HabariTech
HabariTech

@HabariTech

12 Tweets 4 reads Jul 03, 2023
⚡5G Inastahili Sifa na Hype Inayopewa? Na Inafanya Vipi Kazi?
Tangu kutangazwa kwake 5G imepata attention kubwa sana na kampuni za mitandao zote wanatamani kuwa nayo ili kuvutia wateja.
⚡Kitu nilikaa najiuliza tangu kutangazwa kwake ni kama 5G ni teknolojia ambayo imetolewa kwa wakati sahihi.
Nikifikiria katika elimu ndogo ya physics kuhusu mawimbi ya 5G sioni 5G ikifanya vizuri hasa hapa kwetu Tanzania.
⚡Hii naangalia na uhalisia wa mtandao wa 4G namna coverage yake imekuwa ya kusuasua.
Kabla hujasema kwamba simu yako haipati 5G ni vyema ukumbuke kwamba 5G sio ishu ya software update.
habaritechtz.com
⚡Sio kwamba utafanya update ya system ya simu yako ili upate 5G, na mtu yeyote akikwambia inawezekana kwa kufanya hivyo basi anakuongopea.
Kwa ajili ya uelewa ni vyema ufahamu maana ya 5G.
⚡5G ni nini?
Mpaka miaka miwili iliyopita tulikuwa na mtandao wa 4G peke yake ambao huo ni mtandao wa kizazi cha 4 tangu kuanza kutumia mitandao isiyotumia waya (wireless networks).
habaritechtz.com
⚡Wataalamu walitulia na kufanya tafiti wakaona kwamba kizazi hiki bado kina spidi ndogo ukilinganisha na mahitaji ya watu.
Hivyo wakaanza kutengeneza kizazi cha 5 cha mtandao ambacho kinaitwa 5G.
habaritechtz.com
⚡Na kizazi hiki mpaka sasa kina kampuni na simu chache ambazo zinaweza kutumia mtandao huu.
Katika nadharia inasemekana 5G iko haraka zaidi ya 4G mara 100. Kwa maana hiyo kwa anayepata 1Mbps kwenye 4G akitumia 5G atapata 100Mbps.
habaritechtz.com
⚡Kitaalamu 5G ni mawimbi ya high frequency na wavelength fupi. Wakati 4G inakuwa na frequency ndogo na wavelength kubwa.
Frequency ni sawa na kusema kama una duara lenye mzungo wa mita 10, uwezo wako wa kuzunguka hili duara lote ndani ya sekunde moja ndiyo frequency.
⚡Kwamba tukisema una frequency ya 10Hz basi unaweza kuzunguka hili duara mara 10 ndani ya sekunde moja.
Wavelength ni umbali kati mawimbi mawili ukipima kutoka kima cha juu kabisa cha wimbi la kwanza kwenda kima cha juu kabisa cha wimbi la pili.
habaritechtz.com
⚡Sasa 4G unaweza kuitumia kwa umbali hati wa mita 100 au 500 bila shida kwa kuwa ina wavelength kubwa na frequency ndogo,
lakini 5G haiwezi kufanya hivyo kwa sababu ina wavelenght ndogo. Wavelength inapozidi kuwa ndogo ndivyo ambavyo uwezo wa mawimbi kwenda mbali unapungua
⚡Na hata uwezo wa kupenyeza kwenye baadhi ya vitu unapungua.
Mfano kwa mtu aliyetumia Oven au Microwave ushawahi kujiuliza kwanini lile joto la mle ndani halitoki nje? Sababu ni hiyo kwamba lina wavelength ndogo sana hivyo haliweza kupenyeza kutoka nje ya kuta za hiyo microwave
⚡Na hizi limits za Elon Musk humu twitter bado unataka kusoma uzi wote hapa umalize tweets zote za leo? 😁😁
Cha kufanya tembelea hii link hapa chini usome uzi wote katika blog yetu
habaritechtz.com

Loading suggestions...