Madinidotcom
Madinidotcom

@madinidotcom

10 Tweets 1 reads Dec 08, 2022
ZIMEVUJA, AMRI 6 ZA ELON MUSK KWA WAFANYAKAZI WAKE WA TESLA,SPACE X NA TWITTER n.k .Ameziita “Productivity recommendations"
No meetings zisizolazima na kama huna la kuchangia sepa "walk out". #PichaLinaanza
Bosi mpya wa Twitter bilionea ELON MUSK ametuma emails ya maelekezo/Mwongozo kwa wafanyakazi wake za namna ya kuwa na tija kazini,No vikao visivyo na umuhimu na ukiona huna la kuchangia kwenye kikao ‘sepa’ .Pedeshee Musk ametuma maelekezo haya kwenye kampuni zake nyingine pia.
Wahuni wakazianika kwenye ‘sosho media’ na zipo kama ifuatavyo kwa ufupi.
1.EPUKA MIKUTANO YA MTU KIBAO (WATU WENGI).
Mikutano ya watu wengi inapotezaga muda na ‘eneji’ ya watu.Pia wanavuruga-ga mada kwenye majadiliano,Watu hujikuta hawawi wawazi kama mikutano ya wachache.
Pia hakuna muda wa kutosha watu wote kuchangia.
Usiitishe mikutano ya watu wengi ambao hawatakuwa na chance ya kuchangia.Unless kuna jambo muhimu sana.
2. KAMA HUNA LA KUCHANGIA “SEPA” .
Ukiona meeting haihitaji sana mchango, maoni au maamuzi yako ‘pita hivi’ .Sio ‘ukorofi’ kuondoka kikaoni,ni ‘ukorofi’ kumlazimisha mtu kubaki kupoteza muda. “it is not rude to leave, it is rude to make someone stay and waste their time."
3.EPUKA MLOLONGO (URASIMU)
Wasiliana na mhusika moja kwa moja sio kupitia meneja wala ‘supa-vaiza’ wake.Inarahisha kufanya maamuzi ya haraka na ndo huleta tijaYaKazi. “Fast communicators makes fast decisions. Fast decisions = competitive advantage”
4.SOMEKA USILETE UJUAJI
Epuka maneno ya ‘kitaalamu’ sana “BE CLEAR, NOT CLEVER” someka(eleweka) .Ongea na watu kwa namna watakayoelewa unachomaanisha sio ili wajue unaelewa sana unachowaambia. “we don’t want people to have to learn to a glossary to function at Tesla"5.
5.ACHANENI NA MIKUTANO YA MARA KWA MARA.
Ni kupotezea watu muda,tumia mikutano kuongeza ushirikiano,kujadili jambo lililo mbele yenu au kutatua tatizo la ghafla au linalohitaji ‘solusheni’ ya chap.Baada ya kutatua 'ishu' husika mikutano sio lazima.
6.TUMIA COMMON SENSE.
Kiujumla tumia akili/busara.Kama sheria za kampuni hazi-make sense,hazisaidii kuboresha utendaji au haziwezi kuapply kwa ‘situesheni’ ya muda huo,tumia akili.
“Avoid following the rule with your eyes closed. Don't follow rules. follow principles.”
Najua una la kusema ukilinganisha na mazingira ya kazi uyajuayo. Story ya huyu mwamba tunayo na tayari tupo Part 1 - 2 zipo hapa audiomack.com na ukizama youtube.com
Tulikuahidi #TaarifaNaMaarifa

Loading suggestions...