9 Tweets 4 reads Jun 17, 2023
Mtangazaji: Msikilizaji wetu ktk line Hallo!!
Mpigaji simu: Woi Woi Woi ni Mimi BINGWA WA KUUZA SIMU ORIJINO ZA SMARTPHONE KIGOMA NZIMA wananiita Francis Rutela KUTOKEA Stand kuu ya mabasi. Mambo vipi hapo studio!!
Mtangazaji: Safi kabisa Francis haya twende watu watatu
Mpigaji simu: Moja kwa moja namsalimia jamaa yangu Thadeo Yessaya aliyepo Lindi, Pili salam zangu zimwendee Yemughabo Yusto K. Yusto aliyepo Daslam hapo. Wa tatu na mwisho salam ziende kwa Dokta Dikson Maluli aliyepo Zenji.
Ujumbe: MAISHA BILA SMARTPHONE SAWA NA KAZI BILA UJIRA
Msikilizaji: Daaaahhh huyu Silvanus mbona kila siku anapiga simu? Ana vocha za kuchezea? ๐Ÿคท๐Ÿพโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿพโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿพโ€โ™‚๏ธ
You guys you don't know ujanja wa kupenetrate kwenye soko. ๐Ÿ˜‚
Sasa leo nataka nikusanue inawezekana hujui au hujawahi kuelewa.
Hii ni mbinu ya MARKETING AT NO COST
Kwanza shout-out kwa watangazaji wote ambao wako kwenye vipindi vya redio vinavyotuma salamu.
Maana Kuna watu wanajenga majina kwa njia ya urahisi. Mfano mzuri ni hapo juu.
Jamaa ametumia dakika 2 kujenga JINA, AINA YA BIASHARA, MAHALI ALIPO, alafu kwenye ujumbe kaweka TAGLINE
Hii ni marketing ya kimkakati sana yaani.
Utauliza kwanini...
Chukua glasi weka maji ya kunywa, kunywa taratibu... Huku unafikiria unakwama wapi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Hapana shaka wanaotuma salamu mara kwa mara ni wauzaji wazuri sana wa bidhaa zao. Kwa sababu ya kujenga majina yao.
Kitendo cha jina kusikika mara kwa mara, kinafanya Jina lako linase zaidi kichwani.
Nakumbuka nikiwa Mbeya, miaka ile Kuna redio moja ya dini inaitwa BARAKA FM, alikuwepo dada mmoja anaitwa Judith Chatila. Ilikuwa haipiti siku hajatamkwa wala hajajitaja.
Mpaka ilipelekea mimi kulishika sana jina lake ingawa simfahamu mpaka leo.
Okay, now nataka kusema, kama upo kwenye nafasi ya kubrand jina lako kuna some hole chances hutokea. Na unahitaji umakini sana kujua.
Huyu jamaa anajitangaza ili wale watu watatu ni kama kibebeo tu
Jina lake likikaa sana katika akili za watu, hata wakiona Bango pale stendi wataenda kupata huduma Moja kwa moja.
Kwanini? Kwa sababu
1. Watataka kumjua Francis ni yupi.
2. Wanunue ili jamaa awapeperushe kwenye redio.
3. Wametokea tu kumuamini kwa kutajataja kupitia redio
Jamani vitu vingine havihitaji BACHELA, MASTAZ WALA PIHECHIDII. Ni ubunifu tuu.
Sema Nini shout-out sanaa kwa wanangu WAHA ninyi na redio kama mlizaliwa pamoja ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Nawakubali miaka buku, hamkawii kubishana na watangazaji hasa morali za salamu zikipanda.
Hope you've enjoyed ๐Ÿงต

Loading suggestions...