Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

22 Tweets 2 reads Dec 08, 2022
HACKING NA HACKERS🔥🔥
UZI 🧵
PICHA LINAANZIA 2014 usiku wa manani,ingawa tumezoea usiku wa MANANE ila sahihi ni USIKU WA MAANANI wahuni wanalegeza kwa kuita NIGHT KALI,ndani ya RUSIA mhuni mmoja akiwa amelala zake geto akapokea simu like
“Haloo nani mwenzangu night kali yote hii?” kwenye simu alisikika mwamba ambaye alikuwa kama kachanganyikiwa hivi.Huyu mhuni ninayekwambia alipokea simu night kali, kimsingi sio mhuni ni MWAMBA kabisa tena mtalamu wa mambo ya ‘kukorokochoa’ komputer na software kutoka kutoka
kampuni ya KASPERSKY (tamka Kaspa-skai) kampuni maarufu ya ulinzi wa kidigital nchini Urusi.Kwa watumiaji wa Computer wengi wanafahamu jina hili Kasper- SKy tangu kitambo,
kwasababu ni wanatengenezaji wa Antivirus za computer nyingi.
Ukisikia Antivirus kama upo Tanzania simaanishi ile Movement ya PiPOZ PAWA ya Ramadee ,sugu na wenzake Dhidi ya Mwenda zake Ruge. LA HASHA! Na kama hujawahi kabisa kusikia ANTIVIRUS ya KASPERSKY ninayoizungumzia hapa, basi fahamu tu ni CD flani iliyokua inauzwa steshenari ,
ambayo ndani yake ina program inayoilinda computer yako dhidi ya virusi hasa ukiwa ONLINE au ukiingiza flashi.Kibongobongo utasikia “Angalia Usiniwekee Flashi yenye wadudu”.Sasa kama una hiyo KASPERSKY unakua huogopi hizo mambo za wadudu.Hadi sasa zipo.
Sasa hao jamaa walitamba sana miaka ya nyuma wakati computer nyingi zilitumia Window 7 ambayo ilikuwa ‘vono-rabo’ kushambuliwa na wadudu.
Labda kiki yao imeshuka huku kwetu sana siku hizi kwasababu mifumo ya computer imeimarika sana dhidi ya wadudu au tatizo ambalo KASPERSKY
walikua wanasaidia kutibu. So Demand imebadilika Lakini jamaa wapo na Labda ulishatumia huduma zao ila leo ndo umegundua ni kampuni ya Urusi? Well,Habari ndo hiyo asemavyo Ay na Mwana Fa.
So mfanyakazi wa hii kampuni ndiye alipokea simu ikiwa inatoka kwa jamaa mmoja mwajiriwa wa bank kubwa nchi Russia.Huyu mwamba aliyekua anasikika kwenye simu kama amepanik, alimwambia “MKUU NDUGU YANGU,mkuu ndugu yangu,nimekuita mara 3 mkuu ndugu yangu, nina msala mzito."
Akaulizwa MSALA GANI MZEE BABA?Hata hujajitambulisha?” Akajibu “MKUU NDUGU YANGU nimepigwa na kitu chenye ncha kali na Kizito na wahuni! Akamwambia hata simu yake haiamini tena na hawezi kuongea kwenye simu issue husika, akaomba pliiiz waonane haraka iwezekanavyo wazungu
wanasema ASAP yaani AS SOON AS POSSIBLE!Hivi ndiyo story ilianza ya kuja kukamata genge hatari Zaidi la wadukuzi kwenye historia ya wizi wa mtandaoni. Na Hii itatuingiza DEEP lakini kwa lugha nyepesi uelewe kuhusu UDUKUZI na WADUKUZI kwa yai tunaita HACKING AND HACKERS .
