WatuNiStory
WatuNiStory

@watunistory

4 Tweets 1 reads Aug 20, 2022
"Aisee leo nafika ofisini asubuhi nakuta kuna mbaba mmoja hivi ananizidi ka miaka 15 ila ni mshikaji wetu pale ofisini, akaniomba nimpe kampani home kwa mke wake (ukweni), aisee tumefika kule usukumani (Nje ya Mwanza kidogo kama unaelekea Misungwi).
Tumekaribishwa chakula tumekula sijui ni chakula gani mpaka tunamaliza, sikutaka kukikataa wala kuuliza ni chakula gani ila ki ukweli sijawahi kula chakula cha hivyo tokea nazaliwa sikutaka nimuaibishe jamaa yangu ukweni.
Ile tusharudi kutoka kule nikamuuliza, akaniambia ni michembe.... Ngoma ilikuwa imesongwa ina rangi ya zambarau haina radha kabisa!. Halafu ilibidi mwanaume nimalize.
Yaani nilikuwa nakula kibabebabe tu vitu vipite shingoni.
Tujifunze kuadapt kulingana na tunavobadilisha mazingira, unless otherwise tutaaibika au kuwaaibisha rafiki zetu maana utafutaji huu unajikuta ushachangamana na jamii ambayo hukufikiria maishani mwako kama unaweza kukutana nayo". Anonymous, Mwanza.
#WatuNiStory

Loading suggestions...