Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania

@radiomariatz

4 Tweets 19 reads Dec 12, 2022
FAHAMU RANGI ZA KASULA NA MAANA YAKE KATIKA KANISA.
Kasula ni vazi analovaa kuhani (Padri/ Askofu) kwa Kiingereza tunaita Chasuble hutofautiana kwa rangi kadri ya majira ya Kanisa.
1.Kasula yenye rangi ya Kijani huonyesha matumaini huvaliwa katika kipindi cha kawaida cha Kanisa
2.Kasula nyeupe huonyesha ushindi pia huvaliwa katika sikukuu za kikanisa au sherehe za Kanisa mfano Noeli,Pasaka n.k.
3.Kasula ya zambarau au urujuani huvaliwa wakati wa msiba, kipindi cha kwaresma na majilio huonyesha huzuni au toba.
4.Kasula nyekundu huonyesha ishara ya moto na mateso na pia ni ishara ya upendo. Huvaliwa katika siku za ijumaa kuu, Pentekoste, Dominika ya matawi.
na pia sikukuu ya mashaidi au wafia dini huonyesha damu iliyomwagika kwa ajili ya KRISTO pia katika sikukuu za Mitume.

Loading suggestions...