Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

24 Tweets 5 reads Dec 08, 2022
KUPANDA KWA MAFUTA, DOLA NA SIASA ZAKE. 🧡
Ukweli na uhalisia ambao hatutabishana sana ni kwamba 'wese limepanda' na maisha yamepanda kote duniani na kifupi TUNAOUMIAniSisi na sababu zipo kadhaa,lakini KUBWA LAO sio vita Ukraine na Russia inayoendelea kama wengi wanavyo simplfy
Trustory kisa na mkasa wa yote haya ni wahuni wa kuitwa The Organization of the Petroleum Exporting Countries kwa ufupi 'OPEC' Kama zamani ulisikia zile za kijiweni kwamba Marekani wako na 'stoku' ya mafuta ya kutosha kutumia miaka hata 100 mbele?
Basi ulipigwa na kitu chenye ncha kali ,Kwasababu Trustory ndicho kinachomzururisha rais Biden ziarani Saudia Arabia kuomba OPEC wazalishe mafuta wahuni wanaumia!Utajiuliza kwanini Marekani wasichimbe mafuta yao?au Kwani mafuta yanachimbwaje au yanapatikanaje?
Tukijadili WESE mara nyingi nchi zinazotajwa ni ukanda wa mashariki ya kati na uarabuni na hilo ni swali la kwanza juu ya kwanini wao tu? Kwa tuliopo afrika mashariki issue ya mafuta inakwenda kubadili kabisa taswira tunayoiona kufikia 2025
kwasababu tutakuwa ukanda wa mafuta na kuna dili inaendelea kati ya UGANDA na TANZANIA ambapo litajengwa bomba refu zaidi duniani la mafuta ghafi yaliyochemshwa(HEATED OIL) .
Haya mafuta yaligunduliwa 2006 eneo la KABAALE magharibi mwa Uganda ,
So kuelewa saga zima la mafuta na kwanini ndo chanzo cha kila kitu ni vizuri tukupe kwanza historia ya uwepo wa mafuta duniani.Kama ulikua nasisi tangu kwenye season 1 tulikuletea teknolojia ya nishati ya nyuklia audiomack.com
Ambayo tuliona lengo lilikuwa kureplace Nishati ya mafuta ambayo kimsingi ndio inaongoza dunia, tuliona nyuklia ilivyoanza tangu siku ya kwanza hadi kugeuka nishati kubwa na hatari,je?mafuta yalianzaje?Acha tuzame ndichi kwa fasi ya Somo la history chap kwa ufupi na wepesi.
Mpaka sasa jibu la kisayansi juu ya chanzo cha uwepo wa mafuta, hata mimi sipendagi sana kumuaminisha mtu, nitakuelewesha wanasega nini lakini ukiona huamini basi tukubali tu MUNGU FUNDI.Lkn wanasema ni matokeo ya mgandamizo wa mimea,viumbe waliowahi kuishi duniani na mazagazaga
kibao yaliyovunda ardhini ambapo vilitengeneza hewa ya HYDROCARBON.
Hii HAIDRO-KABONI wala isikuogopeshe,hili jina ni kitu kinachotokeaga pale kemikali za asili wanaita Organic chemical yaani unajua kuna zile kemikali za maabara au za kutengeneza mwenyewe,kwa mfn kuna chemikali
zinaweza kujiumba zenyewe tu labda umetupa makopo ya vinywaji na vyakula sehemu moja,then zinajimix zikivunda huenda kuna chemical zinajitengeneza,sasa ile chemical ikikutana na gesi ya Carbon kama tunayopumua ndio inaitwa HYDROCARBON. Hii ndo ambayo mafuta yote hukutwa nayo
kwa kiasi kikubwa na ikiondolewa ndo tunapata mafuta safi ya kutumia,ukisikia MAFUTA GHAFI au CRUED OIL ujue ni kabla hayajawa tayari na nitakuelezea process yote.
