Inapofika Mwisho wa wiki huwa nakaa na Mke wangu baada ya mlo wa jioni, tukiwa na utulivu wa hali ya juu kabisa huku redio ikiwa inaimba kwa sauti ya chini ile Kwaya ya Mt. Theresia Matogoro- I love you.
Huku nikiwa nimempa nafasi ya kulala karibu na unapodundia moyo wangu..👇
Huku nikiwa nimempa nafasi ya kulala karibu na unapodundia moyo wangu..👇
Naanza kumwambia, Mke wangu Pole na majukumu ya wiki nzima na namshukuru sana Mungu kwa ulinzi wake hata sasa tena tupo tumekaa tukiwa na amani na furaha. Wiki imekuwa na mambo mengi ya hapa na pale lakini katika nyakati zote huenda kuna wakati nawe kama Mwanadamu...👇
Nimekukwaza au kukushtua kwa matendo yangu. Naomba nitumie nafasi hii kukuuliza kama jambo la namna hiyo lipo ili niweze kulitambua, nilikiri kisha nikuomba radhi ili kuoweka nafsi yangu na yako huru na mwisho tuzidi kuijenga familia yetu katika misingi ya Kumpendeza Mungu...👇
Basi baada ya hapo atachukua muda kidogo atawaza na kisha ataeleza ikiwa lipo jambo hilo au halipo. Kama lipo basi natumia njia iliyo sahihi kujielezea na kisha kuomba msamaha na akiridhia ananisamehe bila masharti au kama kuna masharti nayatimiza nasamehewa. Baada ya hapo...👇
Nae ananiuliza hvyo hvyo kisha natafakari na namwambia kama lipo au halipo kisha nae anajielezea anaomba msamaha namsamehe maisha yanasonga.
😂 Mfano hapo hivi mahuzi nilishtakiwa kwa kosa kuwa nilirudi nyumbani usiku nikaingia bafuni nikafungulia maji chwaaaaaa..👇
😂 Mfano hapo hivi mahuzi nilishtakiwa kwa kosa kuwa nilirudi nyumbani usiku nikaingia bafuni nikafungulia maji chwaaaaaa..👇
Halafu nikapiga mswaki nikatoka bila kuoga, so nikaambiwa kwanini sikuoga? 😂 Basi nikaambiwa nitoe faini ya Sh. 1000 chap kwa haraka nisamehewe, Nikatoa nikasamehewa na maisha yakasonga...
😂😂🙌 Na huo ndio muktasari wa life langu weekend kwa ufupi. 🥂✊🏿
😂😂🙌 Na huo ndio muktasari wa life langu weekend kwa ufupi. 🥂✊🏿
Loading suggestions...