Millambo®
Millambo®

@Millambo_

9 Tweets 62 reads Feb 24, 2023
SHERIA 20 ZITAKAZOKUSAIDIA KUDEAL NA NDUGU IPASAVYO😎
Moja ya Changamoto kubwa ni namna ya kuishi na ndugu.
Yako mengi ya kujifunza.
Hizi hapa nondo 20 zitakusaidia kupunguza stress.
RETWEET Wengi wajifunze... 🙏
🧵📢
Usijaribu kuprove ndugu kuwa uko vizuri.
.
Watoto wako ndio watu pekee una WAJIBU wa kuwatunza hapa duniani.
.
Waheshimu sana wazazi wako. Jitahidi kuwasaidia kadri utakavyoweza.
.
Saidia ndugu zako pale unapoweza. Wema usizidi uwezo.
Ukijiweza badala ya kuwatumia pesa kila mwezi. Wafungulie mradi wa kuwasaidia kwa ujumla.
.
Usipende wala usikubali kusuruhu mgogoro wako wa ndoa usuruhishwe na vikao vya ukoo. Kataa.
.
Hata uwasaidie ndugu kwa kiwango gani, bado watalalamika tu.
Hakikisha ndugu hawajui kipato chako.
.
Mke wako ni wajibu wako. Usikubali ndugu wamguse. Mlinde.
.
Kufanikiwa sehemu uliyozaliwa na kukulia, ni jambo gumu sana.
Mwanaume ukishaoa, hakikisha unaishi mbali za ndugu zako.
.
Usikubali kuingia kwenye ndoa kwa shinikizo la vikao vya ndugu. Kataa.
.
Epuka sana ndugu (watu wazima) wanaokuja kuishi kwako. Ukiweza wasaidie huko huko.
Jitahidi ndugu wajue misimamo yako. Itakuepusha na mengi.
.
Usitumie nguvu nyingi sana kuwaelewesha ndugu. Wengine hawatakuelewa tu.
.
Ukitaka kufanya jambo kubwa usiwaulize ndugu.
Ukipata changamoto kubwa kwenye ndoa. Fanya utafiti. Jiridhishe 100% na ufanye maamuzi bila kuuliza sana watu.
.
Ndugu wote kwenye ukoo watadeal na wewe kadri unavyojiweka.
.
Ukiwa na familia. Usikubali mgeni yeyote kulala kwenye chumba kimoja na watoto wako.
Yule mchizi wako uliyekutana nae kwenye mishe atakuwa ndugu yako zaidi kuliko ndugu zako wengi.
RETWEET Wengi wajifunze... 🙏
Ili kujifunza zaidi kwenye Personal Development, Expert Business na Bio Hacking:
FOLLOW ME: @millambo_
Karibu sana kwenye group letu la Telegram:
Jeshi la Mtu Mmoja: 👇
t.me

Loading suggestions...