Martin Maranja Masese
Martin Maranja Masese

@IAMartin_

71 Tweets 58 reads May 19, 2022
Tupige kidogo ‘mastori’ ya Mchungaji Christopher Mtikila
Kesi ya kutoa maneno ya uchochezi ambayo ilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mtikila Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam. Katika Kesi hiyo upande wa jamhuri Ulidai Mtikila alienda kosa Hilo kufuati
Kauli aliyoitoa hadharani siku chache baada ya Muasisi wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere kufariki Oktoba 14, 1999 ambapo Mtikila alitamka maneno yafutatayo:
“Marehemu Rais Julius Nyerere alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, ni mzoga, nyamafu na ameenda jehanamu” alisema Mtikila.
Mtikila amekuwa akisema maneno hayo siku zote za Maisha yake na mwisho wa siku Kesi hiyo ilifutwa.
Kesi nyingine ya kutoa maneno ya uchochezi alivyoshitakiwa nayo Mtikila Enzi za Uhai wake ni Jamhuri dhidi ya Christopher Mtikila .
Mtikila alishtakiwa kwa Kesi nyingine ya uchochezi   ambapo ilidaiwa na upande wa jamhuri kuwa Mtikila wakati akihutubia mkutano Katika Viwanja vya Jangwani Dar Es Salaam, Alisema maneno yafuatayo ambayo yalichapishwa Katika Gazeti la Mtanzania
na miongoni wa mashahidi wa upande wa jamhuri alikuwa ni Mhariri wa Gazeti Hilo Badra Masoud ambaye baadae aliajiriwa serikalini kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Cha Wizara ya Nishati na Madini na Askari Polisi pia.
Maneno hayo yaliyotolewa na Mtikila ambayo upande wa jamhuri ulidai ni ya kichochezi ni yafuatayo; 
“Rais Mkapa siyo Raia wa Tanzania ni Raia wa Msumbiji”.
Kesi hiyo iliunguruma na mwisho wa siku Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuta Kesi hiyo dhidi ya Mtikila kwasababu ilichukua muda mrefu kumalizika na mashahidi upande jamhuri ukawa hauleti mashahidi.
Mtikila Katika Kesi hii wakati ikisikilizwa, mapolisi walipokuwa wakifika kutoa ushahidi, Mtikila alikuwa Mara kwa Mara akiomba Mahakama isipokee ushahidi wa mapolisi wale kwa sababu wao sio Rais Benjamin William Mkapa.
Yeye (Mtikila) Kama mshtakiwa aliomba Mahakama itoe hati ya kumlazimisha Rais Benjamin William Mkapa afike Mahakamani atoe ushahidi wake wa kupinga kwamba yeye siyo Raia wa Msumbiji.
“Mweshimiwa Hakimu, huyu Rais Mkapa anaishi hapo nyumbani kwake SVU-Upanga, ni karibu kabisa na hapa Mahakama ya Kisutu. Kwanini asipelekewe Samansi afike hapa mahakamani maana ni karibu na anaweza kutembea hata kwa miguu aje akatae kuwa yeye siyo Raia wa Msumbuji”
“Mimi ninao ushahidi Rais Mkapa ni Raia wa Msumbiji Ndio maana Hana uchungu na taifa hili anauza Viwanda vyetu kwa Wazungu hovyo hovyo tu”
Alisisitiza Mtikila
Wakati Mtikila akitoa Maombi hayo akiwa amesimama kizimbani tena Mkapa akiwa bado ni Rais wa nchi wakati huo, waandishi waliokuwa wameketi mahakamani wanafuatilia Kesi hiyo walikuwa waainama huku wakicheka bila kutoa sauti.
