Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

25 Tweets 27 reads Sep 09, 2022
ANGUKO LA BIBI QUEEN ELIZABETH WA UK.
#PichaLinaanza Picha linaanzia kisiwa cha Barbados anakotokea RIHANNA kipenzi cha mashabiki wa mziki duniani, na litasambaa kwingi kwingine kwasababu kila unachokiona kinatokea
kimezungukwa na chain ndefu ya matukio na mlolongo wake na hapa tukuunganishia doti zote uelewe kwanini na kivipi ilitokea.True story mpya 2021 ni Bibi koko au kenya wanasema Nyanya wetu ELIZABETH II Malkia wa Uingereza anazidi kukimbiwa na wajukuu tena mchana kweupee.
Taarifa za Barbados kujitangaza rasmi kama JAMHURI ni hatua moja lakini inaamsha maswali kwa ambaye hujawahi kujua kwamba MALKIA wa uingereza hadi leo anatawala nchi kibao.Yaani wanamtambua kama KIONGOZI MKUU WA NCHI na incase you don’t know acha nikupe majina yao AUSTRALIA,
VISIWA VYA BAHAMAS,CANADA, GRENADA,JAMAICA,NEW ZEALAND,VISIWA VYA SOLOMON, TUVALU ,na hizo ni kwa uchache na nyingine ni visiwa ambavyo labda hujawahi kuvisikia sana kama unaishi africa na baadhi tutakuwa ndo tumeshangaa leo kusikia hadi CANADA,
nchi ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani hadi leo inaongozwa na MALKIA ambaye kanchi kake ni kisiwa tena kidoooogo ambacho hata mfukoni hakijai.Utajifunza akili ni nywele.Mbali na hao kuna wenzake kama AUSTRALIA,JAMAICA,NEW ZEALAND kwamba zinatawaliwa na MALKIA hadi leo.
Utajiuliza imekuwaje? au huyu bibi mchawi?
Kuna nchi ziliwahi kufanya walichokifanya BARBADOS kumuondoa QUEEN ELIZA kwenye utawala wa kikatiba.GUYANA walifanya hivyo 1970,TRINIDAD AND TOBAGO wakamkataa bibi 1976,DOMINICA ambao ni majirani wa HAITI walimkimbia Bibi 1978
TRINIDAD AND TOBAGO wakamkataa bibi 1976,DOMINICA ambao ni majirani wa HAITI walimkimbia Bibi 1978 wakafuatiwa na MAURITIUS(tamka Maurishaz) 1992 na 2020 BARBADOS wakaanza mchakato wa kujiondoa kutoka kuwa WATOTO WA BIBI kama JAMBO SQUAD wa arusha,
na sasa ni watoto wa MAMA kama ilivyo Tanzania.Rais wao ni Mwanamke na Rihhana kala mashavu kibwena.
Hiki ni kisiwa kilichopo kwenye ile bahari inafahamika km CARIBBEAN SEA.Najua sometimes huwa inachanganya hii CARIBBEAN SEA ndo ipi tena?Well ,kwanza kuna tofauti ya OCEAN na SEA
Kwenye kiswahili labda BAKITA watusaidie lkn huwa tunasema bahari tu lkn unaposikia OCEAN na SEA zina maana 2 tofauti kidogo.Ocean ni eneo lote la BAHARI na SEA ni sehemu ya maji ya bahari ambayo yapo karibu au yamezungukwa na nchi kavu km kisiwa n.k .So SEA ni ukanda wa bahari,
OCEAN ni BAHARI YENYEWE.
Kifupi ni kama unaposema MKOA na WILAYA so OCEAN ni MKOA alafu SEA ni wilaya. Viumbe wengi tunaowajua na kuwategemea kila siku baharini wanapatikana SEA areas na sio OCEAN,wale wanaopatikana kwenye OCEAN ni wale ambao sio rahisi kuwawinda kirahisi.
Kina nyangumi na wenzake.
so ukisikia CARIBBEAN SEA tunazungumzia eneo ndani ya ATLANTIC OCEAN ambalo lina visiwa na nchi kibao zinazoisogelea bahari hiyo kama BAHAMAS,COSTA RICA ,CUBA ya mzee Fidel Castro,JAMAIKA ya wazee wa kukiwasha cha chuga,HAITI ambao juzi kati tulikuletea
la rais wake kuuawa,MEXICO, NICARAGUA ,PANAMA na vingine kibao.Vingine wanamiliki Matajiri ambao either wanatoka Marekani au UINGEREZA.Juzi kati kwenye kisiwa kimoja wapo ya hivi matajiri wa Marekani akiweno JEFF BEZOS walishutumiwa kukwepa kodi kupitia makampuni haya.
