ALLY MSANGI
ALLY MSANGI

@ally_eh

50 Tweets 19 reads Jul 08, 2022
Fursa ni kama embe, wakati wewe unalisubiri liive lidondoke, wengine wanalifuata mtini likiwa bichi na wanalila kwa chumvi.
Nina kuletea "Fursa 10 za mtandaoni zinazo weza kukuingizia kipato mtandaoni".
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa Fursa ziko nyingi sana, ni jinsi tu ya wewe kuzijua na kuzifanyia kazi.
Basi ungana na mimi tuzichambue hapa ndani ya thread hii.
Iwe ndio unaanza kufanya biashara ya mtandaoni, au unauza ujuzi wako (Freelancing) au ni mwajiriwa basi kuna njia nyingi sana za kukuingizia kipato mtandaoni.
Katika mwongozo huu nitatoa njia 10 bora zaidi za kutengeneza pesa mtandaoni na hatua kadhaa za vitendo unazoweza kuchukua ili kuanza.
Hayaa twende pamoja kuzichambua fursa hizi.
1. Pata pesa kama mwandishi (Content Writer)
Hii mimi naifanya sana, na imenipatia pesa nyingi tu.
Hapa tuna zungumzia uandishi wa aina nyingi mfano; Articles mbali mbali, blog post, makala za social media na zinginezo.
Ili uweze kuwa mwandishi mzuri utahitaji kukuza ustadi wako na kuwa na vigezo vifuatavyo.
- Ujuzi wa kuandika
- Ujuzi wa kutambua maneno muhimu (Keyword)
- Ujuzi wa SEO
- Ujuzi wa uchambuzi
Kwa walio somea journalism, marketing au mass communications hii kwao inaweza kuwa ni rahisi tu na kuna fursa kibao tu mtandaoni kwa wenye ujuzi wa kuandika.
Ukitaka kuwa mwandishi ni vizuri zaidi ukawa na website/blog yako, hii itakusaidia kukuza ujuzi wako zaidi na
inaweza kutumika kama mahali pa kuuza huduma zako wakati unatafuta kupata kazi au wateja wa kujitegemea.
Mfano mimi nina blog ya Kidigitali.com hapa ndio uwanja wangu wa kuandika kila ninacho jiskia kuandika.
Content writers Mtandaoni asilimia kubwa wana lipwa kuanzia $0.04 hadi $0.50 kwa neno moja. (mfano umeandika makala yenye maneno 1,000 *$0.04 = $40)
2. Uza ujuzi wako kwenye mitandao ya freelancing
Basi hebu tuzame kwa jinsi wewe pia unaweza kupata pesa kwa kufanya freelancing.
Hii ni kuuza ujuzi ulio nao kwenye platform mbali mbali. Mf. Upwork, Fiverr na zinginezo maana ziko nyingi sana.
Unachotakiwa kufanya ni kujisajili huko.
Tengeneza profile yako kisha ainisha ujuzi ulio nao na watu wata nunua ujuzi wako na utajipatia pesa.
Kama uta tumia Upwork, basi hakikisha kazi zote zinazo tangazwa na unaona una uwezo wakulifanya tuma maombi na hakikisha una andika maombi yako vizuri maana kuna ushindani pia.
Kujifunza zaidi jinsi ya kujiunga na namna unavyo weza kuzitumia hizi freelancing platforms pitia - kidigitali.com nimekuwekea mwongozo mzuri zaidi.
Au soma makala za @mafolebaraka ana andika sana kuhusu freelancing na unaweza nunua kitabu chake uka jifunza pia Namna ya kuanza kuuza ujuzi Upwork.
Ujuzi gani unaweza kuuza kwenye hii mitandao.
@mafolebaraka - Kutafsiri lugha (Huku kuna watu wana hitaji watu wa kutafsiri mpaka kilugha chako na wanakulipa)
- Uandishi wa makala
- Kuendesha social media account za watu
- Watengenezaji wa Graphics
- Na vingine vingi tu
3. Kuwa mtaalam wa SEO na uuze huduma za SEO
@mafolebaraka Kwanza SEO ni nini? SEO - "Search engine optimization": Ni mchakato wa kufanya tovuti iweze kutambuliwa na injini za utafutaji (Mfano, Google).
SEO ni moja ya maeneo muhimu zaidi katika uuzaji wa mtandaoni kwa kuwa inaweza kuwa muhimu katika majukumu mbali mbali.
@mafolebaraka Kama mtaalam wa SEO, unaweza kuuza huduma zako kwa wateja wasio na ujuzi katika suala hili.
Ili kuwa mtaalam wa SEO, utahitaji kwanza kuelewa jinsi injini za utaftaji kama google, bing na zinginezo zinavyofanya kazi.
@mafolebaraka Ili upate kipato kwa kufanya SEO unaweza kujisajili kwenye freelancing platforms na kuuza huu ujuzi. Pia una weza kuunda website yako na ukajinadi kuuza huduma hizi pia.
