James Munisi
James Munisi

@NjiwaFLow

24 Tweets 1 reads Apr 06, 2023
MAJARIBIO 06 YA KUMUUA ADOLF HITLER—AMBAYO HAYAKUFANIKIWA.
#UZI
💨Imekuwa ikiripotiwa katika vyanzo kadhaa vya habari kwa muda sasa kuwa, April 30 ya mwaka 1945, ndiyo siku ambayo mwili na roho ya Adolf Hitler vilitengana akiwa pale Führerbunker, Berlin.
💨Inaaminika, mwamba Hitler alifayafikia maamuzi ya kuuondoa uhai wake baada ya kuona kuwa hakukuwa na uwezekano wa vikosi vyake kushinda katika ile ‘Battle of Berlin’. Hivyo kama kiongozi aliyekuwa na maono ya kuanzisha ‘Nazi Empire’ aliona hakukuwa na faida za yeye kuishi tena
💨Inaaminika pia, Hitler alijiua kwa kujifyatulia risasi kichwani, akiwa mbele ya mkewe bibie Eva Braun, ambaye naye alifuatia kujiua kwa kunywa sumu.
💨Wengine wanasema kuwa, baada ya kufa kwa wanandoa hao, miili yao ilikokotwa mpaka pale Shallow Crater,
…ambapo hapo ilichomwa, katika eneo hilo la bustani ya Reich Chancellery.
💨Kwenye maisha ya Hilter kuna mengi sana, na ndio maana ni mamia kama sio maelfu ya waandishi wameandika vitabu vingi juu ya maisha yake binafsi, na mitazamo yake ya kiutawala kwa ujumla.
💨Katika miaka 56 ya uhai wake juu ya sayari hii, Hitler alikoswa na mashambulio kadhaa ambayo yalikuwa yamelenga kuuondoa uhai wake. Leo tutayaangalia mashambulio sita pekee ambayo ndio yanatajwa sana katika nakala za waandishi mbalimbali walioandika kuhusu ‘Der Führer’, Hitler.
1. The Munich Beer Hall Melee Attempt.
💨 Hili ndilo lilikuwa shambulio la kwanza la kujaribu kuuondoa uhai wa mwamba Adolf Hitler, na lilifanyika miaka kama 20 hivi kabla ya vita ya pili ya dunia kupamba moto.
💨Nov 1921, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuundwa kwa ‘Nazi Party’,
Adolf Hitler aliambatana na baadhi ya viongozi wa chama chao hicho, mpaka pale Hofbräuhaus Beer Hall, ili akaseme na raia yale aliyokuwa ameyaandaa kwa ajili ya maslahi mapana ya chama chake.
💨Mkutano huo ulijumuisha wana demokrasia na baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa Hitler.
💨Nondo alizokuwa anazishusha Hitler kutoka kwenye hotuba yake, ziligeuka mwiba mkali kwa baadhi ya wale waliokuwa wakimsikiliza, hususan wale waliokuwa na mitazamo ya kisiasa tofauti na yeye.
💨Ghafla vurugu zilizuka mahala pale, risasi zikapigwa kuelekea alipokuwapo Hitler,
ila kwa bahati nzuri hakudhurika, na kisha shambulio hili liliendelea kimpa-mileage zaidi kwasababu watu walikuwa hawamfahamu Hitler kwa ukubwa huo hapo awali, ukizingatia hata chama chake cha Nazi kilikuwa bado ni kichanga, na hakikuwa na misuli imara ya kisiasa.
2. The Maurice Bavaud’s Plot.
💨Mwishoni mwa mwaka 1938, mwanafunzi wa theolojia kutoka kule Swiss, Maurice Bavaud alinunua pisto kwa ajili ya lengo moja tu la kumuua Führer, A.K.A Hitler.
💨Maurice alikuwa na madai ya kuwa Hitler alikuwa ni tishio kwa imani yake ya kikatoliki.
💨Hivyo, alilichukulia jukumu la kummaliza Hitler kuwa kama ni kazi yake ya kutekeleza maagizo ya kiroho anayoyasikia ndani mwake.
💨Maurice alipata nafasi hio November ya mwaka 1938, ambapo Hitler na wa-Nazi wengine walikuwa wakienda Beer Hall kwaajili ha hafla ya kukumbuka,
…kukoswa kwao kuuawa.
💨Alijitahidi kukaa sehemu nzuri kwa ajili ya kutekeleza azma yake hio, ila mazingira hayakuwa rafiki kwake. Na katika kughairi kwake na kisha kuondoka, alistukiwa na baadhi ya askari wa Hitler, wakati akijaribu kupanda treni.
