Martin Maranja Masese
Martin Maranja Masese

@IAMartin_

9 Tweets 3 reads Jun 09, 2022
Wizara ya fedha ya @mwigulunchemba1 imeomba bajeti ya Sh14.94 trilioni. Shs9.09 trilioni zitalipa deni la serikali. Sh13.62 trilioni ni matumizi ya kawaida. Sh1.32 trilioni maendeleo. Deni la taifa limeongezeka kutoka Sh57 trilioni 2021 hadi kufikia Sh88.15 trilioni Machi 2022
Ripoti ya Benki Kuu (BoT) inaonyesha mpaka kufikia Oktoba 2021, deni la Serikali lilifikia Sh 63.5 trilioni. Fahamu, Deni la Serikali ni tofauti na deni la taifa, kwani deni la taifa linajumuisha mikopo ambayo pia inakopwa na sekta binafsi kwenye mashirika na taasisi za nje.
Lakini, deni la taifa ndilo linalotoa sura nzima ya hali ya ukopeshwaji wa taifa na ikiwa kama taifa tunalo deni stahimilivu au endapo hali ni tete. Mpaka kufikia Oktoba 2021, deni la taifa lilikuwa ni Sh82.3 trilioni huku deni la Serikali ikiwa ni 71.6% ya deni lote.
Serikali ya @MagufuliJP ilipoingia madarakani (05 Nov 2015) Deni la Taifa la Nje (external debt) lilikuwa Sh35 trilioni. Ongezeko la Sh16 trilioni kutoka wakati wa serikali ya @jmkikwete ambaye wakati anaingia madarakani Deni la Taifa la nje lilikuwa Sh19 trilioni (Nov 2005)
Serikali ya @SuluhuSamia imefanikiwa kulifikisha deni la nje (external debt) Sh66 trilioni tangu iingie madarakani (19 March 2021). Kufikia June 30,2021 deni la serikali lilikuwa Sh65 trilioni kulinganisha na Sh57 trilioni mwaka 2021 ongezeko ni Sh7.76 trilioni sawa na 13.7%
Deni la ndani (domestic debt) kufikia Machi 2022 limefika Sh50.73 trilioni kuna ongezeko la Sh13 trilioni kutoka Machi 2021 wakati @SuluhuSamia anaingia madarakani. Jumla ya deni lote la TAIFA (National Debt) ni Sh88.15 trilioni kufikia April 2022. Tafsiri yake, deni limepaaa!
Serikali ya awamu ya nne chini ya @jmkikwete ilipoingia madarakani (November 2005) ilikuta deni la taifa la nje ni Sh18 trilioni, hadi serikali hiyo inaondoka madarakani miaka 10 baadae (November 2015) deni la taifa la nje lilikuwa Sh35 trilioni. Ongezeko la Sh16 trilioni.
Ipo hivi, moja kati ya dhamana ya serikali inapokwenda kuchukua mikopo, Asset kubwa ya Serikali ni wananchi wake na rasilimali za nchi. Sasa mmeamua kukopa kwa fujo hivi ili kutuweka wananchi rehani? Rasilimali zetu? Rasilimali fedha zetu (foreign reserve)? Ama namna gani?
Serikali ya @SuluhuSamia wizara ya fedha ikiwa chini ya @mwigulunchemba1 wamefanya nini kikubwa hadi deni la taifa lipae kutoka Sh57 trilioni hadi kufikia Sh88.15 trilioni kwa muda wa utawala wao? Wanataka tufike kwenye debt stress? Pesa zimefanya lipi? Wapi? Lini?
MMM, Mtikila!

Loading suggestions...