James Munisi
James Munisi

@NjiwaFLow

21 Tweets 3 reads Dec 08, 2022
MFAHAMU ‘Bruce Reynolds’ MASTERMIND WA TUKIO LA ‘Great Train Robbery’.
SEHEMU YA KWANZA
#UZI
💨Sijui kama unalikumbuka au kama umeshawahi kusikia kuhusu tukio la Mwaka 1963 la ‘Great Train Robbery’ ambalo linatajwa kama moja ya “Britain's largest robber”.
7 September 1931 Bruce Richard Reynolds alizaliwa pale katika Hospitali ya Charing Cross Hospital, Strand, central London akiwa kama mtoto pekee wa baba yake Mzee Thomas Richard na Mama yake Dorothy Margaret (née Keen).
Mama yake na Bruce alikuwa nesi, na kwa bahati mbaya alifariki Mwaka 1935, wakati huo Bruce akiwa na umri wa miaka 4 tu.
Kutokana Na Mifumo ya kimaisha, ikabidi baba yake na Bruce, Mzee Thomas ambaye alikua ni ‘trade-union activist’ pale ‘Ford Dagenham assembly plant’, aoe tena
Kisha familia nzima ya Mzee Thomas ikahamishia Makao yake kule Gants Hill, London Mashariki.
Lakini baadae kidogo, Bruce akaona maisha chini ya Mzee wake Pamoja na Mama Wa Kambo kama yanataka kumshinda hivi, akaona ni bora hata akaishi na moja ya bibi zake.
Lakini kufuatia na mbilinge mbilinge za vita ya pili ya dunia, Bruce alikuwa evacuated kwenda Kule Suffolk na kisha baadae akafika mpaka
Warwickshire.
Akatamatisha masomo yake akiwa na miaka 14½, na kisha akaona akajaribu bahati yake jeshini kwa kujiunga na “Royal Navy”.
Huko Jeshini nako mambo yakamuendea vibaya kwasababu alifeli kwenye ‘eyesight test’.
Kwaio mwisho wa siku akaamua kuwa ‘foreign correspondent’.
Ili unielewe kuhusu kuwa ‘Foreign Correspondent’, soma hapa👇
Kwaio aka apply kazi hio pale Northcliffe House, na kisha akaipata.
Alipofikia Umri wa Miaka 17, akaona yuko-bored na hio kazi hivyo akaenda kufanya kazi kwenye taasisi ya ‘Bland/Sutton Institute of Pathology’ pale Middlesex Hospital.
Akatoka hapo na kisha kwenda kufanya kazi na Claud Buttler, ambapo alianza kama ‘bicycle messenger’ na kisha akawa ‘member of their semi-professional racing team’, ambapo hapo sasa ndio Ukurasa wake wa Matukio ya kihalifu ukafunguliwa rasmi.
Kipindi yupo hapo kwenye kazi yake ya sasa, ndipo alipoanza tabia ya udokozi dokozi.
Akaiba iba hapa na pale, na kisha kuwachoropoka polisi mara kadhaa, lakini baadae kidogo aliweza kukamatwa na kuswekwa lupango.
Mwaka 1952, Akakaa Nyuma ya nondo za gereza la Wandsworth Prison Pale London.
Baada tu ya kutoka, akahusishwa kwenye tukio fulani la wizi wa vito vya thamani vya fedha nyingi sana.
Mwaka 1957, akakamatwa tena, mara hii akihusika kwenye wizi wa zaidi ya £500 kutoka pale…
…White City Greyhounds akiwa na Mwanae Terry Hogan.
Hogan akala kifungo cha Miaka 2½ Jela huku Bruce akala Miaka 3½, Mmoja akatupwa gereza la HMP Wandsworth na Mwingine akatupwa gereza la HMP Durham.
Mwaka 1960 Bruce akaachiwa huru.
Mara hii baada tu ya kutoka jela, akajiunga na kundi la kihalifu, ambalo lilikuwa na yeye, rafiki yake wa muda mrefu Harry Booth na mtu kama John Daly.
Kisha Jimmy White na Buster Edwards wakatia timu kundini, na kisha wakakutana kwenye Club moja ya mchizi wao Charlie Richardson
Huyo Charlie Richardson akamu-introduce Mwanetu Bruce kwa Mchizi aitwaye Gordon Goody.
Kwa Kiasi fulani, Kundi lilikua limeshakamilika , na kilichokuwa mbele yao utekelezwaji wa matukio ya wizi tu.
Mwaka 1962, Kundi hilo likafanikiwa kuiba kama £62,000 kutoka kwenye ‘security van’ moja hivi iliyokuwa imepaki kwenye Parking za Heathrow Airport.
Baada ya mchongo huo kutiki, sasa Kama kundi wakawa wanafikiria kuiba £700 zilizokuwepo kwenye Treni moja ya Royal Mail,
Ila…..
Upande wa pili, Bruce alikuwa ameanza Mipango ya tukio la Miezi mitatu mbele, la kutekeleza wizi wa kama £2,631,684 (equivalent to £58 million today).
Hakuna Kilichokuwa kikifuata mbele yake, zaidi ya mpango huo kuwashirikisha wenzake katika kundi hilo.
Bruce aliushirikisha Mpango huo kwa genge lao lote.
(NB: Genge Zima walikuwa kama 15 hivi).
Mpango Mzima ulikua ni Kuvuna Kitita hiko cha pesa ambacho kilikuwepo katika treni iliyokuwa ikisafiri kutoka London Kuelekea Glasgow kupitia ‘West Coast Main Line’ asubuhi ya 8 Aug 1963
Mpango mzima ulianza kutekelezeka baada ya Bruce na genge lake kufanikiwa kumpata mmoja kati ya senior security officer wa treni hiyo, ambaye alikuwa na taarifa kamili kuhusu wapi treni itapita!!? Lini!!? Saa ngapi!!? Na itakuwa na Pesa kiasi gani!!?
Lakini hili kundi la kina Bruce lilikuwa halina Ujuzi sana wa matukio ya utekaji na wizi wa treni, kwahiyo ili kuhakikisha hawafeli, ilibidi walishirikishe Kundi jingine la uhalifu lifahamikalo kama The South Coast Raiders, ambalo hilo lilikuwa na watu kama Tommy Wisbey,
…. Bob Welch, na Jim Hussey ambao hao walikuwa na wataalamu wa matukio mazima ya Wizi wa Mali zilizokuwa zikisafirishwa kwa Treni.
Katika Hili Group la The South Coast Raiders kulikua na mwamba Mmoja alikuwa anaitwa
Roger Cordrey,
….huyu alikuwa ni mtaalamu wa kuivuruga ‘track-side signals’ za treni za ambazo hupelekea treni Kusimama.
Je, Tukio lilikwendaje kwendaje!!? Lilifanikiwa Vipi!!?
Tukutane Jumatatu Jioni Hapa Hapa, Nikupe Mwendelezo wa Stori hii Tamu.
Naitwa Njiwa✅
WhatsApp
wa.me

Loading suggestions...