M.D (πŸ…¨)
M.D (πŸ…¨)

@ReganTesla_

23 Tweets 5 reads May 30, 2023
Skia nikupe story yangu moja kuhusu jambo lile lile πŸ˜„.
Nilikutana na Binti mmoja hivi, nikawa na ukaribu nae akawa rafiki yangu sana ila siku akanieleza kuwa ananipenda. Mimi nilikuwa namtamani sana sema nilikuwa namuona kuwa sio Level yangu. So sikupenda kuathirishwa..πŸ‘‡
So nilikuwa nameza mate mchezo unaisha. Sasa yeye alivyokuja kuniambia ananipenda nikashtuka kwanza nikahisi anatania so nikaenda nae kwa utani utani. Bwana wee kumbe mwenzangu alikuwa serious tena kazama kweli kweli. Akawa ananipenda kiasi sasa tunakuwa na ugomvi kila wakati..πŸ‘‡
Sababu ya wivu, Alifikia hatua akawa ananiambia simpendi anajipendekeza kwangu n.k
Wakati huo sasa na mimi nikaanza kufungua moyo nikaona sasa ni serious sio utani tena. Tukawa Wapenzi tena wale Wapenzi walioiva kabisa yani. Wale Wapenzi walioshibana kweli kweli. Kutokana na..πŸ‘‡
Yake na yangu kuwa tofauti sana nikawa sijiamini sana. Yeye alikuwa ana maisha mimi ndo kwanzaaa tia maji tia maji. Sasa bwana alikuwa haniombi kitu wala haongelei masuala ya mimi kumpa chochote.
πŸ˜„ Sasa kasheshe likaanza, Nikiwa ndo kwanza nimefall in love akaanza kunipa..πŸ‘‡
Story za Ex wake. 😐 Katika hizo story akawa anataja sana mambo aliyokuwa akifanyiwa na jamaa. Mara anasema birthday yake alimpa milioni 2, Mara ananiambia aliwahi kumpa zawadi ya chain ya milioni yaani yeye story zake anataja milioni milioni tu. Eeeh πŸ˜‘ Mchaga mimi..πŸ‘‡
Nikaanza kupigwa na butwaa nikawa sasa nahisi ananisema kwa mafumbo. Nikamsikiliza kisha nikaweka akiba kichwani. Nakumbuka siku moja akaniambia ameagiza kuna mzigo fulani ameuona Kariakoo anaomba nikamchukulie. 😐 Hakunipa pesa nikajua nikifika labda nitalipia aftatu tu..πŸ‘‡πŸ˜
Nikaenda, Bwana wee kufika nikaambiwa nilipie 135,000. Eeh Regan nikaona nishadhalilika, nishafedheheshwa nishatia ukoo matopeni. Nikikumbuka mtoto yeye alikuwa akinipa vizawadi n.k yeye huwa hajali yani.. Basi nikapiga simu kwa Mwanangu sana nikamshirikisha. πŸ˜„Jamaa akaniambiaπŸ‘‡
Sasa kwa Level zetu wakati ule ile story ilikuwa kama kichekesho tu maana kipato kilikuwa haba. Kumwambia mtu inatakiwa ulipie 135,000 kitu wakati msosi tu unatusumbua ilikuwa kichekesho tu.
Basi nikajiongeza nikajisemea kuwa inabidi mimi niachane nae tu ili mambo yasiwe mengiπŸ‘‡
Akanipigia akaniuliza nishachukua? Nikamwambia sijachukua sababu sikuwa na pesa nikawa namlaumu kwanini hakunipanga?
Nae akaanza lawama kuwa simpendi na ndio maana simspoil chochote. Sasa mimi huwa sinaga kona kona nikamchana kuwa mimi hali yangu papatu papatu..πŸ‘‡
Tukazozana palee. Akasema niuache ataufuata mwenyewe. Nikaondoka baada ya hapo akanitext tuachane kwakuwa sitimizi wajibu wangu kwake. Basi kwa bahati nzuri sana mimi Mwanamke akisema Tuachane sinaga historia ya kumpinga, Nikamwambia basi sawa kama kuachana kutampa furaha..πŸ‘‡
Mimi namuunga mkono pia. Nikamwambia asije akaharibika uzuri wake sababu ya fala mmoja tu anaepambania mlo wake.
Akasema sawa sawa, Mimi nikajiona kabisa sub ilikuwa ya kulazimisha ila kiukweli mwendo niliumaliza, Game ilinizidia hvyo sikuona hata kama natakiwa kuumia..πŸ‘‡