Wajuzi wa SEO wana lipwa kiasi gani?
@mafolebaraka Kiwango cha wastani kwa saa kwa wataalamu wa SEO ni kati ya $15 - $125.
Bei hutofautiana pia kwa kila nchi na uzoefu pia. Unaweza kujifunza SEO na ukawa expert na kuuza ujuzi huu sehemu kama Fiverr maana huko ndiko unauzika mnoo.
@mafolebaraka 4. Pata pesa kwa uuzaji wa ushirika "Affiliate Marketing"
Uuzaji wa ushirika "Affiliate Marketing" ni mfano wa biashara ambapo unapata gawio (commissions) kwa kufanya mauzo ya bidhaa za watu wengine.
Mchakato huo uko hivi...
@mafolebaraka Unachagua bidhaa unazotaka kukuza, na kuzitangaza kwa watu wengine na wanapo vutiwa na bidhaa hizo
wakinunua wewe unalipwa kwa kusaidia mauzo.
Basi nikujuze tu, haijalishi kama una website au hauna.
@mafolebaraka unaweza kutumia social media account zako ku tangaza affiliates na ukapata gawio.
Nikujuze tu Kuna kitu kinaitwa #TwitterMoney kuna vijana wana jiingizia kipato mpaka $5,000+ kila mwezi kwa kuuza courses za Gumroad.
@mafolebaraka Vijana hawa wana lipwa asilimia 50% ya kila wanacho saidia kuuza.
5. Pata pesa kwa kuuza matangazo kwenye blog
Hapa sasa ndipo pale ninapo imba sana wimbo wa anzisha blog yako.
@mafolebaraka Kuendesha matangazo kwenye wavuti (Website/blog) yako ni njia maarufu ya kuchuma mapato mtandaoni kupitia watembeleaji wa tovuti yako.
Unda blog yako, chagua topic (Niche) ya blog yako tengeneza maudhui kisha sambaza kwa watu. ukisha pata traffic nzuri jiunge na Network
@mafolebaraka za matangazo mfano, Google Adsense, Adsterra Network, Media.net, Propeller Ads na zinginezo.
Kadri unavyo pata watembeleaji wengi zaidi ndivyo unajiwekea nafasi ya kupata pesa nyingi pia.
@mafolebaraka Kuna website ukiingia utaona matangazo ya Adsense na kila mwezi wana uhakika wa kulipwa pesa kutokana na matangazo tu.
Nimekuandalia course ya 👉 blogging for beginners itakusaidia kama unataka kufanya blogging (Itapatikanda ndani ya jukwaa la @AfricaGetpaid
@mafolebaraka @AfricaGetpaid 6. Unda na uuze bidhaa zako mtandaoni.
Hapa sasa ndipo kuna pesa. Kama asemavyo Amos Nyanda jifunze kuuza.
Kwa msio mjua Amos, ni mtaalamu wa copywriting kwa hapa Tanzania.
Unaweza nunua na kusoma ebooks zake pia
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Basi ukijua kuuza na ukawa na bidhaa yako mtandaoni kuna pesa inakusubiria.
Ni vitu gani unaweza kuuza mtandaoni?
Uza E-books, Courses mbali mbali, au hata bidhaa zako za dukani ziweke mtandaoni kuna soko kubwa sana
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Sasa hivi kuna fursa ya platform za hapa hapa kwetu kama Getpaid Community weka bidhaa zako hapa na uanze kuuza.
Jifunze pia namna yakutumia Facebook Ads Manager kutangaza bidhaa zako zaidi na kuwafikia watu wengi.
7. Kuwa mshirika wa matangazo wa YouTube
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Ikiwa unataka kupata pesa mtandaoni kupitia video unaweza kuunda chaneli ya youtube na kuwa mshirika wa matangazo.
Mchakato wa kupata akaunti ya youtube ni mrahisi sana tu.
Unaunda akaunti yako kwa kutumia email ya gmail na kuchapisha video
@mafolebaraka @AfricaGetpaid kwenye hiyo chaneli yako na kukuza watazamaji wa video zako ili kujenga hadhira kisha omba matangazo uwe mshirika wa Youtube "YouTube advertising partner".
Kila wakati video yako inapo tazamwa aina tofauti ya matangazo yataonyeshwa.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Na endapo mtu anapotazama au kubofya tangazo kwenye video yako, utazalisha mapato na kulipwa ukifikisha $100.
Mfano mzuri ni kama wafanyavyo akima Millardayo, SNS, na wengine wengi tu.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Kumbuka Ili kuidhinishwa kama mshirika wa matangazo utahitaji kutimiza mahitaji yafuatayo:
- Fuata sera zote za YouTube (YouTube monetization policies).
- Uwe katika nchi ambayo Programu ya Washirika wa YouTube inapatikana.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid - Uwe na zaidi ya saa 4,000 halali za utazamaji wa video zako katika miezi 12 iliyopita.
