M.D (๐Ÿ…จ)
M.D (๐Ÿ…จ)

@ReganTesla_

16 Tweets 1 reads Mar 12, 2023
....INAENDELEA. ๐Ÿงต
Jesca aliposhushwa pale nyumbani alishushwa kama Mzigo tu hakukuwa na mzungumzo mengi, Vilishuswa vitu vyake kisha yeye akashukuka na mtoto wake. Kwenye ile gari kulikuwa na Wanaume wawili, Yule mmoja ambae sio dereva akamfuata na kumwambia Jesca samahani..๐Ÿ‘‡
Sana sisi tunatekeleza wajibu wetu ila pole sana kwa hili, Nakuhurumia sana sababu ni wengi wamefanyiwa kama wewe na nakushauri usije ukaendelea kuntafuta huyo bwana maana tunawajua waliokaidi wakamtafuta kilichowapata.
Jamaa akaingia kwenye mfuko wake akatoa Sh. milioni 1 ...๐Ÿ‘‡
Akampatia, akamwambia nikiambiwa nikupe huu mzigo. Jesca akazichukua zile pesa akazitupa. Jamaa akamfuata akamwambia Dada pokea hizi pesa sababu hata ukizikataa hautakuwa umemkomoa yeyote. Akazichukua akazipenyeza kwenye mkoba wake wakawasha gari yao wakaondoka...๐Ÿ‘‡
Jesca analia jamani ๐Ÿ˜ญ, Huyu dada analia mpaka anatia huruma. Anajiuliza anaanzaje kuingia kwenye ile nyumba aliyoitelekeza kwa miezi 7? Anajiuliza ni nani anaishi hapa kwa sasa, Mwanae Mkubwa vipi na kuhusu Ben Je?
Wakati anaendelea kuwaza aliskia sauti ya mlango..๐Ÿ‘‡
Kufunguliwa. Akajisogeza ukutani. Kwenye geti akajitokeza binti, Jesca anaona aibu kumtizama hajajua bado ni nani yule. Anaskia sauti "Oooh Dada Jesca Shkamoo"
Jesca anainua kichwa chake anakutana na dada ambae alikuwa dada wa kazi wa yule dada yake mshauri wake. Si...๐Ÿ‘‡
Mnamkumbuka? Jesca nae anaanza kushangaa , Haya ya vipi tena ina maana huyu binti kahamia nyumba hii au vipi? Jesca anachanganyikiwa anaona haelewi kabisa..
Jesca anakumbuka kuwa mambo mengi aliyopanga na yule Dada huyu binti alikuwa akiyaskia mara nyingi maana mipango..๐Ÿ‘‡
Ilifanyika zaidi kwenye nyumba ya yule dada. Jesca anashindwa kuzungumza chochote.
Anajikuta tena anaanza kulia. Binti nae ni kama haelewi anakuwa na mshangao anaona mabegi makubwa yapo chini, anamuuliza "Dada mbona unalia?" Kisha anamwambia samahani kidogo ngoja nakuja binti..๐Ÿ‘‡
Anataka kuingia ndani, Jesca anamwita anamwambia usiende kwanza embu njoo. Anamuomba wazungumze taratibu kwa ukimya, Anamuuliza anafanya nini pale na yupo nani ndani?
Binti anamwambia yeye na Dada walihamia hapo na sasa wanaishi na Ben.
Jesca anapigwa na butwaa..๐Ÿ‘‡
Mmaishi na Ben? Kivipi? Sijaelewa kabisa. Binti anamwambia mimi sielewi tu tulihamia hapa na sasa Uncle Ben ndio Baba na Dada yupo ndani amepumzika ni Mjamzito. Labda nimwite uongee nae.
Jesca anazidi kuchanganyikiwa anaishiwa na nguvu. Ghafla mtoto akaanza kulia analia sana..๐Ÿ‘‡
Mazungumzo yanashindwa kuendelea Jesca anamwita mtu wa Bajaji anamuomba apakie vitu vyake kisha ampeleke hospitali ya karibu anasema mtoto amebadilika hali yake.
Bajaji anakuja anawabeba, Jesca anamwambia Binti asimwambie mtu chochote iwe siri yao kama alikuja pale...๐Ÿ‘‡
Wanaondoka kwenda hospitali. Kufika Jesca anaambiwa mtoto ana homa kali pia anapumua kwa shida. Anaanza kupewa matibabu, Wakati wote huo Jesca hayupo sawa. Jesca amemuomba yule mtu wa Bajaji amtafutie guest ya karibu apeleke vile vitu vyake.
Jesca hataki watu wajue anakumbana..๐Ÿ‘‡
Na kitu gani. Bajaji kweli anafanya alivyoelekezwa, Vitu vinakaa guest. Jesca anabaki hospitali na mtoto.
Majira ya usiku Jesca anakuwa kama amechanganyikiwa anamtafuta mtu wa bajaji ampeleke alipoviweka vitu.
Jesca anaenda kule guest ila anachelewa sana kurudi hospitali..๐Ÿ‘‡
Madaktari wanaanza kumtafuta maana mtoto alianza kurudi kwenye hali yake ili apelekwe wodini maana alikuwa chumba maalum cha watoto wenye shida ya kupumua.
Inapita usiku mpaka asubuhi Jesca anarudi. Zinafuatiliqa taarifa mtoto alizotoa Jesca ili watafutwe ndugu zake...๐Ÿ‘‡
Inabainika Jesca alitoa taarifa za uongo. Kesho yake Jesca akaondoka guest akaelekea alipomfungulia mdogo wake duka. Kwa kipindi cha muda mrefu hawakuwa na mawasiliano, Jesca anafika pale anashangaa kuna mabadiliko. Dukani yupo mtu mgeni hata hamfahamu anauliza mwenye duka..๐Ÿ‘‡
Yuko wapi? Anaambiwa ndio mimi. Jesca anazidi kuchanganyikiwa? Anamuuliza ni Wewe kivipi? Hii ni biashara yangu nilimwachia mdogo wangu.
Jamaa anachela anamwambia Ooh wewe ndo Dada wa yule Mkamaria?
Jesca anauliza Mkamaria ndio nini?
Jamaa anatoka nje anampa kiti..๐Ÿ‘‡
Anamwambia Dada tulia kuna mambo mengi huenda huyajui. Anaanza kumhadithia mambo mengi mno. Anaanza, Ndugu yako alifikia hatua akanunua mpaka gari ambalo alinunua kwa pesa za Betting yaani alibashiri michezo akashinda pesa nyingi akanunua gari ila hai

Loading suggestions...