Kesi nyingine ya uchochezi Na. 132/2011. Jamhuri dhidi ya Mtikila ambapo Mtikila alikuwa akidaiwa Kutoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuita ‘gaidi’ kwa madai kuwa serikali anayoiongoza inataka kuanzisha Mahakama ya Kadhi,
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 2009 na Aprili 17, 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshitakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema “Kikwete kuuangamiza ukristo”, “wakristo waungane kuweka mtu Ikulu” alinukuliwa Mtikila.
Katika shtaka la pili, Aprili 16, mwaka 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka wenye uchochezi kwa jamii. Na katika kesi hii Mtikila hana wakili wa kumtetea na anajitetea mwenyewe.
Siku Polisi wamevamia nyumbani kwa Mtikila alfajiri kufanya upekuzi kwa Lengo la kusaka Waraka huo na kumkamata, mke wa Mtikila, Georgia alipiga simu saa 12 asubuhi kwa waandishi wa habari kuwapa taarifa Kuwa (Mtikila) amekamatwa na Polisi hivyo waandike Habari na kuharifu umma
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa na Mahakimu watatu tofauti ambao ni Waliarwande Lema, Sundi Fimbo ambao Walilazimika wajitoe Katika Kesi hiyo kwa sababu Mtikila aliwaomba mahakimu wawili wajitoe kwa sababu anaamini hawana hadhi na hawawezi kumtendea Haki na mwisho wa siku Kesi hiyo
akapangiwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo kwa wakati huo Elvin Mugeta ambaye aliisikiliza Kesi hiyo na Septemba 25 Mwaka 2012, alitoa hukumu ya kumuachilia huru Mtikila baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha kesi yao.
Siku Mtikila alipotoa utetezi wake Katika Kesi hii Nilikuwepo, Mtikila Kama kawaida alikanusha Madai ya upande wa jamhuri kuwa ule Waraka wake uliokuwa na kichwa cha Habari kisemacho (KIKWETE KUANGAMIZA UKRISTO) Kuwa ni wa uchochezi, na alikubali Kuwa ule
Waraka ni wake na aliundaa yeye na siyo wa uchochezi na kwamba hawezi Kuukana Waraka ule kwa sababu Kuukana Waraka ule ni sawa na kumkana YESU KRISTO.
Mwenyewe Mtikila alijipambanua wazi kupambana na serikali ya Jakaya Kikwete na hakuogopa kumtaja hadharani
Mashambulizi yake aliyaita mabomu ya Eroshima dhidi ya serikali ya ‘Msanii’ Rais Jakaya Kikwete. Mtikila kabla na baada ya Kikwete awe Rais, ukikutana naye amekuwa akimuita Kikwete ni ‘RAIS MSANII’, Reginald Mengi, Rostam Aziz na wengine aliwajuisha katika kundi hilo.
Badaa ya hukumu kutolewa Mtikila akiwa kizimbani alipaza sauti “Hallelujah”. 
Wafuasi wake walishangilia na baadhi ya Polisi wenye vyeo Vya chini walijipanga nje Wakataka kumuweka chini ya Ulinzi Mtikila aliwaeleza maneno yafuatayo yalisababisha jaribio lile la Polisi kufutika
“Nyie Polisi hamna uwezo wa kunikamata mnavyo vyeo Vya chini sana.... Kama mnataka kanifungulia kesi nyingine nitakwenda Mwenyewe Kituo cha Polisi kuripoti. Hata boss wenu IGP-Said Mwema ananiita kwa heshima kwa kunipigia simu naenda Mwenyewe Polisi, hebu toeni ujinga wenu hapa”
Alisema Mtikila na kusababisha watu kuangua vicheko na Polisi wale waliokuwa wamepanga kumkamata kumuacha Mtikila aende zake nyumbani akapumzike huku wafuasi wake wakiimba na kuchaguza kwa maneno “saa ya ukombozi ni sasa”
Itakumbukwa Kesi hiyo ya kumtolea kashfa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwanzo alipangiwa Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, ambapo Januari 11, 2010 alitoa amri ya kumfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.