Hapo ilikuwa mchana. Jioni ilipofika akanitumia Boooooonge moja la msg. Yaani kuubwa kama waraka wa Mtume Paulo kwa Wayahudi. Yaani msg unasoma mpaka unapunzika. Sasa humo ndani content ilikuwa ni lawama tupu Binti analalamika sikumpenda, anajuta kunifahamu, anateseka..πŸ‘‡
Na isingekuwa hvyo kama asingenijua. Akawa anasema mimi sikuwa namjali wala sikuona thamani yake. Akadai kuwa nilikiwa namfanya kama mpango kando tu inaonekana nina mtu wangu. Ila kusema ukweli wa Mungu wakati ule nilikuwaga na Girl wangu wa level yangu, huyo hatukuwa...πŸ‘‡
Na moto sana maana hakukuwa na jeuri ymπŸ˜„, Sikuwa na kitu nae hakuwa na kitu.
Basi akanilaumu sana mpaka nikajiskia vibaya. Ile msg sababu ilikuwa ndefu sana nikawa naisoma kwa muda mara ikaingia nyingine inasema "Umeona sasa? Unanidharau hata msg hunijibu"
Nikasema Yalaaaa..πŸ˜„πŸ‘‡
Penzi la namna gani hili mimi sijazoea bwana. πŸ˜„Kiukweli kabla yake sikuwahi kupenda na mtu vile.
Ukapita muda kidogo akapiga simu analia anaita tu jina langu.
πŸ™„ Hee asianze kusema kuwa kama akifa nilaumiwe mimi??
Nikasema Yarabiii hii ni ipi tena?
πŸ˜„ Nikampigia..πŸ‘‡
Nikamwambia asiseme tena maneno yale. Nikamwambia tukutane, Akaja tukazungumza nikamwambia ukweli kuwa ninae girl wangu ila sasa sikupata muda wa kumwambia mapema maana tulianza kama utani. Eeeh akaongeza kilio akaanza kusema unanikataa mimi sababu ni Maskini, maneno kibao..πŸ‘‡
πŸ˜„ Nikajichekea nikasema angejuaaaa, Yaani mimi namuona kama mtoto wa Waziri yeye anaeleta kujimaskinisha tena? Nikajichekea tu moyoni.
Basi bwana pale akasema yeye ananipenda mimi na alitania wala hakumaanisha tuachane alitaka tu nimbembeleze. Basi akaanza makiss na hug πŸ”₯πŸ”₯πŸ‘‡
Eeh sasa akaanza kuniuliza namtaka yeye au huyo Girl wangu. πŸ˜„πŸ˜„ Mimi mwehu kweli nikamwambia nawataka wote, nikaliwa kibao shwaaaaaa. πŸ˜‘ Akasema hataki kufananishwa na mtu yeye ananitaka mimi tu na hataki tena nimtaje huyo Girl wangu mbele yake. Nikamwmabia sawa..πŸ‘‡
Basi tukaendelea hvyo hvyo tu kibishi, sasa kwakuwa mimi niliona simmudu ilikuwa akitamka tu kuniacha mimi nasema Tawileee.
Maisha yakasonga nikawa situmii nguvu kubwa kwake akanipenda mpaka akapitiliza ikawa sasa anakuwa kama Mwehu.
Basi nikaishi nae ila kuna wakati..πŸ‘‡
Akaniletea dharau nikampiga block kila sehemu bila kumwambia chochote. Akahangaika akaja mpaka home nikamwambia aniache sipo. Mwisho bwana akaja akanipa pesa niende hospitali maana nilimwambia naumwa. Nikazikataa kisha nikampa facts kwanini simtaki. Alivyoona namtesa sana..πŸ‘‡
Akahamia Mwanza kwa ndugu zake akasema hataki tena kuishi karibu na mimi, Maisha yakaendelea mpaka sasa kila mtu anaishi maisha yake.
Sasa bhana katika story ya huyu Binti ndipo huwa napata picha kumbe bwana kweli Upendo wa kweli sometimes upo. Yule dada alinipenda sana..πŸ‘‡
Alikuwa hapati kitu kwangu ila alinipenda tu na alijitoa sana kwangu na hata mwisho akiniambia anaondoka sababu tu apate amani.
Ila kitu kingine nilichojifunza ni kuwa sisi vijana sometimes tunayumba. Kwanini umuogope Binti kisa huna pesa?
Sometimes we kuwa nae tu akupe hasira
Ya kutafuta ufikie mahali pajuu. Yule Binti page zake alizoandika kwangu ni nzuri sana na nazitumia kufanya masahihisho ya paper zangu za sasa.
True love ipo na haiamuliwi na pesa wala nini ni moyo tu ukifunguka...
πŸ‘ŠπŸ½ TUISHI.

Loading suggestions...