26 Tweets 13 reads Jun 23, 2023
Five people have been confirmed dead inside OceanGate Titan.
Sijui mitambo ilizima ghafla ama wamepigwa na dhoruba kali ila mimi na wewe hatujui kimewapata kitu gani.
Najua unajiuliza kuna nini au kina nani hao.?
Don't worry step by step you'll understand.πŸ‘‡
Usiku wa tar14-04-1912
Meli ya TITANIC ikiwa na abilia zaidi ya 2000 ilikuwa ikikatisha bahari ya Antlantic kutokea Uingereza kwenda mji wa New York, Marekani
Usiku huu haukuwa mzuri kwa safari ya meli hii, dhoruba likatokea meli ikazama na kuua zaidi ya watu 1500
Kisha watuπŸ‘‡
kadhaa wakaokolewa wakiwa wazima, huku makampuni tofauti yakijitokeza kuchunguza sababu za kuzama kwa meli hiyo..
Na zaidi swala la kuyapata mabaki ya meli hiyo likabaki kitendawili.
Miaka ikakatika na ilipofika Septemba 1985 kwa mara ya kwanza mabaki ya meli ya TITANICπŸ‘‡
yakagundulika yako eneo la kina kirefu cha bahari ya Antlantic.
Deep sea....
Baada ya eneo kugundulika
Watu wakawa na shahuku ya kufika eneo hilo ili wajionee kwa macho yao mabaki ya meli ya TITANIC.
Si rahisi kukaribia eneo hilo, sasa makampuni ya uokoaji yakaanzaπŸ‘‡
Kutengeneza vifaa vya kujiokolea, Nchi nazo zili jizatiti juu ya ulinzi wa majini na angani.
Wataalam pia waliwaza kupata vyombo imara zaidi, kupiga mbizi mpaka kwenye meli ya TITANIC.
Ndipo zikapatikana kwa wingi Submarine na Aircraft Carrier.
SubmarineπŸ‘‡ Aircraft CarrierπŸ‘‡
Aircraft Carrier ni zile meli kubwa ambazo huweka kambi baharini kwa ajili ya shughuli za kivita, kishwahili huitwa manowari.
Sasa hizi tuachane nazo zitatutoa kwenye njia.πŸ‘‡
Sisi tunyooke na Submarine..
Kwa kiswahili tunaita nyambizi. Hizi huzama chini kabisa ya bahari.
Zikiwa chini ya bahari "Deep sea" zinaweza kurusha mabomu kuja juu ya bahari na kwenda umbali umrefu zaidi kwa target maalum.
Sasa hiziπŸ‘‡
Pia ziko aina nyingi, kuna kubwa kabisa ambazo ukiingia huwezi kuona kilichopo nje kwa macho ya kawaida isipokuwa kwa computer.
Shida ya hizi kubwa huwa kuna maeneo haziwezi kupita na huwa hazina speed kubwa.
Sasa hapa ndipo zikaundwa Submersibles ambazo hiziπŸ‘‡
huwa ni ndogo zaidi, ndani yake wanakaa watu wawili mpaka wa3. Pia zingine huwa kwa mfumo wa roboti ambazo hutumwa kwenda umbali kadhaa kurekodi taarifa na kukusanya data muhimu.
Hizi unaweza kuziita nyambizi ndogo.
Sasa hapa ndipo tunapokutana na bwanaπŸ‘‡
STOCKTON RUSH ambaye alizaliwa mwaka 1962 huko marekani.
Hiyo inaleta maana kuwa mpaka mwaka 1985 mabaki ya meli ya TITANIC yanagundulika yeye tayari alikuwa na miaka 25.
Bwana huyu akaichungulia fursa kwenye kutumia vinyambizi vidogo kwenda kwenye meli ya TITANIC kama sehemuπŸ‘‡
ya utalii, akiwa chuo akasoma sana maswala ya maji kuogelea na uokoaji mara aliingia kwenye US Navy, hakukaa huko akajikita zaidi kwenye biashara.
Mwisho akaja na mpango wa kufungua kampuni yake, akafungua na kuipa jina la TITANIC SURVEY EXPEDITION
Lakini bado alikula msotoπŸ‘‡
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 kuja juu tayari makampuni kadhaa yalisha tengeneza nyambizi imara na picha za mabaki ya meli ya TITANIC zilianza kupatikana kwa muonekano mzuri.
Kwenye picha hizo meli ya TITANIC ilionekana ikiwa chakavu sana, kwenye kina kirefuπŸ‘‡
kwenye sakafu ya bahari yaani meli ya TITANIC imezama, imegota kwenye ardhi ya bahari "seafloor"
Meli ilikutwa kwa mtindo wa vipande viwili huku sahani zilizokuwa sehemu ya mgawawa wa meli hiyo zilikutwa zimedondoka chini na kupangana bila kuvunjika.
Lakini piaπŸ‘‡
bathtub, jakuzi au bafu la kuogea huku unamwagilia moyo bafu hilo pia lilitazamika likiwa salama na lenye ubora.