Amri hiyo ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Mkazi Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa ambaye alifika katika viwanja vya mahakama hiyo saa tano asubuhi akiwa amechelewa na ghafla alijikuta akikamatwa na askari polisi wa mahakamani hapo.
Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa.
Kabla ya Mtikila kukamatwa, alieleza mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya kobra wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka jana.
Alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.
Hata hivyo hakimu Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25, 2010 kesi yake itakapotajwa tena
Hii ni mara ya pili kwa Mchungaji Mtikila kushindwa kufika mahakamani wala wadhamini wake. Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 22 Mwaka 2009
Mchungaji Mtikila alikuwa akikabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi Na.132/2011
Ilipofika saa saa tano mchana, Mtikila aliwasili mahakamani hapo anashuka Kwenye Bajaji, marafiki zake waandishi wa habari wakamuwahi kule kule Kwenye bajaji na wakampa taarifa Kuwa
Hakimu Lema ametoa Hati ya yeye Kukamatwa hivyo mapolisi Wakimuona watamkamata.
Hata hivyo utetezi wake huo haukumsaidia Mtikila ,Hakimu Lema aliamuru aepelekwe mahabusu.
Mtikila alienda mahabusu na alipotoka Kesho yake alinipiga simu kuwajulisha watu wake Kuwa anakusudia Kuwasilisha ombi la Kumkataa Hakimu Lema ajitoe Kwenye Kesi yake kwa sababu Hana utu na mwisho wa siku kweli Hakimu Lema alijitoa .
Pia Kesi hiyo ilipohamishiwa kwa Hakimu Sundi Fimbo pia, Mtikila kupitia barua yake aliyoiwasilisha mahakamani hapo alimuomba hakimu Fimbo ajitoe kwenye kesi yake kwa sababu amebaini hawezi kumtendea haki kwasababu wakati kesi hiyo ikiendelea Mtikila ambaye ni mshtakiwa
katika kesi hiyo aliwasilisha ombi la kuomba usikilizwaji wa kesi hiyo usimame hadi kesi ya Kikatiba iliyopo mbele ya Jopo la Majaji wa tatu wa mahakama Kuu wanaongozwa na Jaji Fakhi Jundu na Profesa Ibrahim Juma ambapo katika kesi hiyo anaiomba
Mahakama hiyo izifute sheria za makosa ya uchochezi kwakuwa zinanyima haki wananachi ya kutoa maoni yao itakapotolewa uamuzi lakini huyo alilikataa ombi lake.
Mtikila alidai kuna kesi tatu za Kikatiba zilizokuwa zimefunguliwa mahakama kuu na washtakiwa wanaokabiliwa na
kesi za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambao ni Jayantkumar Patel ‘Jeetu Patel’, Profesa Costa Mahalu na mahakama ya Kisutu ilisitisha usikilizwaji wa kesi zinazowakabili hadio mahakama kuu ilipozitolea uamuzi kesi zao za Kikatiba.
“Na huyu Hakimu Fimbo anafahamu fika nimefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu kuzipinga sheria za uchochezi ambao sheria hizo ndizo zimetumika kunifungulia kesi ya uchochezi iliyopo mbele yake na anafahamu fika kesi ya aina hiyo ikishafunguliwa mahakama ya juu,m”
“mahakama ya chini inatakiwa isitishe usikilizaji wa yangu hadi mahakama hiyo ya juu itakapotoa uamuzi lakini yeye amekuwa akilikataa ombi langu na kwa kitendo chake hicho minasema amevunja mwenendo wa kesi na”
“ukiukwaji wa maadili ya sheria za nchi na haki na nimuomba ajitoe kwenye kesi yangu kwani tayari ameishaonyesha hawezi kunitendea haki ”alidai Mtikila.
