Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

18 Tweets 1 reads Dec 08, 2022
Wakati vita inaendelea UKRAINE na RUSSIA unasikia mengi ,lakini acha tukuletee story ya picha hii unayoona ikupe feeling ya vita ni kitu gani.
Kushoto na kulia ni mtu mmoja, kushoto wanasema he is looking at you na kulia he is loking thru you. #PichaLinaendelea
Hii hali wanaita TWO THAUSAND YARD STARE .Nitakuelezea vizuri.
Hii ni story fupi inayokupa picha kamili ya kile vita inaweza kumfanya mtu.Inampata yeyote anayeexperience hili.Dogo pichani ni hali Syria 2013 🇸🇾 akiwa na miaka 7 tu ana 2000yard stare!
Imagine dogo Ahmed yupoje leo au atakuwepo duniani?Maana hizi picha ilikuwa 2013.Kama yupo hai atakuwa na miaka 17,unahisi ni mtu wa aina gani?sote ni matokeo ya mazingira tuliyozaliwa,je?alichagua? #PRAYforPeace .
Jamaa anaitwa Evgeny Stepanovich na maisha yake yalichange ghafla wakati USSR inavamiwa na UJERUMANI.Yaani wakati Russia ya leo inaivamia UKRAINE iliyopo ulaya,Enzi hizi UJERUMANI ndo alikua mbabe wao.Kila mbabe na zama zake.
Jamaa alikua ticha miaka hiyo lakini ndoto zake awe mchoraji mkali na akiwa chini ya miaka 30 alishaenda zake chuo UKRAINE wakati huo ikiwa nchi moja ya USSR yaani UMOJA WA SOVIET na akapiga zake chuo akamaliza.Akiwa anasubiri kula shavu aanze kazi ya ndoto yake,ndipo KIKAUMANA
Imagine mwamba aligraduate chuo mjini KIEV UKRAINE mwaka 1941 ,Mwezi wa 6 mwaka huo huo ndoto yake ikakatishwa ghafla, 22june1941 serikali HITKER ikaamua kuivamia USSR na hii ndo vita ya 2 ya dunia.So ndoto za vijana wengi ziliishia kama hivi.#PICHALINAENDELEA.
Evgeny kutoka chuo direct aliingizwa jeshini kupigania nchi kama ambavyo umesikia rais wa UKRAINE akiambia vijana washike silaha kupigania nchi,Leo adui ni Russia lakini enzi hizo adui alikua Ujerumani.Akawa mstari wa mbele jeshini kulinda miji iliyokuwa kati ya UKRAINE.
Alikua kijana wa miaka 30 wakati vita inaanza na alishuhudia miaka 4 ya mateso na mambo mazito ya vita.
Vita ilianza mwezi june na miezi michache tu mbele September Kwenye Bato moja la kuulinda mji mmoja karibu na KIEV Ukraine,alijeruhiwa mguu wahuni wakamkuta..!🥵
so akakamatwa na askari wa HITLER akawa mateka wa VITA na hapa ndipo alipojua hajui.Hiyo kambi ya mateso aliyopelekwa iliitwa KHOROL .Ni kama ile movie ESCAPING FROM SOBIBO.
Ni kati ya kambi za mateka wa kivita za Ujerumani ya HITLER ambayo ukiingia huko,wachache sana walitoboa.
Wengi walifia humo.Zaidi ya watu 90,000 walifariki na hakuna kuoga wala kuzika wanaofariki.Ilikua ni mtu kula mtu ili apone.
Alikaa kwenye mateso haya hadi miaka 2 baadaye 1943 akafanikiwa kutoroka kwenye kambi ya Mateso,ESCAPING FROM KHOROL.
Alipotoroka alikuta vita bado inaendelea so akaelekea kujiunga na JESHI tena akapelekwa kwenye operesheni nyingine za kijeshi POLAND,MOLDOVA ,UKRAINE NA UJERUMANI ambayo yalikua sehemu ya USSR wakati huo.
Vita ya pili ya dunia ilimalizika 1945 na HITLER alisha sarenda na mwanetu Evgeny unayemuona hapa alikua bado hai na akatunukiwa tuzo ya bato kadhaa alizopigana.Tho hakupewa tuzo ya ushindi dhidi ya Germany sabab muda wote wa mapigano alikua mateka wa vita..#PICHALINAENDELEA
Hiki unachokiona kwenye sura yake kinafahamika kwa SLANG maarufu kama 2000 YARD STARE yaani kiswahili tunasema JICHO au MSHANGAO hatua 2000.Kifupi ni mtu anatisha hata kwa mbali na hii hali huwapata wanajeshi wengi waliopigana vita front line.
Ukifuatilia vita vyingi 2000 YARD STARE ni term maarufu sana.
Kitaalam ni PTSD yaani Post Traumatic Stress Dissorder .Ni shida ya kisaikolojia inayompata binadamu kwa kuona vitu vilivyo nje ya kawaida yake.Matukio yale hushindwa kuondoka na furaha hutoweka kwenye maisha.
Mwanajeshi mmoja wa Marekani RICK CLEVENGER alikua anaelezea kilichomtokea mara ya kwanza alipopelekwa kwenye vita ya Vietnam.Wakati anafika airport alikua wanabadilishana SHIFT na wanajeshi wengine ambao walikua wameshapigana VITA ile mwaka 1. (mwisho litakupa link ya video hii)
So walikua airport kusubiri ndege Inayowashusha kina Rick.Palepale HOFU ilimjaa aliposhuhudia kwa macho yake UHALISIA wa kile alichosikia 2000 YARD STARE yaani nyuso za wanajeshi wale wenzake,Zilikua zinatisha na bila kukuambia chochote sura zao zilisema kila kitu..
Zilibadilika na kumtisha hata RICK na alijua yeye ndiye THE NEXT miezi michache ijayo.Imagine ni hali inayomtisha hadi mwanajeshi mwingine.Mtu mwenye shida hii hawezi kufurahishwa hata na vitu ambavyo vilimchekesha au kumfurahisha mwanzo.Yaani unachange hata starehe yako.
Hii ni taswira ya nyuma iliyo NDANI ya vita.Atleast inaweza kutuonyesha thamani ya AMANI si ndio? Vita isikie. Kusikia ushuhuda huu msikie hapa
youtu.be
Story hii on youtube
youtu.be
Mwisho: #TaarifaNaMaarifa

Loading suggestions...