Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania

@radiomariatz

3 Tweets 17 reads Jul 14, 2023
Sala ya kuomba Mchumba Mwema:
Ee mwumba wetu, umewaunganisha watu katika ndoa takatifu nami natumaini kupokea Sakramenti hiyo na kushirikiana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote.
Kwa hiyo nakuomba ee Bwana unisaidie kuchagua kwa hekima, nipate mchumba mwema, safi na mwaminifu, nifuate zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso, zaidi tabia njema kuliko umaridadi.
Mioyo yetu iwe ya kulingana, na nia zetu zipatane, tupate kuishi pamoja na amani na kulea jamaa zetu kwa kukuheshimu wewe na baraka zako Amina.
radiomaria.co.tz
#RadioMariaTz

Loading suggestions...