Huu ndio ualifu hatari zaidi kwenye dunia tuliyopo na ijayo. Katika episode hii kwa lugha rahisi utajua nini hasa hufanyika kwenye hacking kuanzia account yako ya social media,hacking kubwa kama za Mabank,n.k kwasababu kuna yale maswali utajiuliza au tunajiulizaga...
hivi blaza HACKER anajuaje password yangu?na je?kifupi hawa mablaza hackers huwa wanafagafanyagaje ?na zaidi UJILINDEJe? ONE THING FIRST,Kama utafuatilia hii EPISODE kwa lengo la kujifunza kuhack watu,basi utatoka kapa kwasababu sio lengo letu wala utakachokipata,😁😁🚮
Na pia ni kazi inayohitaji vitendea kazi kuanzia mashine za computer hadi ulinzi wa kidiplomasia na jeshi sometimes na ukitiwa mikononi pia Wanasema Jela haziwahi kujaa.Nadhani ushasikia pia KOREA KASKAZINI ikilaumiwa kujiendesha kwa kazi hii.
So twende nikupe ulimwengu huu unavyofanya kazi na utaanza kupata uelewa wa mambo mengi unayoyasikia tu. Turudi kwa yule mwamba aliyepiga simu KASPASKY.Walipokutana ndipo mwamba akatoa ya moyoni kilichompata akasema wamegundua kwamba SYSTEM kuu ya bank yao YAANI DOMEIN CONTROLLER
yao pale Russia, inatuma taarifa kwenye server nyingine iliyopo CHINA mji wa MACAU.Picha linaanza hiki ni kitendo kinachoashiria hatari kiasi gani ,utajua ukielewa domeini kontrola yenyewe ni nini. Ukisikia DOMAIN CONTROLLER hii ndiyo sever au shina kuu la system yote ya biashara
au taasisi yoyote inayotumia computer kwa issue zao.Hata vifaa kama simu vina hii sehemu,ambayo taarifa zote zinahifadhiwa kama zilivyo.Hii ndiyo sehemu EDWARD SNOWDEN alisema serikali ya Marekani hupewa access na makampuni yake,kuweza kuacces simu yako au yeyote duniani au email
Ukiweza kuingia kwenye DOMAINE CONTROLLER ya kampuni au biashara yoyote maana yake una access ya kila kitu kwenye system husika.Kwa kesi kama ya bank,ukishakuwa na access ya eneo hili maana yake una uwezo wa kufanya na kuona kila kitu ikiwemo taarifa za wateja na account zao zote
Unaweza kuhamisha au kuingiza pesa kwenye account yoyote,au hata kutuma mabilioni ya dolla kupitia system ya SWIFT ambayo hutumika duniani kote.Means unaweza kuhamishia hata account zilizo nje ya nchi husika.Kifupi unakuwa unamiliki bank husika na una access kuliko wafanyakazi
Kama ulifuatilia Sakata la RUSSIA na Ukraine utakumbuka moja ya vikwazo ni kuwaondoa kwenye system hii ya SWIFT ambayo ni kama GMAIL ya Mabank, yaani kama tunavyowasiliana na GMAIL au whats app BASI MABANK YANAWASILIANA KWA SYSTEM HII kufanya miamala.
So ukiingia DOMAIN CONTROLLER ya bank maana yake una access hii na ndicho kilitokea siku hii na ndicho chanzo cha wenge lililompata mwanetu baada ya kugundua DOMAIN CONTROLLER imeingiliwa kwa mlango wa nyuma kiambaruti ,tena na wahuni ambao bado alikuwa hajui wameshafanya mangapi
mpaka muda huu.Kama nilivyokuambia wangeweza kuhamisha kiasi chochote, muda wowote lakini utaelewa kwanini huwa hawaibi muda huo huo? Kuna process.
Process gani? Ilikuwaje wakakamatwa? Vipi walifanikiwa? #PichaLinaendelea huu ni mwanzo tu wa story
Usikose kutuskiliza kila Jumamosi kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 10 jioni kupitia @earadiofm

Loading suggestions...