- Akaunti yako ina zaidi ya wanachama (subscribers) 1,000
- Una akaunti iliyounganishwa ya AdSense.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Kwa wastani, washirika wa Youtube huingiza kati ya $ 0.01 hadi $ 0.03 kwa mwonekano wa tangazo (Inategemeana na inchi ya mtazamaji).
Hii inafikia mahali fulani kati ya $3 hadi $5 kwa mitazamo (views) 1,000 ya video.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Muhimu zaidi, unahitaji kupata idadi kubwa ya mitazamo ya video ili kupata mapato makubwa na Youtube.
8. APP Monetization (Google Admob na Facebook Audience)
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Huku kuna pesa sana, naposema hivi namaanisha sababu nimesha fanya na nimepata pesa nyingi tu kupitia matangazo ya kwenye Application za simu.
Najua unajiuliza inafanyikaje?
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Iko hivi kampuni ya Google na Facebook wana mifumo yao ya kuweka matangazo kwa watu wenye application za simu.
Unachotakiwa ni kujisajili na huduma hizo tu.
Kwa Google ni Admob na Facebook ni Facebook Audience kwa Developers.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Unacho takiwa kufanya ni kutafuta mtu mwenye uwezo kwa kuunda application za simu na kukutengenezea APP na kuiwekea matangazo.
Muhimu hakikisha app yako ina lenga watu gani na iwe na content unazo weka kila mara.
Nitumie mfano wangu halisi.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Mimi niliunda App ya ajira za DUBAI kisha nikaweka matangazo ya Facebook. (Unaweza kujiuliza kwanini DUBAI na mimi niko Tanzania)
Hapa kikubwa ni soko unalo likusudia na lina pesa kiasi gani.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Baada ya kupata "NICHE" na app tayari, Nilicho fanya nikutumia Facebook ads manager ku tangaza app yangu kwa watu wa dubai.
Ukiweka tangazo lako la $10 kwa siku na ukapata app Installs hukosi kuinigiza $50 kuendelea kila siku.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid 9. Social Media Influencer
Kunamtazamo wa baadhi wana hisi ili uwe Social media influencer ni lazima uwe na followes wengi la si hivyo.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Ushawishi wako kwenye bidhaa fulani au engagement unayo ipata kupitia account yako ina weza kabisa kukufanya ukawa na ushawishi na kutangaza bishaa au brand za kampuni yoyote ile.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid Mfano mzuri ni @JemsiMunisi @NjiwaFLow unapo ongelea kuhusu simu za Xiaomi au OPPO twitter basi ukurasa wake ndio unakuja kichwani haraka zaidi.
Ametengeneza umahili kwenye eneo hilo na ushawishi wake una aminiwa na wengi.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow Unapo ongelea freelancing basi jina la @mafolebaraka na @ally_eh litakuja kwa haraka zaidi, ukija kwenye Digital Marketing kuna @Gillsaint
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt 10. Forex Trading/ Cryptocurrency
Mfano mzuri na rahisi ni @Sirjeff_D jinsi alivyo fanikiwa kupitia Forex trading, kuna watu kama @MaujanjaCrypto na @NNgailo waliyo jikita kwenye crypto currency.
Kikubwa na muhimu ni ujuzi tu.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt @Sirjeff_D @MaujanjaCrypto @NNgailo Leo hii kuna vijana wanaishi kwa pesa za Forex trading na wana maisha mazuri sana
Leo hii unaona jinsi bitcoin ilivyo kuwa na thamani, kuna vijana wana invest kwenye pesa za mtandaoni kwa kununua coin mbali mbali na kupata faida pale zinapo panda thamani.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt @Sirjeff_D @MaujanjaCrypto @NNgailo Nawewe pia unaweza anza kufanya investment kwenye crypto (Ila muhimu fanya utafiti kwanza)
Unaweza kununua XLM au USDC hapa hapa ndani ya Getpaid Africa.
Ila kumbuka kabla huja fanya hivyo soma kwanza na ufanye tafiti.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt @Sirjeff_D @MaujanjaCrypto @NNgailo Ili kuwa safe zaidi ni bora kuwa na stablecoins kama USDC.
Mwisho kabisa.
Kuna fursa nyingi sana online, kikubwa ni ujuzi na kujua fursa ziko wapi.
Usikimbilie kila kitu chagua vitu vichache wekeza nguvu zako zote na elimu juu ya hivyo vitu kisha tengenza pesa.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt @Sirjeff_D @MaujanjaCrypto @NNgailo Kumbuka hakuna kitu rahisi au pesa ya haraka haraka, kila kitu kina chukua muda na kujifunza zaidi.
Niwatakieni siku njema na usiache kuni follow @ally_eh na tembelea kidigitali.com kwa kujifunza zaidi.
@mafolebaraka @AfricaGetpaid @JemsiMunisi @NjiwaFLow @GillsaInt @Sirjeff_D @MaujanjaCrypto @NNgailo That's a wrap!
If you enjoyed this thread:
1. Follow me @ally_eh for more of these
2. RT the tweet below to share this thread with your audience

Loading suggestions...