikisha wanapangua sifa zao kwa Magufuli kwamba ni kiongozi makini na mchapakazi. Pili, kumsafisha Lowassa ambaye alikuwa anaitwa 'fisadi'. Video za sifa kwa Magufuli kutoka kwa wapinzani zilisambazwa 👇
Nataka kusema nini? Kiongozi wa upinzani ambaye unaamini chama unachoongoza lengo lake ni kuingoza dola, ni muhimu sana kuwa mtulivu katika Jambo linalofanywa na dola. Unaweza kukubaliana nao kimoyomoyo au kukubali-kutokubaliana au kutokubaliana nai kabisa. Hii ni muhimu. 👇
Lakini kama unaamini unaweza kuwa sehemu ya watawala siku za mbeleni, ni haki yako kumwaga pongezi, maana ni wenzako rohoni ingawa kimwili bado unajionyesha upo upinzani. Ni ushauri tu, ambao siyo lazima uwe na mantiki kubwa, lakini lakini TUISHI nao, utatusaidia.
#MMM, MTIKILA!

Loading suggestions...