💨Alikamatwa, na kisha May 1941 alihukumiwa kifo akiwa ndani ya gereza la “Berlin’s Plötzensee Prison”.
3. Georg Elser’s Beer Hall Bomb
💨Fundi mwashi aliyekuwa akifahamika kama Georg Elser, ndiye aliyesimamia huu mchongo wa hili jaribio.
💨November 1938, Elser alitegesha bomu pale pale, ‘Beer Hall’ ambapo Hitler alikuwa na ratiba ya kwenda kuhutubia wananchi wake, katika halfa ya kuenzi ile ‘Beer Hall Putsch’.
💨Kwa bahati nzuri, Hitler aliwahi kumaliza hotuba yake, na kisha akaondoka mapema, kabla ya mlipuko.
💨Bomu lililokuwa limetegeshwa na Elser ndani ya Beer Hall, lililipuka dakika 13 baada ya Hitler kuondoka, likiishia kuua watu nane na kujeruhi baadhi.
💨Elser alikamatwa wakati akijaribu kukimbilia Swiss, na kisha aliuawa mwaka 1945, mda mfupi kabla ya ukomo wa WWII.
4. Henning von Tresckow’s Brandy Bomb Attempt.
💨Huu mchongo ulisimamiwa na baadhi ya maafisa wa polisi wa Ujerumani.
💨Bomu lilitegeshwa katika ndege ya Hitler, ambayo alikuwa ikitarajiwa kuruka kutokea Smolensk kwenda Rastenburg, huko mashariki mwa Prussia.
💨Kinara wa mchongo huo alikuwa ni afande Tresckow na afande Fabian Von Schlabrendorff. Bomu lao halikuwa limesukika vizuri kwenye mfumo mzima wa muda wa ulipuliwaji wake, na hivyo Hitler akapona shambulio hilo kwasababu ya ‘Malfunction in the timing mechanisms of the bomb’.
5. Rudolf von Gertsdorff’s Suicide Mission.
💨Wiki moja baada ya kufeli kwa mpango mzima wa Tresckow, afande Rudolf von Gertsdorff’s naye akajaribu kutekeleza njama za kumuangamiza Hitler.
💨Ilikuwa ni March ya 1943, ambapo Rudolf alikuwa amepewa jukumu la kumpitisha Hilter,
katika maeneo kadhaa ya Jiji la Berlin na kumuonesha silaha ambazo zilikuwa zimekamatwa kutokea Urusi.
💨Mapango uliokuwepo ni wa Rudolf kutembea na briefcase ambayo ingekuwa na bomu, ili pindi amtembezapo Hitler ajitoe mhanga, ili wafe wote.
💨Baada ya taarifa kuenea kuwa kulikuwa ni shambulio la afisa usalama kuwa tayari kujitoa mhanga kwaajili ya kumuonda Hitler madarakani, wenye kuusoma upepo walimshauri Hitler kuwa, afanye kuimaliza tu vita na hata kuachia madaraka kiroho safi.
💨Ila kibishi mwanenu akakaza😁🤝
6. The July Plot/Operation Valkyrie.
💨Huu ulikuwa ni mpango mkakati serious kabisa wa kuua Hitler na kuiondoa Nazi madarakani.
💨Ulisimamiwa na Claus von Stauffenberg,kanali wa jeshi aliyepotezaga jicho moja na mkono wakati wa moja ya vita alizowahi kushiriki huko North Africa
💨July 20, mwaka 1944 Hitler alitegewa bomu katika chumba cha mkutano kule “Wolf’s Lair Hq”,
bomu liliripuka ila Hilter hakufariki, bali alipata majeraha kiasi.
💨Baada ya hilo kufeli, Claus na wenzake wakapanga kuleta mapinduzi ya kijeshi siku hio juu ya Hitler ( Op Valkyrie)
💨Likini wakawaiwa wao, Claus akakamatwa yeye pamoja na wenzake na kisha kuuawa kwa kupigwa risasi.
💨Haya mashambulio mawili ya mwisho (5 na 6) yalikuwa ni taarifa nzito sana kwa Hitler na waliokuwa nyuma yake. Na kuanzia hapo inasemekana kasi ya uongozi ya Hitler ilianza,
kupungua, kuonekana kwake mitaani na hata sehemu zake za kiofisi kukawa ni kwa nadra sana, kabla ya kujifyatulia risasi April 30 ya mwaka 1945.
💨Pumzika Führer, Adolf Hitler.

Loading suggestions...