Nikitendo kinachoshangaza na kuvutia.
Bwana STOCKTON RUSH alivurugwa aliposikia na kuona picha hizo kiu yake ya kuisimamia kampuni yake ikaongezekaπŸ‘‡
Miaka ikakatika ilipofika mwaka 2009 ndipo STOCKTON RUSH akafanikiwa kuunda nyambizi yake na akaiita kwa jina la OceanGate.
Submarine hii ya STOCKTON RUSH ilikuwa ni tofauti kabisa na nyingine zote.
Hii akaiunda kwa mfano wa ndege ya angani na zaidi mbele kuna kioo kikubwaπŸ‘‡
chenye mfano wa jicho la binadamu lakini pia utofauti wa chombo hiki kikawa na uwezo wa kubeba watu 5 na speed kubwa zaidi.
Mkiwa ndani ya chombo hicho mnaweza kukaa siku4 ndio Oxygen itaisha, it means Oxygen ikiisha na nyinyi shughuli yenu inaisha maana huko chini ya bahariπŸ‘‡
Hakuna hewa kama hii tunayovuta sisi.
hii ikaenda, taratiibu OceanGate kikaanza kujulikana na kampuni ya TITANIC SURVEY EXPEDITION ikazidi kuwa maarufu kupitia Submersibles "Nyambizi" yake yenye jina la OceanGate
Kwakifupi jamaa alichanga karata zake vyemaπŸ‘‡
Mwaka 2016 dunia ilianza kuwajua baada ya kuzama chini ya bahari na kwenda mpaka ilipo meli ya TITANIC na kupiga picha nzuri zilizowavutia watu wengine.
From there watu wengi wenye hadhi za juu walipenda kwenda kutalii kwenya meli ya TITANIC kwa kutumia kampuni yaπŸ‘‡
TITANIC SURVEY EXPEDITION kupitia usafiri wake wa OceanGate.
Viongozi wakubwa na wafanya biashara wakubwa duniani walikwenda huko kupitia OceanGate.
Alikuwa akiwatoza dollar 250,000 ni pesa nyingi mnoo, na ndio maana pengine ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingiπŸ‘‡
Na ili kuwaaminisha wateja wake STOCKTON RUSH katika safari zote yeye mwenyewe pia alikuwa anaenda mpaka yalipo mabaki ya meli ya TITANIC kisha wanarudi pamoja.
Baada ya kufanya dhiara hizo za utalii mfanyakazi wake alihoji ni Vipi ikiwa siku chombo kitapata ajaliπŸ‘‡
Swali ambalo STOCKTON RUSH hakulitolea ufafanuzi wa kutosha.
Mfanyakazi huyo aliyetambulika kwa jina la David Lochridge alihoji kama utani ila siku kadri zilivyokwenda akajikuta anarudia Swali hilo mara kwa mara.
Alisikika akisema...
Kampuni hiyo inahitaji kifaa kingineπŸ‘‡
Madhubuti kwa ajili ya uokoaji haraka iwezekanavyo kabla ya kuendelea kufanya ziara za utalii huo.
Alihoji sana mwisho akawa kero kwa bosi akafukuzwa kazi..
Baada ya kufukuzwa kazi bado akawa anawasihi wafanyakazi wa kampuni hiyo wamuhoji Bosi wao kuhusu hilo.πŸ‘‡
Mr CEO STOCKTON RUSH akaona hii sasa dharau, akampeleka mahakamani na kumshitaki bwana David Lochridge kwa kuwasumbua wafanyakazi wake.
David Lochridge Akaamua kupiga kimya huku akiwaonya juu ya jambo hilo.
Ilipofika tar18-06-2023 ndipo Mr CEO STOCKTON RUSH akiwa naπŸ‘‡
Watu wengine wa4 kwa maana jumla ni watu wa5. Wakafunga safari ya kwenda kutalii kwenye mabaki ya meli ya TITANIC, kama wafanyavyo siku zote.
But hawakujua safari hii ilikuwa ni safari mbaya kwao, wakapotea na kutokomea huko, Mpaka siku ya tar22-06-2023πŸ‘‡
waokoaji walipothibitisha kuvipata vipande vya chombo hicho cha OceanGate, Mr CEO STOCKTON RUSH amemezwa na ndoto yake.
Wengine walio fariki katika ajali hiyo ni..
Hamish Harding
"bilionea wa Uingereza na mmiliki wa Action Aviation"
Paul Henry Nargeolet
"mtaalamu waπŸ‘‡
kupiga mbizi Mfaransa"
Shahzada Dawood
"mfanyabiashara mashuhuri wa Pakistani"
Suleman Dawood
"mtoto wa Shahzada Dawood mwenye umri wa miaka 19"
Bahari ni kiza kinene.
#RIP
Stay safe kwa ground mambo ni mengi sanaπŸ™
Usiache kunifollow as @wisdomjaykwa #wisdomjaykwa

Loading suggestions...