Visiwa vingi hivi vina sheria loose za kodi so matajiri wamegeuza ndo peponi kwao.Story ya siku nyingine hii.
Duniani kuna jumla ya BAHARI kwa maana ya OCEAN 4 na 1 imeongezwa juzi kati so zimekuwa 5,Atlantic, PASIFIC,BAHARI yetu ya HINDI,na ARCTIC OCEAN
na baadhi ya nchi ikiwemo marekani wanaitambua ANTARCTICA kama bahari ya 5.Tho kiuhalisia ANTACTICA ni bara lililoganda so ni barafu tupu na hakuna mtu anayeishi ila wapo watu kadhaa wanaoishi huko lakini wote sio raia wa kawaida,ni wanasayansi wa nchi mbalimbali kubwa.
So sehemu za bahari zinazoitwa SEA huwa na kina kifupi cha maji kwasabab ya kuwa karibu na nchi kavu lakini CARIBBEAN SEA ni eneo lenye kina kirefu cha maji kuliko hata baadhi ya OCEAN lakini kinaitwa SEA kwa sababu hyo ya kuzungukwa na nchi kavu sehemu nyingi kuanzia MAREKANI
YA JUU yaani USA na CANADA hadi MAREKANI KUSINI yaani nchi za SOUTH AMERICA.Kwenye Live na Gee moja tuliongea na mshakaji anaishi COSTA RICA na ni sehemu ya hizi nchi za carebian.
So kwenye huu UKANDA WA BAHARI WA CAREBIAN ni karibu sana na Marekani na pili ni washkaji
na UINGEREZA kiutawala hadi leo ndo maana ukitokea humu unaweza kuruhusiwa kutoboa kirahisi endapo ukienda kuishi Marekani kama RIHANA ambaye anatokea hapa BARBADOS na Wyclif JEAN anayetokea HAITI lakini staa mkubwa marekani.Hutoboi kama hutokei hizo nchi.
Nadhani umeelewa sasa kwanini Drake ni mcanada lakini anahit Marekani,ni kwasabab Canada ni sehemu ya imaya za Malkia. Na Uingereza na Marekani ni ndugu wa kihistoria kwenye damu hadi kisiasa.
Rafiki yetu hayati BABA T pia mtangazaji wa rege aliyefariki akiwa Tanzania alituambia alizaliwa JAMAICA na ikatokea nafasi wakaambiwa wakatafute maisha UINGEREZA kwasababu kama hizi .Kiongozi wao mkuu kikatiba ni MALKIA WA UK.swali linabaki pale pale WHAT THE FVCK?
Ina maana huyu bibi hataki kuachia nchi za watu? Kwanini?Faida yake ni nini?Kwanini wengi hawajitoi?PICHA LINANOGA . Usiku mmoja akaibuka MAMA ambaye ni WAJINA wa mama chibu DANGOTE ,bi Sandra Mason na kumwambia “BI ELIZA TUMEKUCHOKA PITA HIVI"
Bi SANDRA ana miaka 72 na ndiye general mkuu wa nchi na anakuwa rais wa kwanza na kufanya RIHANA kuwa mzaliwa wa nchi kamili,mwanzo Rihana alikuwa binti wa BIBI ELIZA lakini sasa atatambulika rasmi kama BINTI WA MAMA SANDRA na kwenye huu mchakato Rihanna ni kati ya watu maarufu
kutoka Barbados waliopata mashavu ya kutunukiwa heshima na sasa anatambulika kama Mheshimiwa RIHANA, yaani kifupi DA RiRI KAMA RIRI kuke kwao ni kama KONDE BOY ambaye alifanya hadi leo vijana kutoka mtwara wanajiskia FAHARI kutamka I AM kondeboy au Kondegirl.
Movement ya Black Lives Matter ilipush sana kuisadia Barbados kupata uhuru wake maamuzi ambayo yalishaamuliwa miaka 20 iliyopita na tume ya serikali lakini mizengwe ikawa mingi.Wamefanya hivi kama kampeni pana inayoendelea ya kuvunja ushkaji uchwara na UINGEREZA na kujenga
zaidi na nchi za AFRICA ambapo wananchi wengi wa Barbados wanapotokea kiasili.
Hii ni Intro tu tutazama deep ujue walifikiaje hapa? Kwanini Malkia anatawala nchi zote hizo?
Isome hii story chap kwenye kitabu chetu cha Episodes 50 za madinidotcom.
☎️ 0712 760 276

Loading suggestions...