Ujenzi wa shule hiyo Mpya unatekelezwa kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 4 ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo.leo tarehe 06 Januari 2023.
Ujenzi unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya utekelezi wa mradi huo ulianza tarehe 6 April 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Januari 2023 na itatumia fedha Kiasi cha bilioni 3.Katika awamu hii ya kwanza vinajengwa vyumba vya madarasa 12,
jengo la utawala 1, maabara 4, matundu ya vyoo 16, chumba cha jenereta 1, bwalo 1,mabweni 5, mitaro ya maji, kichomea taka 1, matanki ya chini ya maji, matanki ya plastiki, uzio, njia za kutembea na nyumba za walimu 2.
Awamu ya 2 ya mradi huu unatarajiwa kuanza wakati wowote ndani ya mwaka huu kwa fedha na fedha kiadi cha shilingi kiasi bilioni 1 kitaletwa kutoka Serikali Kuu ambapo yatajengwa madarasa 10 yenye ofisi za walimu 3,chumba cha ICT,Maktaba,nyumba nne za walimu na mabweni manne (4).
Loading suggestions...