Mfumo huu pia ndio asili cha MAKAA YA MAWE kwa mujibu wa Sayansi na kwenye episode yetu kuhusu NISHATI ya NYUKLIA
tulikuambia pia makaa ni kati ya VYANZO VYA nishati TULIVYONAVYO DUNIANI since long time NA KABLA YA MAFUTA kugundulika,hata vita ya kwanza ya dunia watu walikuwa wanapigana kwa meli za makaa ya mawe, baadaye wese likaingia na meli zikaanza kubadilishiwa injini kuwa na speed zaid
na pia wepesi wa uendeshaji..So makaa ya mawe yalitokana na wale viumbe hai na microarganism waliofariki wakiwa nchi kavu na mafuta ni wale waliokuwa Baharini na mafuta kutoka kwa viumbe wa kale waliofariki majini.Utauliza Viumbe wa kale gani tena?Nini kiliwaua?Well,
imagine huu ni mwaka 2022, it means ukirudi nyuma kutoka hapa tulipo hadi kufika mwaka wa kwanza bado ni michache sana ukilinganisha na umri wa sayari hii dunia. So hiyo inatupa uelewa tu kwamba before maisha haya, kulikua na maisha mengine ambayo ni ngumu hata kuimagine.
Na labda itakupa swali sasa iweje Saudi arabia au uarabuni ndo lilipo wese la kutosha wakati sehemu kubwa ya nchi husika ni jagwa tupu kuliko bahari?well ni kwasababu miaka milioni 100 iliyopita, inaelezwa sehemu kubwa ya jangwa ikiwemo jagwa la sahara likuwa maji matupu,
Yes na bahari hiyo iliitwa Tethys Ocean(Te-thi-s) na ukienda ku google utaona .Enzi za skuli tulishafundishwa kwamba HAPO zaMani ZA KALE dunia iliku bara 1 lililoitwa PANGEA na kama unatumia vizuri internet yako, youtube kuna story za video za mifano ya bara hili la zamani
au muonekano wa dunia ya zamani sana according to historia.
Kile kilisababisha dunia ikagawanyika na maji kuingia katikati ndo athari hizo ambazo zilifanya kutengenezeka kwa HYDROCARBON kutoka kwenye mazalia ya viumbe hao wa zamani waliokuwa wanaishi duniani.
Kuzungumzia nini kilitokea wakati huo,ni topic nyingine pana na tofaut kabisa na hii ya mafuta,hivi vipindi au Era mbalimbali dunia iliyopitia na viumbe waliokuwepo Zinaitwa geological periods.
Kwahiyo mafuta yanachimbwa au kupatikana baharini na pia kuna yanayochimbwa nchi kavu
na utofauti huu wa sehemu ya upatikanaji unatofautisha pia quality ya mafuta yenyewe na pia gharama za kuyapata. Ni kwasababu uso wa dunia tuliyopo umegawanywa kwenye visahani au tuseme Bakuli kadhaa na kila plate ndani yake kuna ujiuji wa moto ambao ndio unakuwa kama superglueπŸ‘€
ya sayari tulilopo so kadri dunia inavyozunguka kuna wakati plate moja husogea na wanasema ardhi ya dunia ina move kwa cm 1 –13 kila mwaka.Mfano PLATE ya INDIA ilivyosogea na kukutana na plate ya EURASIA ndo kulizaliwa safu ya milima maarufu ya HIMALAYA iliyotenga INDIA na CHINA
na nchi nyinginezo...So wakati huu ambao ardhi ya dunia ilikuwa inamoove na kukutana,katikati ya INDIA na EURASIA ndo kulikuwa na bahari hii iliyotoweka Tethys Ocean na baada ya ardhi kusogeleana ndipo eneo lililokuwa chini maji miaka yote lilijitokeza juu ya dunia na eneo hilo
siku hizi linafahamika kama NCHI ZA MASHARIKI YA KATI au kwa kihaya wanaita MIDDLE EAST (mido isti) ambalo lina nchi kama SYRIA,IRAQ,IRAN,SAUDI ARABIA,KUWAIT,BAHREIN,OMAN ,YEMEN,JORDAN,ISRAEL bila kusahau QATAR tunapoenda kuchezea kombe la dunia .
Hii ni 3.4% ya ardhi yote ya dunia lakini karibu nusu ya yaani 48% ya supu yote aina ya wese ilikwenda kujikusanya hapa na nishati asilia nyingine ambapo mashariki ya kati ina 38% ya nishatia asilia yote duniani mbali na mafuta
audiomack.com
#PichaLinaendelea lengo ni upate #TaarifaNaMaarifa kaa sisi uendelee kujifunza mengi, story nzima inapatikana hapa; audiomack.com

Loading suggestions...