Aidha Mtikila alidai sababu nyingine ya kumkataa hakimu Fimbo, ni kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa aliwai kuwasilisha ombi
kutaka afutiwe kesi hiyo ya uchochezi kwasababu kesi hiyo ilifunguliwa nje ya muda kwani kesi za uchochezi zinatakiwa zifunguliwe mahakamani ndani ya miezi sita tangu mshtakiwa alituhumiwa kutenda kosa hilo na kwamba kesi hiyo inafanana na kesi ya madai ya fidia Na.166/2004
Inayosikilizwa na Jaji Robert Makaramba, ambapo katika kesi hiyo anamdai Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa alikamatwa kinyume na sheria na kwamba kesi ile ambayo nayo ni ya uchochezi iliyokuwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilifunguliwa nje ya muda.
Na kweli Ilipofika Machi 22 Mwaka 2013 Hakimu Fimbo alitangaza Kujitoa kusikiliza Kesi hiyo ikapangwa kwa Hakimu Elvin Mugeta ambaye aliisikiliza Kesi hiyo hadi akatoa hukumu ya kumwachilia huru Mtikila.
Juni 2013, Mchungaji, Christopher Mtikila, aliibwaga  serikali katika kesi namba 009 & 011/2011, aliyokuwa ameifungua Katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCHPR) ya kutaka kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, nafasi mbalimbali ikiwamo urais.
Mtikila alifikia uamuzi wa Kufungua Kesi Katika Mahakama Kimataifa baada ya Juni 17 Mwaka 2010, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, kutoa hukumu ya rufaa ya Madai Na. 45/2009 ambayo ilifunguliwa mahakamani hapo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila.
Mrufani (Mwanasheria Mkuu wa serikali) ambaye alikuwa akitetewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye baadae alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju Katika rufaa hiyo alikuwa akiomba Mahakama hiyo ya juu kabisa nchini kutengua hukumu iliyotolewa na
Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam katika kesi ya madai Na.10/2005 
Mbele ya jopo la Majaji wa Tatu, Amir Manento (Mstaafu), Salum Massati (Jaji wa Mahakama ya Rufaa hivi sasa ) na Thomas Mihayo (Mstaafu) ambayo ilitangaza  Ibara ya 39, 67, 77 zinavunja Haki ya za watu
wasiokuwa wanachama wa vyama vyovyote  vya siasa kugombea urais na hivyo hukumu ile ikaruhusu mgombea binafsi.
Juni 17 Mwaka 2010 ndipo jopo la Majaji Saba wa Mahakama ya Rufani Tanzania lilokuwa likiongozwa na Jaji Mkuu wa Kipindi hicho ambaye kwa sasa amestaafu,
Augustino Ramadhani, Eusebio Mnuo (Mstaafu), Nataria Kimaro, Mbarouk Mbarouk, Sauda Mjasiri, January Msoffe, Bernad Luhanda walitoa hukumu ya rufaa hiyo ambapo walitangua hukumu ya Mahakama Kuu kwa maelezo Kuwa Mahakama haina mamlaka ya kutunga Sheria,
Mhimili wenye mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ni Bunge hivyo suala la kuwepo kwa mgombea binafsi litapelekwa bungeni kwasababu Mhimili wa Mahakama haina mamlaka ya kufanyia marekebisho Katiba ya nchi.
Ieleweke Kuwa Katiba ya Tanzania hadi sasa hairuhusu kuwepo kwa mgombea binafsi kwa sababu Ibara ya 39(1) (c) inasomeka hivi : “(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa”
siku hukumu ya rufaa mgombea binafsi Imetolewa ambapo ili mkataa mgombea binafsi, Mtikila alikasirika sana na alihojiwa na vyombo Vya Habari na alikuwa akisema Majaji wote Saba waliokataa kuhurusu mgombea binafsi   ni Yuda Eskalioti na vibaraka wa serikali yaani wasaliti wakubwa.
Aidha Kesi nyingi ya Mtikila ni ile Kesi ya Madai ya fidia ya Sh. Bilioni Moja ambayo anataka Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Katika Kesi hiyo Mtikila Anadai Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dk. Valentino Mokiwa alimdhalilisha kwa kumshika   makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka 2013.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila alisema kuwa alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholaus, usiku wa saa 03:00.
“Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti.”
Hayo ni maelezo ya Mtikila mwenyewe
“Baadaye Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.”
“Mokiwa alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo yangu kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya yangu” alidai Mchungaji Mtikila .
Mtikila aliomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa amlipe kiasi hicho cha fidia
kwa sababu mdaiwa alimdhalilisha na alimletea madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizo la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Mtikila alikuwa akiwaeleza wafuasi wake kuwa anashahuku kubwa siku ifike aanze kutoa utetezi wake katika kesi hiyo maana atavua nguo zote na sijui huyo wakili wa Mokiwa ambaye ni kijana wangu atakuwa tayari kunishuhudia mimi mzee wake nikivua nguo zote mahakamani kumuonyesha
hakimu makalio yangu maana akinishuhudia nipo uchi nikimuonyesha hakimu makalio yangu atakuwa amepata laana huyo wakili wa Askofu Mokiwa ambaye ni kijana wangu.
Basi wafuasi wake na waandishi wa habari wanafurahi kweli, wakisubiri kesi kuanza.
Mtikila Enzi za Uhai wake alikuwa anataka Shirika la uchunguzi la Scotland Yard Lije Tanzania, ichunguze kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba aliyefariki ghafla kwasababu Mtikila alikuwa akiamini Kolimba aliuwawa na CCM Hali  iliyosababisha kufunguliwa Kesi
Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam, ambapo Hakimu Gabriel Mirumbe (ni marehemu kwasasa ambapo alipofariki Mtikila alisema amefuraishwa na kifo hicho kwa sababu hakimu huyo alimfunga gerezani kwa kumuonea kifungo cha mwaka mmoja gereza la Keko.
Aidha vibekwa vingine Vya Mtikila ni Kwenye ombi la kuomba Mahakama ya Kisutu itoe amri ya kutolewa rumande (Habeas corpus) lilowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa kujitegemea Hurbet Nyange dhidi ya Jamhuri Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Nyange alikuwa akimtetea aliyekuwa mgombea urais nchini Burundi Katika awamu ya kwanza ambaye alikuwa ni Mtangazaji Katika Redio Moja huko Burundi, Sinduije.
Sinduije alikuwa ni rafiki wa Mtikila na aliposhindwa uchaguzi nchini Burundi alikimbilia Tanzania kujificha maana
serikali ya Burundi ilikuwa ikimsaka kwa kutenda makosa ya jinai wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Burundi na alipokamatwa Askari wa Interpol ili upande wa jamhuri uwasilishe ombi la Mahakama itoe Kibali cha kumrejesha nchini Kwao Sinduije ( Extradition request) .
Mtikila alikuwa akifika Katika Mahakama hiyo na kujaribu kukaa karibu na eneo la mahabusu ya Mahakama hiyo lakini Askari Magereza walikuwa wakimtimua wakimtaka akae Mbali na eneo Hilo Mtikila.
Waandishi wa Habari walikuwa wanaenda kuchekea Mbali ili Mtikila asiwaone maana angewaona wanacheka angewashughulikia kwa maneno makali. Mwisho wa siku Mahakama ilitoa Kibali cha Sinduije kurudishwa chini kwako
Mahakamani, Mtikila alikuwa anasema yeye anataka Sinduije abaki hapa nchini kwa sababu endapo atarudishwa Burundi, serikali ya Burundi itaenda Kumkata kichwa Sinduije.
Mtikila yeye alilipachika jina la “Mgodi” Kesi zote za Madai alipokuwa amezifungua. Alisema ameamua kuzipachika jina la mgodi kwa sababu anaamini atashinda na akishinda na Mahakama itaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya Fedha kwa hiyo Fedha ndiyo mgodi.

Loading suggestions...